Anadai mtoto ni wangu

Mzanzibar

Member
Sep 20, 2011
36
2
Ndugu zangu wana jf naombeni ushauri wenu,may mwaka 2008 niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja mkazi wa iringa,ila ilipofika june tarehe za kuanzia 20 alisafiri kwenda kwao iringa ambako alienda kukaa wiki mbili, baada ya kurudi ndani ya hizo wiki mbili nilipata tetesi kuwa ni mjamzito ila nilipomuuliza alikataa katakata kuwa hakuwa na mimba,mwezi wa nane aliamua kurudi kwao iringa na nilimkatia tiketi ya kurudi kwao mimi mwenyewe kwani aliniambia anataka akaishi na familia yake,
mwaka 2009 mwezi wa tatu tarehe kumi na moja nikapata taarifa kuwa amejifungua mtoto wa kiume,lakini hakuniambia mimi aliwambia ndugu wengine,
mwaka huo mwezi wa 11 nilienda iringa kumuona mtoto lakini huyu binti aliniambia mtoto si wangu ni wa jamaa aliyekuwa amemuoa,akanipa na picha ya huyo jamaa aliyemuoa kuwa niangalie na nilinganishe na mtoto lakini nilipoona masikio nikahisi mtoto si wangu,
ajabu jumapili ya wiki hii yule dada akanipigia simu kuwa mtunze mwanao usipoteze hele yako kwa malaya huku mwanao anahangaika,
nikamwambia mbona ulisema mtoto si wangu akasema ukweli anaujua yeye ,
jamani nifanyeje?
 
achana nae yeye mwenyewe sio mkweli vitisho tuu hivyo....ngoma ikibana atakuja mwenyewe kwako ndio hapo nawe wambana aseme ukweli wa mambo....be patient
 
Huyo hajielewi, kama mtoto ni wako hakua na sababu ya kukataa toka mwanzo, it seems baba halisi wa mtoto amemkataa ndo anaamua kukubambikizia wewe. Kama unaweza kafanye DNA upate uhakika zaidi!
 
mmmh, labda script aliyokuwa kaandika imepotea

sasa anakwenda 'heregeni' tu
 
Mwenzangu na wewe kiyasi yakukute,yani matangazo ya condom mpaka kwenye vibajaji na condom mpaka bure unapata ulijisahau vp yakhee? Au nyama kwa nyama ntaaamu? Sasa unauziwa mbuzi kwenye gunia mara mtoto sio wako mara wako, haya mlee kitanda hakizai haramu ....
 
Huyo dada ni muongo! Mwambie akupe sababu za kukataa mwanzo.
 
wewe ni second choice yake yule wa kwanza ambae ni baba halali wa mtoto kamtosa
anatafuta hifadhi kwako, angalia usije ukaingia mkenge
ila kama una uwezo wa kumsaidia kumtunza mtoto we mtunze baadae kacheki DNA kama akizidi kungangania mwana ni wako.
we uliangushaga tu bila kuvaa soksi au alifunga macho nawe ukaambiwa zambi zote kwako?
 
Asikuchezee akili, maji yamemfika shingoni anataka apumlie kwako
 
wewe ni second choice yake yule wa kwanza ambae ni baba halali wa mtoto kamtosa
anatafuta hifadhi kwako, angalia usije ukaingia mkenge
ila kama una uwezo wa kumsaidia kumtunza mtoto we mtunze baadae kacheki DNA kama akizidi kungangania mwana ni wako.
we uliangushaga tu bila kuvaa soksi au alifunga macho nawe ukaambiwa zambi zote kwako?

kweli yeye ni option ya PILI, ya kwanza ikirudi atakuacha. peleka mtoto mkapime DNA.
 
Back
Top Bottom