Anajuuta kuchukua mume wa mtu

Vasco Dagama

Member
Jan 18, 2012
52
10
Habari zenu.

Nina rafiki yangu (mfanyakazi mwenzangu) yamemfika yakumfika.

Amenisimulia visa vingi na mambo mengi ambayo nimemwonea huruma.

Ni msichana wa umri wa miaka 25, alikuwa na boyfriend wake chuo akazaa nae na akamkimbia
akalea mtoto peke yake......ni story ndefu ngoja niifupishe...............
akakutana na mwanaume wa mtu japokuwa yule mwanaume anasema alikwenda kwake ili kuondoa stress
kuwa mkewe (hawajafunga ndoa) anavyosema ana matatizo chungu mbovu..........................
msichana ana stress za kulea mtoto na kuachwa na mwanaume na akapewa mapenzi moto moto
mpaka akafikia kumtukana yule mwanamke mwenzie bila kujali na akaona kaolewa kabisa maana mwanaume alikuwa
anasema kasafiri kumbe yuko kwake.

Kisa chenyewe ni juzi wakiwa wote kwenye matembezi jamaa kaanguka ghafla na kupelekwa hospitali madaktari
wakampima kila kitu wakagundua ni HIV+ na msichana yuko hapo...............amekuja kwangu analia anaomba ushauri
afanya nini sasa kwa wakati huu??!! Nimekosa cha kumwambia

Najua hapa ni kisima cha ushauri naombeni mnisaidie ushauri........kupima kasema atakwenda kupima lakini anasema anaona anakwenda kuconfirm tu maana anajua aliyofanya na huyo jamaa ni mengi sana.

Asante
 
Mwache alie tena sana kabisa - maana amekosea nafsi yake. Mpe pole na hongera kwa ulezi wa peke yake lakini hayo ndio majukumu

Pili, mwambie ukweli kwamba kutembea na mume wa mtu kunamadhara yake hasa kutumia tu statistics za afya, ndoa zinamaambukizi makubwa. Lakini zito zaidi, sio sawa kutoka na kumtukana mke wa mtu - hata kama angekuwa mpenzi wake tu. Hivyo, anapaswa kumuomba radhi na kuomba radhi nafsi yake.

Tatu, swala la kupima ni la msingi - kwani maambukizi anaweza asiwe nayo kabisa. Na hata pale atakapokuwa nayo inawezekana kabisa CD4 zake zikawa ziko juu na hivyo kuhishi vizuri kwa afya kwa muda wa kutosha kabla hajaanza RV's. Na pia atambua, maisha ya watu wanaoishi na virusi yanaongezeka kutokana na kupatikana kwa dawa mbalimbali. Asihofu, ila tabia abadilishe sasa.

Kila la kheri.
 
Pole sisi tunaijua JF,watu wanakuja kwa gear ya care-off,oh rafiki yangu,oh dada yangu,,pole sana nakushauri mtafute kibonde au masoud kipanya watakusaidia sana kwa mawazo
 
Mwache alie tena sana kabisa - maana amekosea nafsi yake. Mpe pole kwa ule wa peke yake lakini hayo ndio majukumu

Pili, mwambie ukweli kutembea na mume wa mtu kunamadhara yake hasa kutumia tu statistics za afya, ndoa zinamaambukizi makubwa. Lakini zito zaidi, sio sawa kutoka na kumtukana mke wa mtu - hata kama angekuwa mpenzi wake tu. Hivyo, anapaswa kumuomba radhi na kuomba radhi nafsi yake.

Tatu, swala la kupima ni la msingi - kwani maambukizi yanaweza uwa sio lazima awe nayo. Na hata pale atakapokuwa nayo inawezekana kabisa CD4 zake zikawa ziko juu na hivyo kuhishi vizuri kwa afya kwa mda wa kutosha kabla hajaanza RV's. Na pia atambua, maisha ya watu wanaoishi na virusi yanaongezeka kutokana na kupatikana kwa dawa mbalimbali. Asihofu, ila tabia abadilishe sasa.

Kila la kheri.

Asante sana kwa ushauri
 
hv unatembeaje na mtu hujui hiv status yake tena kwa ngono zembe enzi hz?
mimi ukinitaka angaza kwanza
ndo maana sina mpenzi maana tukipanga kwenda angaza huwa siwaoni tena

Labda dawa ya penzi ilipasuka ghafla

Halafu ishatokea sasa itabidi tumpe ushauri ajue the way forward
 
huwaga nawachukia sana tena sana wazinifu hvy ushauri wangu utamuweka pabaya bora nisimshauri
 
huwaga nawachukia sana tena sana wazinifu hvy ushauri wangu ni anywe sumu kufidia makosa yake
kuna mdadA MMOJA ANGEL ALIKUWA ANATEMBEA NA MUME WA MTU SASA NAYEYE HVOHVO AKAANZA KUMTUKANA MKEWE.KUMBE WALISHAPIMA HUYO MZEE ANA NGOMA NA MKEWE HANA SO HUYO MAMA AKAMPA RUKSA YA KUJIACHIA
SASA YULE MDADA KUNOGEWA MAANA YULE MZEE KUTOKANA NA RUHUSA YA MKEWE ALIKUWA ANALALA KWA HUYO MDADA SOMETIMES AAKAANZA NYODO
ONEDAY YULE MAMA AKAMTUMIA CHETI CHA HOSPTAL CHA HUYO MDINGI
BALAAA
USIPIME
 
Mwambie akubali matokeo ya yote aliyotenda iwe kwa kujua au kwa kutokujua. Ni muda mzuri kwake kuanza kujipanga upya.

Jambo la kwanza kabisa, aende kupima na sio ku -confirm kama anavyodai. Vipimo vya damu yake ndiyo vitamhakikishia hali yake ikoje na sio kwa kufikiri. Wataalamu watampa ushauri sawa sawa na majibu yake. Baada ya hapo atajipanga aishije. KUMBUMBUKA HUU SI MUDA WAKE WA KUJUTA, NI MUDA WA KUJIPANGA.
 
unafikiri huyo jamaa angekuwa hajaoa na yakamkuta yaliyomkuta akiwa na huyo dada,mdada angekuwa na unafuu wowote au uzito wa virusi ungepungua?am just thinking loudly...
 
Hakuna ushauri zaidi ya kwenda angaza na kijiangazia
Then fuata masharti
 
kuna mdadA MMOJA ANGEL ALIKUWA ANATEMBEA NA MUME WA MTU SASA NAYEYE HVOHVO AKAANZA KUMTUKANA MKEWE.KUMBE WALISHAPIMA HUYO MZEE ANA NGOMA NA MKEWE HANA SO HUYO MAMA AKAMPA RUKSA YA KUJIACHIA SASA YULE MDADA KUNOGEWA MAANA YULE MZEE KUTOKANA NA RUHUSA YA MKEWE ALIKUWA ANALALA KWA HUYO MDADA SOMETIMES AAKAANZA NYODO ONEDAY YULE MAMA AKAMTUMIA CHETI CHA HOSPTAL CHA HUYO MDINGI BALAAA USIPIME
yote hiyo ni kutokana na tamaa za kijinga wacha avune alichopanda
 
Mpe pole sana,mwambie asione ndio mwisho wa maisha yake na wala asichukua uwamuzi wa kuanza kuvisambaza kisa yeye kapewa .
 
Hata angekua sio mune wa mtu bado angeambukizwa virusi vile vile.

Aende akapime sasa apate uhakika ili kama anao aanze kuishi kwa kuzingatia masharti.
 
Naimagine alivyo na wakati mgumu,alikosea sana lakini ajipe moyo na kujipanga upya ikiwa ni pamoja na kupima. Mpe pole na mtie moyo maisha lazma yasonge mbele :A S 465:
 
no way hapo! Akapime na apate ushauri nasaha! Mpe pole sana mkuu!
 
hv unatembeaje na mtu hujui hiv status yake tena kwa ngono zembe enzi hz?
mimi ukinitaka angaza kwanza
ndo maana sina mpenzi maana tukipanga kwenda angaza huwa siwaoni tena

Mtu anaweza kuwa na maambukizo ndani ya kipindi cha miezi mitatu mara nyingi virusi havionekani. Dawa ni kuacha kabisa zinaa au ingalau kutumia kondom zinasaidia kwa asilimia mpaka 60% (research data), inabidi tuambiane ukweli ndugu zangu.

Mshauri akapime kabla ya yote atapewa ushauri nasaha na wale maprofesheno wa ushauri nasaha, na maisha yataendelea kama kawaida. Kama ameambukizwa au la ajue sio mwisho wa dunia, ila amuombe Mungu amsamehe na kuendelea kutenda sawasawa na mapenzi yake, ila kama ameambukizwa asisambaze kwa wengine bali awaambie ukweli.
 
hv unatembeaje na mtu hujui hiv status yake tena kwa ngono zembe enzi hz?
mimi ukinitaka angaza kwanza
ndo maana sina mpenzi maana tukipanga kwenda angaza huwa siwaoni tena

Kwa hiyo ukipata mtu akakubali kwenda angaza utakuwa tayari kuwa na mpenzi? Wewe ni jinsia gani? Kama ni ke mimi nipo tayari kwenda angaza. Tehe
 
sisi wakatoliki tunasema mshahara wa dhambi ni mauti, ajiandae tu kuweka mambo safi
 
Back
Top Bottom