Anakula kuku na mayai yake mpaka mfuga kuku kashtukia dili...

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Kuna mtu anaomba msaada wenu. Yeye anajuta kuwa na uhusiano na mke wa mtu. Kwani sasa maji yamefika shingoni. Amekuwa katika uhusiano wa siri kwa zaidi ya miaka 4, na cha ajabu kwa jinsi alivyozoeana na familia ya huyo mama kuna siku mambo yalienda vibaya kwani alikula hata mtoto wa mama huyo mwenye umri wa miaka 19. Mtoto huyo amenogewa sana na huyo jamaa anashindwa kumudu mahusiano kwa mama na mtoto huyo kwani mtoto hajui kama jamaa huyo anamega mama yake! Ajabu ni kwamba hivi majuzi mambo yameharibika baina ya mama na mtoto baada ya kuujua ukweli (pia baba wa mtoto na mume wa mama huyo ameujua ukweli). Huyu jamaa yuko hatarini sasa kwani mume wa huyo mama ametishia kulipiza kisasi! Je, afanyeje kwani haoni pa kuificha sura yake!
 
Sina namna ambayo ninaweza kumuelezea jamaa huyo kwani Ms!@#":><*& na hastahili kuishi na jamii. Hebu fikiria athari za mahusiaono hayo ie kama katika kipindi hicho mke wa watu huyo amezaa mtoto inakuwaje?? Jee yule mtoto wa kike angepata mimba ingekuwaje?? Uwezekano wa ndoa ya huyo mama kuharibika ni mkubwa tu jee haoni kuwa yeye ndiyo chanzo cha kusambaratisha ndoa hiyo??? Hivyo ajitayarishe kwa lolote lile kutoka kwa mume hata kama ikibidi kumnyofoa m"|+o ni halali tu kwani huyo jamaa yako hafai kuwa mwanajamii ni sawa na kuku tu
 
Ntungila nunshiwakwe, anenkuzolya mumpishi zyose..inkuku nu twana twakwe!...Amassongelo gipasa mushitundu...! Huyu jamaa akilizake si nzuri eeh!..Hata mimi ningekuwa ndo mwenye mali hizo namshikisha ukuta..huh!
 
...Kule kwetu saa hizi tayari tumeshamvalisha gauni huyo anakata mitaaa!!!
 
Kuna mtu anaomba msaada wenu. Yeye anajuta kuwa na uhusiano na mke wa mtu. Kwani sasa maji yamefika shingoni. Amekuwa katika uhusiano wa siri kwa zaidi ya miaka 4, na cha ajabu kwa jinsi alivyozoeana na familia ya huyo mama kuna siku mambo yalienda vibaya kwani alikula hata mtoto wa mama huyo mwenye umri wa miaka 19. Mtoto huyo amenogewa sana na huyo jamaa anashindwa kumudu mahusiano kwa mama na mtoto huyo kwani mtoto hajui kama jamaa huyo anamega mama yake! Ajabu ni kwamba hivi majuzi mambo yameharibika baina ya mama na mtoto baada ya kuujua ukweli (pia baba wa mtoto na mume wa mama huyo ameujua ukweli). Huyu jamaa yuko hatarini sasa kwani mume wa huyo mama ametishia kulipiza kisasi! Je, afanyeje kwani haoni pa kuificha sura yake!

jamaa inabidi aombe msamaha na kutubu makosa yake
 
Kimsingi huyo akimbie nchi kwa muda aje huku upepo upite kwanza

Malipo ni humu humu duniani...hata aende kona gani, lakini bado chanzo cha yote ni huyo mama, yeye angekua anajiheshimu isingefika hapo. kama jamaa hajaoa then anakua hana tuhuma sana kama huyo mama, na huyo mtoto wala hausiki coz yawezekana alijua ndo kapata mume hapo....

so huyo mama na huyo jamaa wote ni MICHARUKO TU...huwezi kwenda kumtokea mke wa mtu, na wewe mama huwezi kukubali kugawa u-house kwa mtu mwingine.
 
Mshahara wa dhambi ni.... hana cha kujificha mnafiki mkubwa,watu wengine bwana unataka mtu kama huyo eti afanyeje tumsaidie kwa yapi mazuri zaidi ya kuharibu nyumba ya mwanaume mwenzake,hasitahili hata kidogo kuwa mmoja wetu katika jamii huyo ni sawa na mchawi akila nyama ya mtu hataacha nawewe rafiki yake atakugeuka,achana naye asubiri yatakayompata kutesa kwa zamu
 
Makosa yameshatokea na kwa kuwa maisha ni lazima yaendelee tunapaswa kusema chochote katika hili ili jamii iwe na rejea wakati mwingine likitokea. Kwani hata sheria za uingereza (common laws) zilitungwa kutokana na mazoea na tabia za watu na maisha yao, yakiwemo makosa.

Ushauri: Huyo jamaa naturally ni mchafuzi wa mazingira na ni mtu ambaye ki maadili huwezi kumuwekea dhamana kwani waswahili wanasema mwenzako akinyolewa wewe tia maji. Maana yangu hapa ni kwamba kama ni mahakamani ki tabia sio mtu wa kumuwekea dhamana, hata wewe jamaa yako ukimuweka kwenye kumi na nane anaweza kufanya mambo.

Ni vyema umshauri tu aache hiyo tabia mbaya na aangalie jinsi anavyo weza kulikwepa hilo soo kwa sasa kwa sababu ameshalikoroga na inabidi alinywe. Ili maisha yaendelee itabidi aishi kama mkimbizi.
 
Ntungila nunshiwakwe, anenkuzolya mumpishi zyose..inkuku nu twana twakwe!...Amassongelo gipasa mushitundu...! Huyu jamaa akilizake si nzuri eeh!..Hata mimi ningekuwa ndo mwenye mali hizo namshikisha ukuta..huh!
Nimeipenda hii mkuu lugha ya wapi?
Huyo jamaa inabidi ashikishwe adabu!
 
hana haja ya kujifanya anaogopa yeye ni mtu mzima wakati anafanya hayo alikuwa anajua kuwa ni hatari na akaamua kufanya, he has to face the consequenses. there is no way we can let you die a natural death NO.
 
hehehehehehe
Anaomba msaada?? wakati anawatokea kuku na mayai aliomba msaada? Gadem
akitaka nimsaidie anitumie namba ya huyo binti wa miaka 19 nitampa ushauri kuntu tena hatodhurika kamwe.
 
heeeeee? huyu kweli mbofya! yaani kuku na mayai yake tena kuku wa mtu eeeh? we umejitafutia balaa,haya sasa kimbilia hata sudan,ukilipuliwa hakuna hasara
 
Mhhh nadhani ana mtihani mkubwa sana na sijui ataukwepa vipi kwa kweli...Sasa jamaa yeye alikuwa na tamaa ya aina gani??yeye anatembea na mama mtu anaamua kuchukua na mtoto wake alikuwa anataka majibu ya aina gani??Hakuona kama mwenyezi mungu alikuwa anamuangaza kwa wakati huo na alivyoona vishawashi vinakuja hakujua kama ni mtihani na inabidi abadilishe tabia??Sidhani kama kuna ushauri zaidi kama anaweza kama yupo hapo bongo basi ajaribu kuongea na huyo mother na ikiwezekana hata mtoto kila mtu kwa wakati wake then atoke hapo nchi kwa atleast hata mwaka mzima hivi...Then tuone itakuwaje zaidi ya hapo sijuji jamaa atamfanya nini kwa kweli!!
 
Back
Top Bottom