Amtwanga talaka mkewe

Huyu Mwenegoha ni laana tu inamtafuna. Najua anakoelekea ni kubaya zaidi.
Ushauri wa Bure amrudie Mungu wake!
 
Nyie KKKT mbona mnatukwaza siye waamini? Mara mkuu anunuliwe VX V8 na fisadi, mara mkewe apewe MarkX na mtoto wa fisadi, ni nini jamani? Ebu tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na hayo yote mtarudishiwa.

Sasa KKKT inahusikana na nini hapa??? "Mnakwazwa" na KKKT au hao walionunuliwa VX V8? KKKT na mtu mmoja mmoja ni issue mbili tofauti - hata kama huyo mtu mmoja ni mkuu wa KKKT.
 
'marriage crisis' hakika wanajua kinachowagombanisha na nina hakika kati yao hakuna mwenye gatsi za kuweka sababu bayana!
kuna jambo halijaenda sawa 'kwa chumba'
mix with yours
 
Huyu Mwenegoha ni laana tu inamtafuna. Najua anakoelekea ni kubaya zaidi.
Ushauri wa Bure amrudie Mungu wake!

Ni kweli mkuu. Yampasa akae atafakari vizuri huo uamuzi wake. MUNGU hadhihakiwi. Maisha yake hayako mikononi mwake kujiamulia laana na baraka bali MUNGU ndo mwenye mamlaka hayo. Anapaswa alijue hilo ili atubu na kumrudia MUNGU.
 
Nyie KKKT mbona mnatukwaza siye waamini? Mara mkuu anunuliwe VX V8 na fisadi, mara mkewe apewe MarkX na mtoto wa fisadi, ni nini jamani? Ebu tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na hayo yote mtarudishiwa.
matendo, jamani matendo, matendo kama kweli ninamcha Mungu mtanitambua tu.
 
.
Sio siri huyu Mwinigoha kama hali bangi kisiri basi ana pepo mkubwa sana wa ngono. Ona sababu anayoitoa ya kumtaliki mkewe haina nguvu ya aina yoyote kidila zaidi ya kuitukana imani ya kikristo. KKT mna kazi ya ziada.
mkuu

unaweza ukawa sihihi kwa upande wako, lakini naomba nikwambie kwamba tatizo la mwenegoha siyo ngono, tatizo lake kubwa ni kwamba haambiliki... ni mtu anayeamini kwamba yeye tu yuko sahihi

hata ajira yake pale KKKT iliota mbawa kwa sababu hiyo, yeye si mdini, yeye si mlevi na yeye si kwamba ana laana ya ngono... ila yeye ana kiburi cha kupitiliza na ni type ya either you are with me or you are my enemy
 
mkuu

unaweza ukawa sihihi kwa upande wako, lakini naomba nikwambie kwamba tatizo la mwenegoha siyo ngono, tatizo lake kubwa ni kwamba haambiliki... ni mtu anayeamini kwamba yeye tu yuko sahihi

hata ajira yake pale KKKT iliota mbawa kwa sababu hiyo, yeye si mdini, yeye si mlevi na yeye si kwamba ana laana ya ngono... ila yeye ana kiburi cha kupitiliza na ni type ya either you are with me or you are my enemy

IT LOOKS LIKE UNAMFAHAMU VIZURI SANA HUYU BWANA , NA UNAJUA VIZURI HABARI ZA NDOA YAKE, KWA NINI USIWE WAZI KUIONGEA HUMU ILI NA SISI TUJUE UKWELI KULIKO KUHISI Tu?
 
Kila nyumba ina matatizo na yanazidiana.. Hakuwa na uvumilivu.. NDOA ni KUVUMILIANA.
 
Ndoa ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa takribani miaka 20, Amani Mwenegoha (55), imeingia kwenye skendo nzito baada ya mtumishi huyo wa dini kudaiwa ‘kumtwanga' talaka mkewe kwa kiapo cha mahakamani.

Uwazi lilipata skendo hiyo iliyokuwa nyuma ya pazia kupitia vyanzo vyake makini na kuamua kuichimba kisha kubaini undani wake.

Baada ya Uwazi kuthibitishiwa uwepo wa habari hiyo inayoshtua kwa kiongozi wa dini kuasi maandiko matakatifu, waandishi wake mahiri waliingia mtaani na mtu wa kwanza kumnasa alikuwa ni mke wa mtumishi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mwanuni Mwangile (49) (pichani), ambaye alifunua mengi ya usichokijua juu ya ndoa hiyo.

Katika mahojiano maalum na gazeti hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwangile aliweka kweupe kwa kudai kwamba, mumewe huyo alimtelekeza miaka sita iliyopita huku wakiwa wamejaliwa watoto watatu ndani ya ndoa yao takatifu iliyofungwa mwaka 1988 katika Kanisa Kuu la KKKT, Azania Front, Dar.

Mwangile aliyeonekana kutojua hatma ya maisha yake hasa pale anapoona kuwa yuko kama mtu ambaye hajawahi kuolewa, alisema kuwa katika kipindi hicho chote haamini kama ameachika na kwake ilikuwa ndoto ya alinacha.

Mama huyo aliyeonekana kulilia penzi la mumewe aliendelea kusema kwamba, amekuwa akiishi maisha ya kubahatisha hasa linapokuja suala la kazi ambapo ameweka makazi yake wilayani Kisarawe, mkoani Pwani akiwa mfanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Aidha, mke huyo wa zamani wa Mwenegoha ambaye kitaaluma ni mwalimu wa muda mrefu, alisema kuwa tangu waoane na Mwenegoha mwaka 1988, wana miaka 22 kabla ya kukutwa na fedheha ya talaka hivi karibuni.

Huku akiwa na majonzi makubwa alisema: "Nilisikitishwa sana na tabia ya mume wangu alipoanza ishara za kutokunitaka kabisa na hata kufikia hatua ya kutofika nyumbani tulipokuwa tukiishi, Mtaa wa Wazuki, Masaki, Dar.

"Nilihisi mume wangu ana kimada aliyekuwa akimzuzua kwani hakuwa hivyo."
Akisimulia kwa undani wakati wakiwa Arusha kikazi Mwenegoha akiwa Kiongozi wa KKKT, Mwangile alisema kuwa walikuwa na maisha mazuri kiasi kwamba: "Familia kadhaa zilikuwa zikitamani maisha yetu," alisema mama huyo.

Alisema kwamba, baada ya mambo kuharibika katika Kanisa la KKKT, Arusha, Mwenegoha alirejea Dar kwa lengo la kuandaa makazi mapya lakini chakushangaza mawasiliano kati yao yalikatika ghafla.

"Kuona hali hiyo, nikaamua kufungasha virago na watoto kuja Dar kwa mume wangu aliyekuwa akiishi Masaki lakini sikupokelewa." Alidai Mwangile na kumalizia kwamba:
"Niliamua kwenda kwa ndugu zangu Kisarawe na katika kipindi hicho ndipo tulipovurugana na mume wangu akaniacha."

Kwa upande wake, Mwenegoha alikiri ‘kumtwanga' talaka mkewe huku sababu kubwa akiitaja kuwa mama watoto wake alikuwa akimnyima usingizi usiku.

"Alikuwa akiamka usiku wa manane na kuanza kusali bila sababu wala kuwepo kwa tatizo lolote. Mimi kama dini naijua sana na kila kitu kina wakati wake, kuna wakati wa kula na hata wakati wa ibada," alisema Mwenegoha na kuongeza:

"Mimi nilimshindwa mwanamke yule na tatizo hili lilikuwa ni la muda mrefu sana, nilichelewa tu kuchukuwa hatua madhubuti lakini baadaye niliamua kumpiga chini."
Mwenegoha alisema kuwa alichukua hatua ya kwenda mahakamani kwa ajili ya kiapo cha mahakama cha kutengana na mkewe ili kila mtu afanyanye shughuli na maisha yake.

Kuhusu watoto, Katibu huyo wa zamani wa KKKT alisema kwamba, anaendelea kuwalea kwa kuwa ni wanawe wa ndoa.
"Nimetengana na mke wangu na si watoto, huduma wanapata kama kawaida ikiwa ni pamoja na haki yao ya elimu," alimalizia Mwenegoha.

SOURCE:-GLOBAL PUBLISHERS

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, upendo hauoni uchungu, upendo hauesabu mabaya, upendo haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hutumaini yote, hustahimili yote, upendo haupungui neno wakati wote
 
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, upendo hauoni uchungu, upendo hauesabu mabaya, upendo haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hutumaini yote, hustahimili yote, upendo haupungui neno wakati wote

.... Na zaidi ya yote Upendo ni zaidi ya tendo la ndoa!!!
 
Back
Top Bottom