Anachotaka ni mimba tu!

umeona eeh mtu unaanza kuwaza kumbe walioko ktk ndoa siku akikutana na wakale wake akiomba msaada wa kimapenz atasaidiwa ingawa sio woote wanawaza ivo ila wanaharibia wale ambao hawawazi ivo
na pili anaonesha hampendi sana mkewe mana angekua anampenda sana wala isingefikia hatua ya kumpa huyo mama nafasi ktk moyo wake kumuwaza mchana kutwa mpaka kuja kuomba ushauri kwa rafiki yake hapo inaonesha yuko fifty fifty

Kweli kabisa
Tusema mambo mengine huwa tunatayataka wenyewe na yanafikia kututesa
Ni maamuzi kuamua kuw asawa tulikuwa marafiki na kila mmoja ana familia yake
heshimu hili la mwenzako analokuambia ana familia yake na hapendi hilo unalotaka kumwambia
Inaonekana hata jamaa mwenyewe hana msimamo na hajajua kama aende au aache na anapokumbuka what happens in those old good days anaona mhhh ngoja nisikilizie ushauri
Ila ushauri wa maana ni kwamba aheshimu ndoa yake
 
Wana JF nawapongeza kwa ushauri mzuri kwa huyu jamaa wa kumwkoa kwenye janga maanake angekuja juta. Na si yeye tu mliyemshauri kwani tupo wengi wenye haya matatizo na ni ushauri mzuri wa kuachana na hayo mambo na kulinda ndoa zetu
 
Bora lawama kuliko fedheha, anaweza kumpa hiyo mimba leo lakini huko mbeleni yakaja kutokea ya kutokea akajikuta ameiweka rehani ndoa yake, namshauri aendelee kumkwepa tu
 
Heshima mbele wanaMMU

Ninayoiweka hapa ni mada ya ukweli ambayo rafiki yangu aliniletea tuidisscus..sasa katika kuidiscuss kuna mawazo ambayo nilimpa na of course kuna mengine ambayo tulishindwa kuafikiana. Lakini kwa sababu kisima cha JF hakikaukiwi maji nimeona kabla hajafikia uamuzi rasmi basi niwashirikishe nanyinyi hapa ili nione kama mnaweza kuchangia kitu gani katika huu mpango mzima!

Iko hivi..Jamaa yangu huyu alishawahi kuwa na rafiki wa kike kama miaka kumi iliyopita maeneo ya huko Mwanza. Na kama mnavyojua raha ya maisha kuhangaika, baada ya muda mrefu kila mtu kuwa kwenye mihanjo yake mawasiliano yalikatika na kila mtu kupata uhusiano mpya. Jamaa yangu alioa na kwenye ndoa yake kajaaliwa kupata mtoto mmoja, halikadhalika bibie naye aliolewa na kubahatika kupata mtoto mmoja pia. Kwa kipindi cha miaka ya karibuni kama miaka mitatu iliyopita marafiki hawa wa zamani walijikuta wameonana na wakawa wamebadilishana mawasiliano na wakaanza kuwa wanajuliana hali na vitu kama hivyo. Kwa mujibu wa huyu jamaa yangu, ilionekana kama mwanamke alikuwa anapenda wakumbushiane na jamaa yangu kwa mujibu wa alivyoniambia alimwambia waheshimu ndoa zao na wabaki kuwa 'friends'. Kwa mujibu wa mshkaji, mwanamke aliliafiki kwa shingo upande tu.

Sasa, tatizo limekuja,Mume wa yule mama alifariki..na mshkaji wangu hajui kilichomuua japo inasemekana ni 'pressure' na ofcourse ni kama mwaka mmoja uliopita na jamaa kwa mila na desturi baada ya siku nyingi za kutokwenda Mwanza alienda kwao na akaamua kwenda kumpa pole huyu mama. Cha ajabu huyu mama aliipokea pole yake lakini pia akamwambia angependa azae naye kwa sbb anahisi anahitaji mtoto na hayuko tayari kuolewa tena coz umri umeenda. Mshkaji wangu anadai alimchomolea, lakini yule mama alimwambia..'wewe nipe mimba tu hayo ya ulezi niachie mimi'!.

Sasa ili kufupisha habari hapo ndio kesi ilipo..Jamaa alifanikiwa kuchomoa kwa mara ya kwanza lakini huyu mama kaja hapa Dar na kampata jamaa na madai yake yamesimama vilevile!!..Naomba ushauri hapa 'Je? ampe tu hiyo mimba au asepe mazima!!..

NB: Matusi na Kejeli sio kitu cha maana hapa, na kama huna la kuchangia please ukimbie huu uzi!!

Asijaribu kabisa inawezekana mwenzie ana nia ya kumwambukiza au kumwaribia ndoa ili wawe wote
 
sasa kuna haja ya kuomba
ushauri hapo kwa situation kama hiyo? Huyo jamaa yako ana tamaa na
anataka ndo maana anajiuliza uliza wkt jibu ni rahisi tu, NO. Amwambie
haiwezekani bse ye ni mume wa mtu tayari.

mimba maana yake ngono bila kinga. hatari zake sote tunazijua!
 
..Jamaa
alifanikiwa kuchomoa kwa
mara ya kwanza lakini huyu
mama kaja hapa Dar na
kampata jamaa na madai yake yamesimama
vilevile!!..Naomba ushauri
hapa 'Je? ampe tu hiyo mimba
au asepe mazima!

Jambo kama hulitaki unalipa nafasi ya nini kwenye akili yako? Yeye kama mwanaume hakupashwa kutafuta ushauri, maamuzi yake binafsi yanatosha!! Mambo mengine yanakua kama "sitaki nataka", huku nikutokujitambua!!
 
Akili zako changanya na za jirani yako kisha chukua hatua......
 
Back
Top Bottom