Amos Makalla nje, Zhakia Meghji ndani!

No Research no right to speak.Hakuwepo hazina wakati wa EPA,alikuwa maliasili fedha alikuwa mramba, Blunder alofanya ni kuingizwa choo cha kiume na Balali ku sign asokijua wakati wa Auditing, baadae alipostukia aka withdraw the statement.

Mkuu nadhani utakumbuka kuwa yeye ndio alisaini barua inayowapa ruhusa kagoda kuchota yale mabilioni kwa sababu yalikuwa yanelenga kufanya kazi za usalama wa nchi. Kwa hiyo sio wakati wa mramba tu alihusika pia kutoa some mane.
 
Mkuu nadhani utakumbuka kuwa yeye ndio alisaini barua inayowapa ruhusa kagoda kuchota yale mabilioni kwa sababu yalikuwa yanelenga kufanya kazi za usalama wa nchi. Kwa hiyo sio wakati wa mramba tu alihusika pia kutoa some mane.

Hiyo ni spin, Kagoda ni part ya pesa zilizotoka EPA, yeye hakutoa ruhusa kwa kampuni yoyote kuchukua pesa kama ulivyosema. Alicho sign ni barua kwenda kwa auditors period. The rest ni spin kwa sababu mnazozijua. Kujaribu kupotasha umma ni kuhujumu. You can't go wrong JF, information source!! Ukweli umepewa hapo chini
No Research no right to speak.Hakuwepo hazina wakati wa EPA,alikuwa maliasili fedha alikuwa mramba, Blunder alofanya ni kuingizwa choo cha kiume na Balali ku sign asokijua wakati wa Auditing, baadae alipostukia aka withdraw the statement.
 
Meghji abebeshwa zigo la Rostam CCM

ATAONGOZA KAMATI YA FEDHA NA VIFAA KATIKA UCHAGUZI MKUU
Ramadhan Semtawa

KATIKA kuweka sawa mpango mzima kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba, kamati kuu ya CCM imeteua watu wanne kuongoza kamati zake za ushindi, huku mbunge wa kuteuliwa, Zakia Meghji, akibebeshwa mzigo wa kamati ya fedha na vifaa.

Uamuzi huo wa kuteua majina hayo umechukuliwa katika kipindi ambacho serikali ya CCM imefanikiwa kupitisha sheria ya udhibiti wa matumizi ya fedha kwenye uchaguzi, sheria ambayo, pamoja na mambo mengine, itashughulikia masuala aliyopewa Meghji, ambaye alikuwa waziri wa fedha mwanzoni mwa utawala wa serikali ya awamu ya nne.

Meghji anachukua nafasi hiyo kumrithi mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ambaye alikuwa mweka hazina wa CCM na ambaye aliiongoza kamati hiyo wakati serikali ya awamu ya nne ikipambana kuingia madarakani mwaka 2005.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete vilieleza kuwa kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana, ambaye ni mjumbe wa kamati ya kutafiti chanzo na kutafuta suluhu ya uhasama miongoni mwa wana-CCM, ameteuliwa kuongoza kamati ya mikakati na uenezi.

Meghji aliiongoza Wizara ya Fedha na Uchumi katika baraza la kwanza la mawaziri la Rais Kikwete na akajiuzulu kabla ya kuundwa kwa baraza jipya huku kukiwa na habari za kuwepo kwa kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyosababisha Rais Kikwete kumfuta kazi gavana wa wakati huo, Daudi Balali.

Meghji sasa ataongoza kamati ambayo itashughulikia uandaaji mipango ya kifedha na ndiyo itashikilia fungu zima la bajeti ya chama katika mchakato mzima wa kampeni wa ngazi mbalimbali za uongozi ikiwemo urais, huku pia ikipanga na kuratibu upatikanaji wa vitendea kazi kama magari.

Alipoulizwa kuhusu maamuzi hayo, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba hakutaka kuweka bayana mpango huo, na akaeleza kuwa chama hicho kingetolewa taarifa ya maandishi kueleza maazimio ya kikao hicho.

"Wewe bwana nani kasema hizo taarifa wakati kikao ndiyo bado kinaendelea. Ngoja tutatoa taarifa rasmi muda si mrefu," alisema Makamba. Makamba alithibitisha CCM kujadili mpango mzima wa uchaguzi wa Oktoba, lakini akasita kueleza uamuzi wa kuteua kamati hizo.

Hata taarifa rasmi ya CCM haikutaja waliopewa nafasi hizo, lakini ilithibitisha moja ya ajenda iliyojadiliwa kwa kina na kikao hicho kuwa ni namna ya kufanya maandalizi kuhusu uchaguzi mkuu.

"Aidha, kikao hicho kilipokea na kujadili taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya ndani ya chama na miongoni mwa masuala hayo ni maandalizi ya Chama Cha Mapinduzi kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu," inaeleza taarifa kutoka ofisi ya katibu mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, sehemu kubwa ya ajenda za kikao hicho ilihusu maandalizi ya mkutano wa halmashauri kuu ya CCM uliopangwa kufanyika wiki hii.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa ajenda nyingine za mkutano huo ilikuwa ni kujadili mapendekezo ya wana-CCM wanaogombea nafasi ya katibu wa siasa na uenezi mkoani Dar es Salaam na mwenyekiti wa CCM wilayani Shinyanga Mjini.

"Kwa mujibu wa katiba ya CCM, mwisho wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa na halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo fupi ya aya tano.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kuwa Kinana ataongoza kamati hiyo ambayo itakuwa chini ya idara ya uenezi iliyo chini ya John Chilligati.

Wengine walioteuliwa na kamati hiyo ni Bibi Chikwinda ambaye ataongoza kamati ya mambo ya nje.

Wadadisi wa mambo ya siasa wanaona kwamba mpango huo umelenga kutoa nafasi kwa waliokuwa wakishikilia majukumu yao waweze kujipanga vema katika nafasi zao za kugombea majimboni.

Rostam anatarajiwa kutetea jimbo lake la Igunga huku Amos Makalla, ambaye naye ni mweka hazina wa CCM akitarajiwa kuwania ubunge wa jimbo la Mvomero ambako atapambana na mbunge wa sasa, Suleiman Sadiq Murad.

Chilligati ataelekeza nguvu zake kuwania ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki huku Benard Membe akiachiwa ajiandae na uchaguzi jimboni kwake Mtama.

Souce: Gazeti la Mwananchi

Hapo kwenye nyekundu, kujiuzulu lazima kuandika barua ya kujiuzulu. Meghji hakuchaguliwa kwenye baraza jipya baada ya reshuffle, lakini mimi sikumbuki kama alijiuzulu kama mwandishi alivyoweka hapo. Mwenye data kamili weka hapa
 
Back
Top Bottom