Anakatazwa kutoka ndani!!

Huu ndio ushauri tuliompa mwanzo kuwa amtafutie shughuli ya kufanya, lakini kama walivyosema wazazi wa binti siku ya harusi yule mwanamke hataki kufanya kazi ni mvivu sana.

:juggle: kumbe jamaa tangu hajaoa anajua mwanamke ni kiburi na mvivu sasa anatala ushauri gani wakati wazazi walishampa go ahead??alaa watu wengine bwana..kweli inawezekana ana psychological problem kama mdau hapo chini alivyosema..aaii uzoba mwingine unatia hasira
 
samahani lakini,huyo mke wa jamaa ni kabila gani????????? n.b sianzishi ukabila bt nataka kujumuisha in my personal tribal research.............:juggle:
 
Kama ameamua kuwa jeuri kiasi hicho
Mwambie huyo rafiki yako achukue likizo
asafiri kwa wiki au mbili
Asiache matumzi wala nini..
labda hapo ataitambua thamani ya mumeo..

Hilo la kusafiri na kupeana likizo la muda linaweza kuwa sehemu ya ufumbuzi, lakini kutowacha matumizi..... tukumbuke kuwa wana mtoto. Si haki kwa huyu mtoto kuteseka kwa sababu ya migogoro ya wazazi wake.

:focus:Tatizo huyu jamaa laini sana, hawezi hata kukaa na kuzungumza na mkewake? Kama tu tungelikuwa na utamaduni wa kuongea matatizo yetu, "pros and contra", tungefika wakati tunachukua misimamo ya kati na kufikia maelewanao. Inavyoonesha huyu jamaa hawezi kufanya lolote, kwa hiyo hata kama ataenda kwa wazazi, washenga, atapata ushauri wa marafiki na wataalamu... ikiwa hatajinasua na mtindio wake wa maamuzi, hakuna litakalobadilika. Ni juu yake kushika hatamu.
 
Huyo mwanamke ana inferiority kama anaweza amtafutie hata cha kusoma awe busy, na kama ni mjeuri wa asili basi mume amtolee uvivu amuonyeshe yeye sio zoba. Na kwa kuwa bazazi banajua tabia ya binti yao basi awaeleze. Pole yake sana.
Kweli kabisa nadhani ni inferiority complex.................hivi elimu haiwezi kuwa imechangia maana mama mwenyewe ni darasa la saba.
 
Ahahahahaaaaahhh!! Hii tulishamwambia mpaka tumechoka.

Kama ni hivyo mshauri siku moja aombe ruhusa halafu mpandishe kwenye gari yako bila kumwambia unampeleka wapi nenda nae mkoa wa jirani mnyang'anye simu zima mkalishe hapo kwa huo muda alioomba ruhusa asiwasiliane na mkewe halafu hakikisha haachi pesa ya chakula kama wengine walivyosema lazima atashika adabu tu
 
Ushauri amrudishe huyo mama nyumbani kwao kwa muda wa mwaka mmoja au hata miezi sita asimpe matumizi mahitaji ya mtoto awe ananunua mwenyewe, na kwa sababu huyo mama hafanyi kazi baada ya huo muda atakua amekula jeuri yake na kujifunza. Na kama baada ya huo muda hajajifunza basi hafai ampe talaka sio ubavu wake huo atapata ugonjwa wa moyo. Ila ampe muda wa kujirekebisha kwanza asimuache moja kwa moja ghafla.
 
Mwanamke mvivu, jeuri, hapatani na majirani, mgomvi, ukiwa mvivu lazima uwe mchafu sasa huyo mwanamke wa kazi gani
ushauri wa mwisho apewe talaka akajifunzi upya
Kwa jinsi hali ilivyofikia hivi sasa talaka ndio suluhisho..
 
Ushauri amrudishe huyo mama nyumbani kwao kwa muda wa mwaka mmoja au hata miezi sita asimpe matumizi mahitaji ya mtoto awe ananunua mwenyewe, na kwa sababu huyo mama hafanyi kazi baada ya huo muda atakua amekula jeuri yake na kujifunza. Na kama baada ya huo muda hajajifunza basi hafai ampe talaka sio ubavu wake huo atapata ugonjwa wa moyo. Ila ampe muda wa kujirekebisha kwanza asimuache moja kwa moja ghafla.
Kuna siku alimripoti kwa wazazi wake(wakwe zake) wakamwambia kama amemshindwa amrudishe kwanza kwa muda, jamaa akasita eti kwa kuwa mke wake ni mjamzito!! Kwa kweli nilimshangaa sana.
 
Kama ni hivyo mshauri siku moja aombe ruhusa halafu mpandishe kwenye gari yako bila kumwambia unampeleka wapi nenda nae mkoa wa jirani mnyang'anye simu zima mkalishe hapo kwa huo muda alioomba ruhusa asiwasiliane na mkewe halafu hakikisha haachi pesa ya chakula kama wengine walivyosema lazima atashika adabu tu
Ahahahahaaaah!! Dena mimi nina miliki baiskeli........lol...
 
Kitchen party tunaziponda ila zinasaidia kwa kiasi fulani, huyo dada analotafuta atalipata muda si mrefu. mtoto wa watu kumkataza kutoka out na wenzie utafikiri umemzaa wewe! hata mtu hawezi pata dili za maana maana nyingine zinapatikana wanapokaa wenyewe huko wanaume. Tatizo lake kubwa ni kutokujiamini kila akitoka anakuwa na wasiwasi wakati jamaa anaweza enda lunch time fasta na akarudi home saa kumi na mbili mkavuuuuuuu.
 
Ulimbukeni wa mapenzihuo " wapo waliopendana kama kumbikumbi eeee.........wanapotembea ....bibi mbele...bwana nguma.......":lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol:
 
Kwa jinsi hali ilivyofikia hivi sasa talaka ndio suluhisho..

Talalaka sio suluhisho kwa sasa akampumzishe kwanza aone atajirekebisha au kwani anaweza akajirekebisha na kuwa mwanamke mzuri sana baadae baada ya kujifunza kutokana na makosa, ila asipojirekebisha hapo sawa talaka itoke ila huyo mkaka awe mvumilivu kipindi huyo mdada yuko kwao asijetegwa na mwanamke mwingine akamuoa alafu akakuta afadhali ya yule alieondoka yanatokea sana haya mambo.
 
Ushauri amrudishe huyo mama nyumbani kwao kwa muda wa mwaka mmoja au hata miezi sita asimpe matumizi mahitaji ya mtoto awe ananunua mwenyewe, na kwa sababu huyo mama hafanyi kazi baada ya huo muda atakua amekula jeuri yake na kujifunza. Na kama baada ya huo muda hajajifunza basi hafai ampe talaka sio ubavu wake huo atapata ugonjwa wa moyo. Ila ampe muda wa kujirekebisha kwanza asimuache moja kwa moja ghafla.

Hivi unaanzaje kumkatalia mume kutoka jamani huyu dada ni mwehu, kweli maty amrudishe tu home akanywe chai
 
Hivi unaanzaje kumkatalia mume kutoka jamani huyu dada ni mwehu, kweli maty amrudishe tu home akanywe chai

Hiyo chai ataisikilizia kwenye kipindi cha mapishi.

Ni kavu kavu tu mpka saa tisa na tena mpaka kesho.

Mie nadhani ni zaidi ya mwehu kabisa kha?!!
 
Heshima wakuu...
Kuna jamaa yangu ambaye tumekuwa pamoja nikiwa na maana michezo ya utotoni na shule ya msingi pia tumesoma darasa moja kule kijijini kwetu. Amekuwa kama ndugu maana ndiye alinipokea hapa mjini kabla sijaanza kujitegemea. Matatizo yalianza alipooa, baada ya miezi kama sita hivi nilipigwa marufuku na mkewe nisiwe na mazoea na huyu jamaa eti namtafutia wanawake, pindi tunapotoka pamoja hasa siku za wikendi. Kuepusha mgogoro nikaacha kwenda nyumbani kwa jamaa na kama kuna shida ya muhimu namuibukia ofisini kwake. Si mimi tu, bali marafiki wote wa karibu wa jamaa walipigwa mkwara kama mimi.
Ishu ni juzi huyu jamaa kaja kuniomba ushauri amfanye nini mkewe maana kero zimezidi, akichelewa kurudi kazini ni zogo, na akirudi haruhusiwi kutoka labda atoe sababu za msingi kwa nini anatoka na ikiwezekana wanatoka wote. Kifupi jamaa hana sauti mbele ya mkewe.
Nilimshauri jamaa hii ishu aifikishe kwa wazee akianza na mshenga, kabla ya kuchukua uamuzi. Mke wa jamaa ni mama wa nyumbani.
Nimeileta hapa ili tupate uzoefu kutoka kwa wataalamu wa mahusiano na mapenzi huenda tukapata uzoefu kwa waliowahi kupata mkasa kama huu.
Nawasilisha...

Wanawake wa design hii unamtongoza yeye sasa

Lengo kula na nduguyo tu. Utakuwa unamtoa out yeye badala ya mmewe.
 
Kweli kabisa nadhani ni inferiority complex.................hivi elimu haiwezi kuwa imechangia maana mama mwenyewe ni darasa la saba.

Wapo wengu darasa la saba na ndoa zao utazifurahia
hiyo ni tabia yake ya kuzalia na itamchikua karne huyo jamaa kumrekebisha
kama huyo mama hatakuwa tayari kujirekebisha mwenywewe
 
Kwa jinsi hali ilivyofikia hivi sasa talaka ndio suluhisho..

Kuna vitu vingi tu vya kumnyoosha huyo bibie, sio talaka . kwanza abadilike awe mkali na sheria kibao. akipiga kelele anampa ban la unyumba kama mwezi hivi ashike akili kwanza
 
Back
Top Bottom