Amos Makalla nje, Zhakia Meghji ndani!

mkuu mara nyingi hizi Post za kuteuana haziangalii sana sifa za kielimu, Maslahi kwanza halafu elimu baadaye. Mtu anayeteua Anaangalia ni jinsi gani atakutumia na kufaidika na wewe, na unajua kuficha siri kiasi gani, Basi.

Nakubali ila angalia post yangu ya vyeo vya UTENDAJI versus SIASA. Ndo tunakosea Tanzania
 
Hii nimeipenda sana maana hata kama huna uhakika na jambo lenyewe bado unatanguliza malalamiko du. Sijuwi inakuwaje kwa mwendo huu. Yaaani hii inaitwa "Complains in advance". ili itakapotokea uwe umeshatimiza wajibu wetu wa kulalamika safi sana.

Na hii je: Nimesikia JK atamteua RA kuwa PM akishinda uchaguzi ujao na RA amekubali kugharamia gharama za kampeni za uchaguzi ujao kwa 75%.

Akimteua RA nitaamini kweli JK ni chaguo la Mungu! Atakua ameamua kuua chama kwa ujanja wa ajabu,lol
 
Hivi huyu JK mnamwita muungwana kwa nini?yaani siwaelewi mnaomwita muungwana ana uungwana gani?na kama hizi tetesi ni kweli basi it is another proof that we have a president ambaye hana ubongo...Huyu Meghji si ndio alisema kadanganywa na kaweka signature mihela ya EPA ?au naota???
 
Hiyo ya uwaziri mkuu haiwezekani

kama ameweza kusaini sheria ya uchaguzi bila kusoma na kuhamaki kuona viprngele vimechomekwa bila yeye kujua sishangai RA akiwa PM...kwa nini asiwe PM? kwani wengine wamekuwaje na yeye ashindwaje
 
Mkuu FP,

Ninakubaliana na nadharia yako, lakini inapowekwa kwenye utekelezaji, si CCM wala Rais ambaye hufuata hayo unayoyasema wewe.

Naomba nikuulize, kwenye orodha ya Watunza Hazina wa CCM waliopita, yupi kati yao alikuwa na utaalam wa fani ya Uhasibu?

Tuanze na Rostam Azziz ambaye alimrithi Mama Mbatia (RIP), then twende kwa Mama Mbatia mwenyewe na wengine waliowahi kushika nyadhifa hizo kabla. Je, walikuwa ni magwiji wa fani ya Uhasibu?

Tatizo wenyeji wa Mbagala sie huwa tunafikiria mambo yanaeenda inavyotakiwa.

Upo sahihi mzee
 
Hivi huyu JK mnamwita muungwana kwa nini?yaani siwaelewi mnaomwita muungwana ana uungwana gani?na kama hizi tetesi ni kweli basi it is another proof that we have a president ambaye hana ubongo...Huyu Meghji si ndio alisema kadanganywa na kaweka signature mihela ya EPA ?au naota???

Megji hakuweka signature ya Mihela ya EPA kama unavyo fikiri. Pesa za EPA zilitoka enzi ya Basili Mraba, chini ya Benjamin Mkapa, kabla ya Meghji kushika nafasi ya uwaziri wa fedha.

Megji, aliwaita kampuni ya Ernest Young kuchunguza mahesabu alipoingia wizara ya fedha. Kampuni hii iliona hii issue ya EPA iliyofanyika BoT. Waziri akapingwa mchanga wa macho na Balali kwamba hiyo issue ni ya usalama. Sasa kosa la Megji liko wapi ? Kama wewe ni waziri ungefanya nini? isitoshe issue kama zile ata mkulu anakua anafahamu.

Mgonja na Mkulo ambaye sasa ni waziri wa fedha atakua anaijua hii issue fika. Mkulo alikuwepo wizarani wakati hii issue inatokea. Yuko pale sasa hizi kumlinda RA na issue ya Kagoda, kazi ambayo asingefanya Meghji... Rudi kwenye interview ya MKJJ
 
Megji hakuweka signature ya Mihela ya EPA kama unavyo fikiri. Pesa za EPA zilitoka enzi ya Basili Mraba, chini ya Benjamin Mkapa, kabla ya Meghji kushika nafasi ya uwaziri wa fedha.

Mkulo Yuko pale sasa hizi kumlinda RA na issue ya Kagoda, kazi ambayo asingefanya Meghji... Rudi kwenye interview ya MKJJ
.
Wengi bado wanapotea maboya kuwa Kagoda ni RA, no, RA was just a medium, the means, master mind ni BWM na chief wake wa TISS. RA aliwapatia tuu means na medium ya siphoning!.
 
Nadhani tumefanya speculation ya kutosha na hata ku-enter verdict bila hata kujua kitakachojadiliwa kwenye hicho kikao (kama kweli kitakuwepo). Ili tusiendelee kutabiri hata ambayo hayatajadiliwa, ni vizuri sasa tukasubiri kuona au kusikia kitakachojiri na hapo ndiyo tutatoa hukumu kwa facts ambazo ziko sahihi.
 
Tangu lini? Angepata muda wa kusoma CPA?
hata kama ana CPA(T) ,ama ACCA,CIMA AU VYOVYOTE IWAVYO, hakuna mafungamano na uadilifu, unapoona wale kina Balali, Yona ,Mramba ama wezi wengine wa mali za umma usidhani hawana elimu ya kutosha katika taaluma zao.
wapo madaktari wa falsafa , wamebobea kwelikweli kwenye taaluma zao, lakini ndio mafisadi papa hapa Tanzania.
Elimu ama kutokua na elimu , hoja ni namna gani kijana anajiheshimu na kujitenga na ufisadi.
Makalla ni kijana ambae kaishaonja tamu ya Ufisadi, kaisha nufaika nao kwa namna moja ama nyingine, kwa vijisenti vya mafisadi papa amekua akimsumbua sana mbunge wa jimbo la Mvomero katika kutimiza majukumu yake, huu ni mwaka wa pili na nusu tangu makala aanze harakati za kisiasa za kuutaka ubunge wa mvomero, amekua akipewa suppor na watuhumiwa wengi wa ufisadi.
 
Anachofanya JK kwa sasa ni kuunda upya timu yake ya kampeni mbali na ile ya 2005 ya akina RA na EL na wanamtandao wengine ambao kwa muda huu wa miaka mitano wamejichafua na kuchafuliwa sana. Mama Meghji ni mtu wa karibu na anamwamini sana. Anataka kumkabidhi mfuko wa mahela ya kampeni. Kinana naye ameonekana siku zote kuwa mtu asiye na kashfa wala makundi ndani na nje ya CCM. Labda la kujiuliza hapa ni kwa nini mahela haya ya kampeni yanaweka nje ya mfumo wa kawaida wa masuala ya fedha ya CCM?
 
Anachofanya JK kwa sasa ni kuunda upya timu yake ya kampeni mbali na ile ya 2005 ya akina RA na EL na wanamtandao wengine ambao kwa muda huu wa miaka mitano wamejichafua na kuchafuliwa sana. Mama Meghji ni mtu wa karibu na anamwamini sana. Anataka kumkabidhi mfuko wa mahela ya kampeni. Kinana naye ameonekana siku zote kuwa mtu asiye na kashfa wala makundi ndani na nje ya CCM. Labda la kujiuliza hapa ni kwa nini mahela haya ya kampeni yanaweka nje ya mfumo wa kawaida wa masuala ya fedha ya CCM?

Sio fedha safi.....
 
Kudadadeki........, jamaa kajusahau sana, bendi zimuimbe yeye na ubunge wa mvomero atake yeye, kweli anafuja hela kwa mantiki hiii.Achape lapaaaaaaaaaaa.
 
Kama ni kweli, basi JK atakuwa anaruka mkojo anakanyaga mavi. Kumrudisha yule aliyeidhinisha malipo BoT yasiyokuwa na kichwa wala miguu!! Meghji anajua pale alipozipeleka hizo fedha haramu yeye na Mrhm. Balali.
Anyway, tusubiri ukweli, maana bado ni tetesi.
No Research no right to speak.Hakuwepo hazina wakati wa EPA,alikuwa maliasili fedha alikuwa mramba, Blunder alofanya ni kuingizwa choo cha kiume na Balali ku sign asokijua wakati wa Auditing, baadae alipostukia aka withdraw the statement.
 
Makalla na wanaCCM woote kasoro mzee Mwinyi ni kundi la WEZI na Wafujaji, sasa inapotokea wanaibiana wenyewe kwa wenyewe sasa hayo ndio matokeo yake.
 
Meghji abebeshwa zigo la Rostam CCM

ATAONGOZA KAMATI YA FEDHA NA VIFAA KATIKA UCHAGUZI MKUU
Ramadhan Semtawa

KATIKA kuweka sawa mpango mzima kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba, kamati kuu ya CCM imeteua watu wanne kuongoza kamati zake za ushindi, huku mbunge wa kuteuliwa, Zakia Meghji, akibebeshwa mzigo wa kamati ya fedha na vifaa.

Uamuzi huo wa kuteua majina hayo umechukuliwa katika kipindi ambacho serikali ya CCM imefanikiwa kupitisha sheria ya udhibiti wa matumizi ya fedha kwenye uchaguzi, sheria ambayo, pamoja na mambo mengine, itashughulikia masuala aliyopewa Meghji, ambaye alikuwa waziri wa fedha mwanzoni mwa utawala wa serikali ya awamu ya nne.

Meghji anachukua nafasi hiyo kumrithi mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ambaye alikuwa mweka hazina wa CCM na ambaye aliiongoza kamati hiyo wakati serikali ya awamu ya nne ikipambana kuingia madarakani mwaka 2005.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete vilieleza kuwa kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana, ambaye ni mjumbe wa kamati ya kutafiti chanzo na kutafuta suluhu ya uhasama miongoni mwa wana-CCM, ameteuliwa kuongoza kamati ya mikakati na uenezi.

Meghji aliiongoza Wizara ya Fedha na Uchumi katika baraza la kwanza la mawaziri la Rais Kikwete na akajiuzulu kabla ya kuundwa kwa baraza jipya huku kukiwa na habari za kuwepo kwa kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyosababisha Rais Kikwete kumfuta kazi gavana wa wakati huo, Daudi Balali.

Meghji sasa ataongoza kamati ambayo itashughulikia uandaaji mipango ya kifedha na ndiyo itashikilia fungu zima la bajeti ya chama katika mchakato mzima wa kampeni wa ngazi mbalimbali za uongozi ikiwemo urais, huku pia ikipanga na kuratibu upatikanaji wa vitendea kazi kama magari.

Alipoulizwa kuhusu maamuzi hayo, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba hakutaka kuweka bayana mpango huo, na akaeleza kuwa chama hicho kingetolewa taarifa ya maandishi kueleza maazimio ya kikao hicho.

"Wewe bwana nani kasema hizo taarifa wakati kikao ndiyo bado kinaendelea. Ngoja tutatoa taarifa rasmi muda si mrefu," alisema Makamba. Makamba alithibitisha CCM kujadili mpango mzima wa uchaguzi wa Oktoba, lakini akasita kueleza uamuzi wa kuteua kamati hizo.

Hata taarifa rasmi ya CCM haikutaja waliopewa nafasi hizo, lakini ilithibitisha moja ya ajenda iliyojadiliwa kwa kina na kikao hicho kuwa ni namna ya kufanya maandalizi kuhusu uchaguzi mkuu.

"Aidha, kikao hicho kilipokea na kujadili taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya ndani ya chama na miongoni mwa masuala hayo ni maandalizi ya Chama Cha Mapinduzi kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu," inaeleza taarifa kutoka ofisi ya katibu mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, sehemu kubwa ya ajenda za kikao hicho ilihusu maandalizi ya mkutano wa halmashauri kuu ya CCM uliopangwa kufanyika wiki hii.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa ajenda nyingine za mkutano huo ilikuwa ni kujadili mapendekezo ya wana-CCM wanaogombea nafasi ya katibu wa siasa na uenezi mkoani Dar es Salaam na mwenyekiti wa CCM wilayani Shinyanga Mjini.

"Kwa mujibu wa katiba ya CCM, mwisho wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa na halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo fupi ya aya tano.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kuwa Kinana ataongoza kamati hiyo ambayo itakuwa chini ya idara ya uenezi iliyo chini ya John Chilligati.

Wengine walioteuliwa na kamati hiyo ni Bibi Chikwinda ambaye ataongoza kamati ya mambo ya nje.

Wadadisi wa mambo ya siasa wanaona kwamba mpango huo umelenga kutoa nafasi kwa waliokuwa wakishikilia majukumu yao waweze kujipanga vema katika nafasi zao za kugombea majimboni.

Rostam anatarajiwa kutetea jimbo lake la Igunga huku Amos Makalla, ambaye naye ni mweka hazina wa CCM akitarajiwa kuwania ubunge wa jimbo la Mvomero ambako atapambana na mbunge wa sasa, Suleiman Sadiq Murad.

Chilligati ataelekeza nguvu zake kuwania ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki huku Benard Membe akiachiwa ajiandae na uchaguzi jimboni kwake Mtama.

Souce: Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom