Ana Tibaijuka vipi?

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,515
20,005
alianza kwa mkwara na wadau tulitabiri kuwa atazima tu,...kiko wapi??viwanja vya wazi kibao vimeporwa anajua na atafanya kitu,..hiyo ndio ccm,...nitavunja plaza....kigamboni hakuongea chochote cha maana na kuna kila dalili ya wananchi kupigwa mchanga wa macho...
 
mkuu kazi nzito hii na ndani ya ccm hawaiwezi HAKUNA WAKUWEZA KUMBUKA MAGUFULI MKUU!
 
Mama Anna Kajumulo Tibaijuka watu waliisha mtabilia kuwa kuvunja pale palm beach ilikuwa nguvu ya soda!! Jangwani Beach wenye fedha wamejenga na kuzifunga barabara na hakuna lolote alilofanya!!
 
Anna tibaijuka na upepe wake imefikia wapi jamani ? Au amenyamazishwa na chama cha mafisadi mafias ?m
 
Jamani, huyu mama alianza kwa spidi kubwa, ghafla kimyaaaa! Imekuwaje? Au ndo amechakachuliwa tayari? Mwenye taarifa zaidi atujuze kulikoni?
 
Duh Mama aligusa maslahi ya wenye nchi.hakupata ushirikiano toka kwa wanene wenzake akajikuta mwenyewe.
Kwa sasa hata maisha yake anakuwa na hofu.nchi hii..... Nadhani mama angeelekeza nguvu kurasimisha maeneo yanayomilikiwa hata kama yalikuwa ya wazi alafu ajipanghe vizuri kwa yale ambayo bado yapo wazi.
 
Jamani, huyu mama alianza kwa spidi kubwa, ghafla kimyaaaa! Imekuwaje? Au ndo amechakachuliwa tayari? Mwenye taarifa zaidi atujuze kulikoni?

alipo zungumzia uvamizi wa maeneo ya wazi hapa nchini naona hakujua ukweli kuwa chama chake ndicho kinaongoza kwa uvamizi wa maeneo ya wazi, kaujua ukweli ndio maana sasa kapoa. amuulize magufuli alipokua waziri wa ardhi naye alikuja juu akaondoka chini
 
kama profesa angejiuliza kwanza daud balali yuko wapi na kwa nini yuko huko alipo? jibu lake lingemwonesha namna ya kulitumikia taifa katika mfumo lililomo
 
Nimemwona kule kwenye blogu ya michuzi akikumbatiana na Mh Wassira ambaye ni mkali kwa wajane. Shauri yake!
 
Jamani, huyu mama alianza kwa spidi kubwa, ghafla kimyaaaa! Imekuwaje? Au ndo amechakachuliwa tayari? Mwenye taarifa zaidi atujuze kulikoni?

Labda Kikwete kishamuwekea stop kama alivyowekewa Magufuli. "Speed yako kubwa sana mama, punguza!"

 
Duh! bahati mbaya sana kama ameshatulizwa, nilishafurahi kama angesafisha na fukwe za Dar, kwani wawekezaji wanakuja na kurudi, watu wamevamia maeneo na kuuza kuku badala ya kupisha uwekezaji wa kitaliii wenye ajira kwa watanzania.
 
wewe Unamzungumzia huyu hapa au? Bibi yangu walimpatia wizara ngumu, ile wizara inahitaji jemedari a.k.a Shababu.
IMG_0637.jpg
 
hii kazi wapewe watu binafsi kuifuatilia tu, watumishi wa ardhi hawawezi
 
Back
Top Bottom