Amos Makalla nje, Zhakia Meghji ndani!

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Kuna Tetesi kuwa Mwungwana kamtema Amos Makala kutoka nafasi ya Mtunza Hazina wa Chama, na kumteua Zhakia Meghji kuchukua nafasi yake.Kama tetesi hii ina ukweli, naamini la Kuvunda halina ubani.
 
Hata kama sio Megji, ndani ya CCM kabakia Makufuli tu, japo hata naye sina uhakika sana
 
FMES amesema kuna mkutano wa dharura tarehe 28/03/2010, tusubiri tuone.

In the meantime......

Hamna mtu ndani ya chama anaweza kukomesha haya mambo jamani?

Mtu alituhumiwa kwa MATUMIZI MABAYA YA FEDHA katika wizara aliyokuwa anaongoza halafu kabla hata uchunguzi juu yake haujakamilika (hatujaambiwa) anapewa madaraka ya fedha ya chama?
 
Kuna Tetesi kuwa Mwungwana kamtema Amos Makala kutoka nafasi ya Mtunza Hazina wa Chama, na kumteua Zhakia Meghji kuchukua nafasi yake.Kama tetesi hii ina ukweli, naamini la Kuvunda halina ubani.

Kama ni kweli, basi JK atakuwa anaruka mkojo anakanyaga mavi. Kumrudisha yule aliyeidhinisha malipo BoT yasiyokuwa na kichwa wala miguu!! Meghji anajua pale alipozipeleka hizo fedha haramu yeye na Mrhm. Balali.
Anyway, tusubiri ukweli, maana bado ni tetesi.
 
La kuvunda halina ubani sasa jamani mnataka amteua nani ambaye ni msafi Sofia Simba alishatuhabarisha longi kuwa CCM hakuna msafi wote ni wachafu wananuka na sasa wanazidi kujichafua teh teh
 
Huyu Makala ni yule anayegombania jimbo huko Morogoro na yule Mhindi?
Kama ndivyo basi hawa wahindi ni kiboko!
Anasaka hela ya kugombania ubunge?? Duh.....
 
Sisi ndo tunawapigia kura, hasa wale ambao hawajiandikishi au wanajiandikisha lkn hawapigi kura, kwa kususia kupiga kura hawa jamaa wataendelea kutafuna mafao tu kila siku na hizi kelele zetu.. Zitakuwa zile za chura ambazo hazimzuii ng'ombe kunywa maji
 
wat is JK doing,anaemtoa na anayemuweka wote ni wabovu.hivi ccm imeisha watu makini au ndio msemo wa kwamba jamaa hashauriki ndio unazidi kujidhihirisha?
 
mlitaka mpewe ninyi hiyo nafasi? maana kila kitu akifanya kwenu ni kosa, utafikiri ninyi ndio wenye maamuzi sahihi. na inawezekana hata maamuzi katika familia zenu hamuwezi laqkini mkiwaona wenzinu mnachonga mbaya
 
Zhakia anajua vizuri system ya fedha ya Tanzania kwa sababau amekuwa waziri mwandamizi wa wizara husika, kwa hiyo ni mtu muhimu katika CCM hasa hasa kuelekea uchaguzii mkuu.

Mimi stoshangaa kama itakuwa kweli, Namtakia kila la kheri.
 
FMES amesema kuna mkutano wa dharura tarehe 28/03/2010, tusubiri tuone.


Hamna mtu ndani ya chama anaweza kukomesha haya mambo jamani?

Mtu alituhumiwa kwa MATUMIZI MABAYA YA FEDHA katika wizara aliyokuwa anaongoza
Kwani yeye ametuhumiwa kivipi?
Kwanza angalia matumizi ya fedha za EPA yalipofanyika yeye hakuwa Waziri wa Fedha.
Pili ni kwamba kwa mfumo wa wakati ule (sina hakika kama kumetokea mabadiliko) Gavana wa BoT hawajibiki wa Waziri wa Fedha.
Aliwajibika kwa kukubali kudanganywa na Balali na sio matumizi mabaya ya fedha. Na inawezekana hata kama ungekuwepo wewe ungefanya uamuzi ule ule.
 
Jamani inasekekana kamati ya utekelezaji CCM makao makuu wote wanataka kugombea ubunge isipokuwa makamba tu!na hiyo kamati inatakiwa iwe active kipindi cha uchaguzi sasa wakiwa busy na kugombea ubunge nafasi zao zitashikiliwa na nani?Mkuchika,Makalla,Chiligato,Shigella wote wanataka ubunge kipindi cha uchaguzi !wakubwa wanaona ni bora kubadili nafasi zao ili wapate timu itakayo wajibika kipindi cha uchaguzi!
 
''Kama ni kweli, basi JK atakuwa anaruka mkojo anakanyaga mavi. Kumrudisha yule aliyeidhinisha malipo BoT yasiyokuwa na kichwa wala miguu!! Meghji anajua pale alipozipeleka hizo fedha haramu yeye na Mrhm. Balali.
Anyway, tusubiri ukweli, maana bado ni tetesi''

Idume umesema! Mi najiuliza je zile fedha c kuna fununu zilitumika kwa gharama za kapeni za chama dume ktk uchaguzi ulio mwingza mkuu madarakani, inawezekana akawa anataka kumtumia tena huyu mama kwa uzoefu wake namna ya kupata fungu la gharama za uchaguzi.
 
Wewe Kafiribangi na Injinia it appears you are not informed at all. Hela ya EPA na matumizi hayo mabaya Waziri wa Fedha hakuwa Meghji jamani. Meghji alipewa portfolio hiyo ya Fedha baada ya JK kuwa Rais. Hivi mbona hamna jema nyinyi watu? Wakati JK is working so hard to deal na ufisadi in his own unique way within a rotten system not of his creation badala ya kumuunga mkono mko busy kumkandia. Lo shame on you!! Inaelekea nyie kama mmmeoa au kuolewa basi spouses weni watakuwa wanaumia sana. Maana mna gubu haswa.
 
Back
Top Bottom