Amri kumi za mwanajeshi wa Tanzania

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,017
1. ITUKUZE TANZANIA NCHI YAKO KAMA MAMA YAKO MZAZI.

2. USIPENDE KITU CHOCHOTE CHA DUNIA KUZIDI NCHI YAKO TANZANIA.

3. USITUMIE JINA LA NCHI YAKO TANZANIA KWA FAHARI, SIFA, AU FAIDA YAKO MWENYEWE.

4. UTAIPA NCHI YAKO TANZANIA BILA KUSITA MALI YAKO, FURAHA YAKO, NA MAISHA YAKO.

5. SHINDANA DAIMA NA MAADUI WA NCHI YAKO TANZANIA MPAKA PUMZI YAKO YA MWISHO NA TONE LA MWISHO LA DAMU YAKO LAKINI MHESHIMU NA MPOKEE MTU YEYOTE AMBAYE NI MSAIDIZI WA NCHI YAKO TANZANIA.

6. SHINDANA NA UZEMBE WAKO NA WOGA WAKO. ANGALIA MWOGA HAWEZI KUWA MTANZANIA.

7. WAPENDE MAADUI WAKO LAKINI USIWAACHE WAIANGAMIZE NCHI YAKO TANZANIA.​

8. SIKU ZOTE NA MAHALI POPOTE KUBALI BILA HOFU KWAMBA UNAONA FAHARI KUWA MWAFRIKA WA TANZANIA.

9. KUMBUKA DAIMA KWAMBA KANUNI YAKO KUBWA KUPITA ZOTE NI KUJITAWALA. UHURU NA NEEMA YA WATANZANIA NA TANZANIA KUWA NI NCHI YA MWAFRIKA.

10. USIKUBALI MTU AITUKANE TANZANIA NA WATANZANIA AU KUIKASHIFU SIFA NA UKUBWA WAO AU HAKI ZAO ZA UHURU NA KUJITAWALA. IPENDE TANZANIA KULIKO KITU CHOCHOTE ISIPOKUWA MUNGU PEKE YAKE. IPENDE TANZANIA KULIKO NAFSI YAKO.


SOURCE: "VITA VYA KAGERA--KAGERA HADI ARUA" BY NGATUNI, KIGADYE,GHAHAE

cc Echolima, Kichuguu, Nguruvi3, Manyerere Jackton
 
Sijui sana. Naona kama yako kinyumezungu sometimes hapa kwetu! Ila huwa nakipenda kiapo cha jeshi la nchi flani chenye maneno...."I will.........defend.... from all enemies, foreign and domestic...."

Nadhani hapa kwetu tumetoa macho nje ya nchi zaidi, tukiamini kuwa maadui ni lazima watoke nje, huku tukiachia domestic enemies wananeemeka. It is bad that kuna wakati utafika...kuvuna tulichopanda, kupokea ujira wa kazi na kuangalia kwa uchungu matendo matukutu ya mtoto tuliyemlea.(umleavyo ndivyo akuavyo)
 
kisha serikali imesahau kujenga uzalendo huku ikijidai kusahau kwamba mtu anazaliwa mwananchi bali uzalendo hujengwa.
Wenyewe wanafikiri uzalendo unaendana na uwezo wa kuvaa skafu wanazovaa kina Mwigulu kwenye jua kali la Dar.
 
Wenyewe wanafikiri uzalendo unaendana na uwezo wa kuvaa skafu wanazovaa kina Mwigulu kwenye jua kali la Dar.

yaani bila ya mikakati thabiti na ya makusudi, hivi punde uzalendo tanzania utakuwa stori ya kale. nchi itabaki na wananchi tu.
 
Unajua hao kina Kigadye, Ghanai na Ngatuni walishia wapi?


..wako wapi hawa askari wetu, mashujaa wa vita vya Kagera?

..hizi amri nimezipata toka kwenye kitabu walichoandika kuhusu vita vya Kagera.

..kitabu hicho kina utangulizi ulioandikwa na Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine[r.i.p]

NB:

..Albert Kigadye ameandika kitabu kingine " Edward Moringe Sokoine -- Kiongozi wa watu aliyejitolea "

cc Echolima, Nyenyere, Kichuguu
 
Kwa upande wa jeshi naona hali siyo mbaya bado wana roho ya kizalendo na wanajua nini walifanyalo kwani walio wengi hawana muda na kauli mfu za akina Komba wala Lukuvi.

Hapa najiuliza ikiwa hawa makomredi na wazee wenzangu tulipitia jkt karibu wote na kiapo kikaliwa je, ni kipi kiliwafanya wawe mafisadi na wezi waliokubuhu kupitia hiki chama cha c.c.em ambacho mzee nyerere alikuwa tayari kukifia?

Hapa naona anguko la kaul na amri hizi kwa watawala na nashuhudia hawa wanao maform six wanakula kiapo upya ili wajekuijenga nchi na kuongoza vyema kupitia chadema.

Ni swala la kupeana muda tu ili utabili utimie.

Ni mimi.
 
Hata ile kauli ya kolimba aliyoitekeleza kwa kusema ukweli daima wakaamua kumzima kama kibatari.
C.c.em ni kimbilio la wahuni na na matapeli wa kisiasa na kiuchumi kwa rasilimali zetu.
 
Siku hizi kiapo chao ni kimoja tu, "Nitawatetea na kuwalinda usiku na mchana mafisadi wa ndani na nje ya nchi bila kujali wadhifa wao nchini kwa uwezo wangu wote."
 
Hata jeshi ambalo lilikuwa halijawa diluted kama huko kwingine taratibu sumu zinapenya na kutuharibia chombo pekee tulichokuwa tunajivunia.....tunahitaji watu wenye moyo safi kuamua kwa dhati kujitoa taifa lipone....
 
Tukitoa Shimbo aliyeharibu emage ya jeshi, bado niko na imani na maadili ya jwtz maana ndiyo taasisi iliyobaki na nidhamu Tanzania kwa kumhenzi Mwl Nyerere,Sokoine na Kawawa. Lakini siyo kwa wanafiki kama Kikwete na kwa unafiki wake aliamua kuikimbia monduli maana hapakuwa mahali pake kimaadili. Nadhani watanzania mwengi watakuwa wamelitambua hilo.
 
I like it.....mafisadi wameua uzalendo wetu kila mtu ana Chukua Chake Mapema....

Eti Uzalendo wa sikuhizi ni kukata mauno kwa sanaaa...hawana mapenzi ya kweli na Tanzania, wanafurahia first world facilities, wanafurahia nyimbo za kuhamasisha ushoga, wako tayari kuutangaza ushoga kwa kuwaleta bongo kwa gharama za walipa kodi wa nchi hii! Hakuna kiongozi hata mmoja ambaye ana mapenzi ya kweli kwa nchi yetu, pengine ndiyo maana MAFISADI wanakuwa wenyeviti wa kamati ya fedha wanatupangia bajeti ya kutukamua na kuwapendelea wazungu wenye kuchukua madini yetu bure bure... I wish hizo amri kumi zingeanzwa kuingizwa kweny mitaala yetu! Yafaa kuanza upya kama taifa maana kizazi hiki cha watawala hakina wasomi walioelimika na kujitambua bali kimejaa wachumia tumbo wabinafsi kupitiliza...
 
Back
Top Bottom