Amos Makala Vs. Viongozi wa Chadema

Hivi kuna mtu ana CV ya huyu Makala? Naona hata kama hayuko sahihi kwenye baadhi ya mambo lakini anapangua hoja kisomi sio kama akina Makamba au Chiligiti (kama sijakosea jina).

Naomba mwenye CV yake.
 
Mkataba mwingine tata UV-CCM
Kizitto Noya na John Dotto

WAKATI timu ya kuchunguza utata wa mkataba wa jengo la Umoja wa Vijana wa

Chama cha Mapinduzi (UV-CCM) ikiendelea na kazi yake, imebainika kuwa

uongozi wa umoja huo ulishawahi kuingia mkataba mwingine tata na

mwekezaji kwa ajili ya kuendeleza jengo hilo.


Habari zilizopatina kutoka ndani ya CCM zinaeleza kuwa umoja huo,

kupitia kampuni yake ya Vijana Development Corporation Ltd iliyoundwa

kwa ajili ya kuendeleza jengo hilo lililo kiwanja namba 1081 na 1082, uliingia mkataba na kampuni ya Mek-One Traders ya jijini Dar es salaam Aprili 24 , 2003.


Imeelezwa kuwa katika makubaliano hayo ambayo Mwananchi imeona nakala yake, Vijana Development Corporation Ltd iliwakilishwa na mweka hazina wa wakati huo wa umoja huo, Amos Makala ambaye akawa sasa ni Mweka Hazina wa CCM, pamoja na mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Mohamed Seif Malinda.


Kampuni ya Mek-One General Traders Ltd iliwakilishwa na mkurugenzi wake, Mohamed Edha Awadh, mbele ya Mwanasheria, Paul Faustine Kihwelo wa jijini Dar es Salaam.


Kwa pamoja walikubaliana kuanzisha kampuni iliyoitwa Mek-One Vijana Development Investment Ltd kwa ajili ya kutekeleza mradi huo na kampuni ilisajiliwa kwa Msajili wa Makampuni kwa 45980 /Mei 13, 2003.


Kampuni hiyo ya ubia ilitakiwa kujenga jengo kubwa la ghorofa ambalo

lingetumika kwa ajili ya kupangisha shule ya kimataifa na eneo jingine

kutumika kupangisha ofisi mbalimbali na mapato yangeingia katika mfuko wa UV CCM na mwekezaji huyo.


Hata hivyo, makubaliano ya mradi huo yameingia doa baada ya uongozi wa

UV-CCM kupoteza maelewano na mkurugenzi wa Mek-One, Mohamed Awadh.


Imeelezwa kuwa chanzo cha mgogoro wao ni pale uongozi wa juu wa UV-CCM ulipokatisha ghafla mawasiliano na Awadh na kumgeukia

mwekezaji mpya, ambaye mkataba wake sasa ndio ulioelezwa na Nape Nnauye kuwa una kasoro na sasa unachunguzwa na timu maalum ili kuhakikisha maslahi ya chama yanazingatiwa.


Inaelezwa kwamba mwekezaji huyo hakukubaliana na hatua hiyo hivyo aliamua kutafuta njia mbadala ya kunusuru mkataba huo, ikiwa ni pamoja na kuwaona viongozi wa juu wa CCM, lakini hajafanikiwa.


Habari za uhakika zinaeleza kuwa mkurugenzi huyo alifikisha

malalamiko yake hata Ikulu ambako baadaye waliushauri uongozi wa Umoja wa

Vijana kumrejeshea gharama zake endapo wangependa kuvunja uhusiano naye.


Hata hivyo, mpaka sasa suala hilo bado linaendelea huku baadhi ya viongozi

wa umoja huo wakitaka lisilipuke kwa kutoa maelezo kuwa mwekezaji huyo

alikuwa na kasoro ndio maana wakaamua kumwacha.


Mweka hazina wa CCM, Amos Makala alikiri kuwepo kwa makubaliano hayo na kwamba wakati huo akiwa UV-CCM waliingia katika makubaliano na Mek-One General Traders kwa lengo la kuendeleza eneo hilo, lakini akakanusha kuhusu kusaini mkataba.


"Ni kweli tulikuwa na mazungumzo ya awali na Bwana Awadh... mapendekezo yetu tuliyapeleka sekretarieti na baadaye kamati ya utekelezaji ambako tulitakiwa kuelewa uwezo wa kiuchumi wa kampuni ya mwekezaji, lakini baadaye ikagundulika kuwa hakuwa na uwezo wa kuwekeza," alisema Makala.


Aidha alisema baada ya kubaini upungufu huo, walipoamua kuachana

naye na akaongeza kuwa wao kama viongozi wa UV-CCM wa wakati huo hawakuchukua hata senti kutoka Mek-One General Traders.


Alipoulizwa ilikuwaje mpaka wakafikia hatua ya kusajili kampuni ya pamoja

Brela na mwekezaji huyo kama walikuwa hawajui uwezo wake, Makala alisema

hilo ni jambo la kawaida katika mikataba.


"Kwani wewe ukioa mahali fulani halafu baadaye wakwe zako wakakataa kumwoa binti yao, utauliza sababu za kukataliwa," alihoji Makala.


Makala aliongeza kuwa kumekuwa na taarifa za kupotosha juu ya makubaliano

hayo na tayari Awadh alishafika mpaka Ikulu kwenda kulalamika na

wao walishatoa maelezo juu ya suala hilo kwa ujumla.


"Huyu mtu alishakwenda mpaka kwa Mtawa Ikulu na kwa Mzee Rashid Kawawa na sehemu nyingine kulalamika, lakini sisi tulishatoa ufafanuzi wa suala

hili Ikulu na lilishakwisha," alisema Makala.


Alisema uongozi wa Mek-One General Traders kama unaona kuna uonevu juu ya suala hilo una haki ya kwenda mahakamani ambako ndipo kuna haki.


Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Awadh alikiri kuingia mkataba na UV-CCM na kwamba hivi sasa ana mgogoro na umoja huo.


Alisema hataki kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa kuwa anajua haki yake ataipata kupitia njia za kawaida na sio magazeti.


Hivi kariubuni, kamati kuu ya chama hicho iliunda timu ya watu watatu

kurekebisha kasoro zilizopo katika mkataba wa sasa wa ujenzi wa jengo hilo

na mwekezaji mpya.


Wanaounda kamati hiyo ni Andrew Chenge, Pindi Chana na Dk Abdallah Kigoda, ambao ni wajumbe wa kamati kuu ya CCM.


Timu hiyo kwa kushirikiana na UV-CCM inatakiwa kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika mkataba huo na kuendelea kushauri hatua kwa hatua za utekelezaji wa mradi huo.


Mkataba wa Mradi wa ujenzi wa kitega uchumi cha UV-CCM wenye thamani ya Sh 30 bilioni, ulianza kulalamikiwa mapema mwaka huu na baadhi ya wana CCM na wanachama, wakiongozwa na Nape Nnauye, ambaye alieleza bayana kuwa hauna maslahi kwa umoja na kwamba ulipitishwa bila ya kuepelekwa kwenye vikao husika.


Nape alivuliwa uanachama wa UV-CCM na Baraza Kuu kutokana na sakata hilo, akidaiwa kusema uongo.


Sakata hilo la kusainiwa kwa makubaliano ya ubia huo pia lilimhusisha

mwenyekiti wa baraza la wadhamini, Edward Lowassa ambaye anadaiwa kusaini makubaliano hayo.


Inaelezwa kuwa baadhi ya kasoro zilizogundulika kuwa ni kutokueleza madaraka ya bodi ya wakurugenzi kwa pande zote mbili; kutokuweka wazi mchakato mzima wa uendelezaji wa jengo hatua kwa hatua; na kutokuweka wazi hatua za kusuluhisha migogoro endapo itajitokeza.


Kwa mujibu wa mkataba huo, UVCCM itamiliki asilimia 25 na wa bia asilimia

75 na hauna ukomo.

Chanzo: Mwananchi
 
MEI 27, 2006, Naibu Katibu Mkuu UV-CCM Bara, Amos Makala aliupotosha umma kuhusu tathmini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ya siku 100 za Rais Jakaya Kikwete madarakani.

Makala katika hotuba aliyoitoa wilayani Temeke wakati wa ziara yake ya kuwashukuru vijana wa Chama Cha Mapinduzi, alisema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa kauli kuwa Rais Kikwete amekuwa mtu wa kutoa ahadi, kuzunguka na kutokaa ofisini.

Makala alidai Kikwete anafanya hivyo kuonyesha anawajali wananchi na matatizo yao na ndiyo maana anazunguka ili ajue na kufanya utafiti kwa lengo la kuyashughulikia.

Nimeamua kumjibu Makala kwa masilahi ya Watanzania wakiwamo vijana wa CCM wenyewe ambao Makala amekuwa akizungukia katika wilaya kadhaa na kuwapotosha kwa kutumia ujumbe huu.

Makala hakulielewa tamko la CHADEMA la siku 100 za Kikwete.

Katika tamko la CHADEMA, kipengele cha pili sehemu ya mafanikio, Mbowe alisema serikali imerejesha matumaini ya kinadharia kwa wananchi.

Mbowe alimsifu Rais Kikwete kwa kuonyesha kuwa karibu na wananchi na kwamba amevunja uzio uliojengwa na awamu ya tatu wa kutenga kwenye tabaka moja, viongozi wa serikali na CCM, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa katika upande mmoja, na wapinzani, waandishi wa habari, wakulima, wafanyakazi na wananchi maskini katika upande mwingine.

Hakumaanisha asiwe karibu na wananchi wala asiwatembelee kama Makala anavyotaka kuwasadikisha Watanzania.

Ieleweke kwamba, hoja ya Mbowe si Kikwete kutokuwa karibu na wananchi bali Kikwete kushughulikia matatizo ya wananchi kwa kuipatia nchi uelekeo.

Rais amekuwa akizunguka huku na kule, mara leo yupo gerezani, kesho sokoni na keshokutwa Muhimbili, lakini kote huko hakuna matokeo ya kutosha yanayoonekana, hakuna kinachobadilika na katika baadhi ya maeneo hali imezidi kuwa mbaya.

Kikwete anayafahamu vizuri matatizo ya Watanzania. Hii ndiyo hoja ambayo CCM ilikuwa ikiisema wakati wa kampeni na kujivunia kwamba tayari alishakuwapo katika utawala kwa muda mrefu, hivyo anafahamu hali halisi ya Watanzania.

Vipi leo Makala atake Kikwete apite kuyafahamu matatizo ya wananchi? Hoja ya Makala kuwa Rais anawatembelea wananchi ili kufanya utafiti haina msingi, kwani matatizo ya Watanzania yapo wazi. Na kama itabidi utafiti ufanyike, hauwezi kufanywa na Rais kwa kuzunguka sokoni na hospitalini.

Serikali inatumia mabilioni ya pesa kudhamini tafiti mbalimbali na kama Makala anasema Rais anapita sokoni ili kufanya utafiti, kuna sababu gani ya kutumia mabilioni ya walipa kodi maskini wanaokufa kwa njaa kugharimia tafiti za umaskini?

Katika mifumo ya utawala kuna mfumo wanaita ‘Management by Walking Around' na kipimo ni namna kiongozi anavyoweza kuzungukia na kukagua, na pili kuna “Management by Results or Objectives” ambapo matokeo na malengo ndiyo kigezo cha kupima mafanikio ya utawala.

Sasa Rais ameamua kutumia staili ipi? Na je, Watanzania wanataka staili ipi? Wanataka kutembelewa pekee au matokeo ya ufumbuzi wa matatizo yao ?

Kimsingi hakuna maana yoyote kwa Rais kutembelea masoko kwa madai ya kujionea hali halisi ya bei zilivyopanda halafu hakuna kitu kinachobadilika baada ya hapo.

Wala hakuna maana yoyote Rais kutembelea hospitali anakuta wagonjwa wanalala sakafuni halafu baada ya hapo hakuna kinachoendelea.

Wagonjwa hawawezi kupona kwa kutembelewa na Rais, wala bei haziwezi kushuka kwa sababu Rais katembelea soko.

Wagonjwa wanapata huduma bora na bei zinashuka kwa maamuzi ya kisera na kimwelekeo.

Rais kama kiongozi wa juu anapaswa kuwapanga viongozi watendaji wake ili waweze kutekeleza majukumu yao . Ndiyo maana tunaamini kwamba wakati umefika wa Rais kuwaongoza watendaji wengine na wao wawaongoze watendaji wa chini yao hadi tufike wakati ambapo hata mwenyekiti wa kijiji au mtaa anatembelea wananchi na kutatua kero zao.

Kwa upande mwingine, sababu ya Mbowe kumshukia Kikwete aache kuendelea kuahidi, kumetokana na ukweli kuwa wakati wa kampeni CCM ndicho chama kilichoongoza kwa ahadi nyingi.

Mathalani, Rais aliahidi kuwa serikali itaanza kujenga kiwanda cha mbolea mwaka huu, hadi sasa bado haijaeleweka hata ni wapi kiwanda hicho kitajengwa na sasa tunaelekea katikati ya mwaka.

Wakati akizitembelea wizara, Rais alidai kuwa anasikitishwa na viongozi kutembelea mashangingi huku wananchi wanakula mlo mmoja, lakini bado mashangingi yameshamili wakati wananchi wanaendelea kuteseka.

Hoja ya Mbowe si kumhukumu Kikwete katika muda huu ambao kimsingi bado ni mapema, hoja ya Mbowe ni kumuasa Rais kuendelea kuporomosha ahadi. Hii ni hoja ya kizalendo inayopaswa kuungwa mkono.

Upungufu wa Rais kutotulia na kuweka mambo sawa sote tumeuona, kwa muda mfupi tangu aingie madarakani amekuwa akitofautiana na hata mawaziri wake kuhusu mwelekeo wa masuala ya msingi.

Mathalani Rais alitangaza bei ya umeme isingepanda na kwamba lazima TANESCO ihakikishe bei inashuka, muda mfupi baadaye waziri wake wa fedha anakanusha, na kwamba bei ya umeme lazima ipande.

Nasisitiza kauli ya Mbowe kwamba Rais akae ikulu aipatie nchi visheni, tofauti na hapo atakuwa hapingani na kauli yake kuwa nchi haiwezi kuendeshwa kwa misheni town.


Source: Nchi haiendeshwi kwa misheni town
 
Kama huyu Makala anayesifiwa CCM ndiye anayeongea upuuzi niliosoma hapo juu, basi bado tuna safari ndefu sana.

Inakuwaje huyu Makala alinganishe watu walioiba Mabilioni ya fedha za umma kwa manufaa yao binafsi na watu waolishindwa kutimiza ahadi kutokana na mifuko yao binafsi? Ingawa kutotimiza ahadi ni kosa, lakini ukweli ni kuwa kosa hilo halilingani na la wizi wa mali ya umma. Inaelekea kuwa Makala hajui maana ya neno fisadi anapodai kuwa Mbowe ndiye fisadi mkubwa kwa kuwa aliahidi kutoa pikipiki zenye thamani ya Shs 78m, lakini hakufanya hivyo. Kwake yeye aliyeiba bilioni 40 hana hatia ila yule alyeshindwa kutumiza ahadi ya kutoa milioni 78. Duh!!!, hiyo ni kali sana!!

Halafu kama kweli ana uhakika kuwa CCM haihusiki na hizo tuhuma za EPA, basi si atoe ruhusa mahesabu ya chama hicho yakaguliwe? Kukataa kukaguliwa huku akidai kuwa hakuna uhusiano baina ya CCM na fedha hizo za EPA ni ukigegugeu(hypocricy) wenye kuficha ukweli.
 
Hii kesi ya Fisi na mbwa kumshtakia Mbuzi kwa
Simba na chui. Wote mnajua kesi za namna hii zilivyo! Lakini pia unaweza kukuta ni danganya toto. Je, mshtaki ana mahekalu na magari mangapi. Fedha yoooote ya CCM ilikuwa salama mikononi mwake? Au hawa jamaa ndio wale wanaoitumia CCM kuchukua bilioni 4 BOT kisha wakaipa CCM milioni 400 na wao kubakia na bilioni 3.6?
 
Amos Makala is a clever man and gud man , hana kashfa yoyote ya ufisadi ,that is why jk appointed him mweka Azina wa CCM taifa
 
Amos Makala is a clever man and gud man , hana kashfa yoyote ya ufisadi ,that is why jk appointed him mweka Azina wa CCM taifa

Jk pia alimteua Mgonja kuwa Katibu Mkuu wa Fedha wa Taifa la Tanzania. Na Yona na Mramba nao waliteuliwa kitu gani vile? What about Rostam Aziz? Hakuwa mshika mikoba wake pia?

Asha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom