Anadai mtoto ni wangu

Mbona amekutuka?
Ati usipoteze hela kwa malaya? Duh......................
 
Ndugu zangu wana jf naombeni ushauri wenu,may mwaka 2008 niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja mkazi wa iringa,ila ilipofika june tarehe za kuanzia 20 alisafiri kwenda kwao iringa ambako alienda kukaa wiki mbili, baada ya kurudi ndani ya hizo wiki mbili nilipata tetesi kuwa ni mjamzito ila nilipomuuliza alikataa katakata kuwa hakuwa na mimba,mwezi wa nane aliamua kurudi kwao iringa na nilimkatia tiketi ya kurudi kwao mimi mwenyewe kwani aliniambia anataka akaishi na familia yake,
mwaka 2009 mwezi wa tatu tarehe kumi na moja nikapata taarifa kuwa amejifungua mtoto wa kiume,lakini hakuniambia mimi aliwambia ndugu wengine,
mwaka huo mwezi wa 11 nilienda iringa kumuona mtoto lakini huyu binti aliniambia mtoto si wangu ni wa jamaa aliyekuwa amemuoa,akanipa na picha ya huyo jamaa aliyemuoa kuwa niangalie na nilinganishe na mtoto lakini nilipoona masikio nikahisi mtoto si wangu,
ajabu jumapili ya wiki hii yule dada akanipigia simu kuwa mtunze mwanao usipoteze hele yako kwa malaya huku mwanao anahangaika,
nikamwambia mbona ulisema mtoto si wangu akasema ukweli anaujua yeye ,
jamani nifanyeje?

yeye kuujua ukweli haimpi haki ya kubadili maelezo whenever she find it fits her purpose and ofcource to her advantage. atakuja kukuambia mtoto si wako pia
ila una moyo mzee, ulienda ad iringa kubembeleza mtoto awe wako? ukatoswa live, now maelezo yamebadilishwa na we ume shake mbayaa! hata hujitambui!
 
toka kuumbwa kwa dunia wanawake wamekuwa wakisema UKWELI WA MTOTO AUJUAE NI MAMA!na wanaume wamekuwa wakiamini hivyo. Lakini mimi nasema huo ni UONGO,tena ni uongo unaoelekea ukingoni..Ikiwa wanawake hawajui vema siku za hatari watawezaje kujua saa na wakati mimba ilipotunga?maana ktk siku ya hatari hiyohiyo unaweza kusex na wanaume wawili mchana na jioni na mimba itakayoingia ikawa ni ya jamaa wa jioni!hili jambo ni complex sana na wanawake wamekuwa siku zote wakioteaotea au kujichaguliachagulia baba za watoto wao

Sasa ili kumaliza utata huo sasa tuweke ktk KATIBA MPYA,katika cheti cha kuzaliwa mtoto anapewa jina la ukoo au la baba baada ya DNA kupimwa,kama huna uhakika mimba ya nani muite mtoto jina la ukoo wenu!full stop.

Wanawake naomba mpiganie hili liingie ktk katiba mpya!mpo tayariiiiiiiiiiiiiiiiiii?

wadada msiwe wakali tujadili taratibu point baada ya pointi
 
ushauri kwa mtoa mada,kwa kesi yako hata kwenda kupima DNA ni kupoteza muda na pesa zako bure!Kauli yake ya kwanza tembea nayo hiyohiyo!ktk mazingira hayo hata Mungu atakusamehe ukimkataa huyo mtoto!asikutishe na msemo wao maarufu ukweli wa mtoto aujuae mama!msemo huohuo watu wamebambikiwa watoto sio wao!uamini msemo huo nawe uongezwe ktk list ya waliobambikiwa watoto!
 
Hakuna Cha Masikio wala pua ..kama alikuwa na sababu za kusema sio mwanao na pia una sababu ya Kumverify uyo mtoto kwa DNA..usipuuze

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Uringa?! ......achelewi kujitundika ukimkataa mtoto.
 
Tunza, Mtoto ni wako. Usijaribu wala usithubutu kupima DNA, kwa kuwa kitendo hicho kinaleta mgogoro ndani ya Familia. Fikiri kwanza! kama Baba yako, akikupeleka kupima DNA, Utajisikiaje? na nini Tafasiri yake? Je! mama atajisikiaje iwapo baba anapeleka watoto kupima DNA. Tafasiri rahisi ni kuwa (baba haamini kama mama ni mwaminifu katika ndoa)
Sisi sote tulio katika ndoa, tunafanyiwa mengi, ila Ili tuishi kwa amani, tunatulia. Hakuna mwanaume ambaye hafanyiwi, ila huwa hajaona tu. Shukuru mungu, kama hujaona. "ZINGATIA USHAURI HUU, UTAISHI KWA AMANI"
 
Back
Top Bottom