Amma kwa hakika saa ya ukutani haivaliki mkononi !

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Wana wa Jamii haijapita hata wiki kabla hata mate yangu, hayajaanguka chini.
Nilishuka na Thread hapa iliyokua na headin' "HII NYUMBA INAKALIKA ? "
Ushauri niliokua nimeomba ni kumhusu Kaka yangu, alietaka nimshauri kua amepata offer toka kwa Baba mkwe wake kwamba ahame katika nyumba aliyokua amepanga na akaishi kwenye nyumba ya mkwewe pamoja na familia yake.
Kaka yangu akihofia huenda huko mbeleni angekumbana na manyanyaso ndiyo chanzo cha kunitaka ushauri.
Hapa jirani kuna bwa-mdogo ambae alikua ameajiriwa kwenye duka la kuuza simu, ambapo girl frnd wake alikua akimiliki duka la hardwire (duka alilorithi toka kwa marehemu babaake).
Bwa-mdogo akapiga (akaiba) kiasi cha fungu kwa muajiri wake kosa lililomsababishia afukuzwe kazi.
Next Bwa-mdogo akajichanganya dukani kwa girl wake na alichotoka nacho kule alikofukuzwa akakichanganya kwa girl frnd wake na wakawa wote wapo dukani.
Bwa-mdg hakuishia hapo akahama na ktk chumba chake na kuhamia kwa mususu (girl frnd).
Hivi majuzi wakiwa wote dukani simu ya girl ikawa inaita, girl akipokea akisema namnukuu "umepaki hapo kwa mbele haya nakuja" (mwisho nukuu na maneno haya ni kwa maelezo toka kwa bwa-mdg).
Girl alitoka hadi nyumba ya 3 kutoka dukani hapo.
Suzuki iliyokua imesimama akashuka mwanaume aliyekua amevalia kipedezshee walikumbatiana na ku'hug na girl.
Hayo yakifanyika bw-mdg kasimama nje ya duka akiona, kilichofata girl kurudi dukani bw mdg alipojaribu kuleta kidomodomo aliamriwa atoke eneo la duka mara moja au anamuitia polisi.
Bw- mdg alisalim amri na kuondoka girl alifunga duka na kuondoka, haijulikani kama ndiyo alimfuata yule jamaa au vipi.
Usiku bw-mdg aliporudi hom kw girl akakuta begi lake liko mlangoni nje.
Akaamua kabla hajachukua begi nakuondoka ni bora agonge amwambie girl amkatie M zake mbili alizozitia dukani, akaambiwa alete maandishi yake ya kuthibitisha suala hilo.
Maandishi ambayo bw mdg hakuanayo kwani hakutegemea kama hayo yangekujakujiri. Polepole akaanza kuchanganya kwato, begi begani mfukoni chwee na girl hanae tena!
AMA KWELI SAA YA UKUTANI HAIVALIKI MKONONI !
 
Ebwana usidanganyike hata siku moja kwenda kuishi ukweni, hutakuwa na kauli nafasi yako kama mume itakwisha zaidi hutakuwa na mamlaka, hutaweza kukoroma mkuu.
kuishi kwako hata kama mnalala chini ni uhuru.
 
Duuh!pole zake, ni ajipange upya tu..ila nayeye aache wizi bana watamkili isee
 
Dhuluma huisha kwa dhuluma!mwanaume anayekubali mporomoko wa maisha na kwenda kuishi kwa wakwe au kwa mpnz wake hana cfa za uanaume bali kavulana na kufukuzwa na beg mkonon halali yake awapishe wanaume,ebo!
 
Kwahiyo mwizi nae kaibiwa?

Ili tuitendee haki fasihi andishi nadhani tuseme bwa-mdogo kaingizwa mjini ! Nachelea kumwita mwizi kwa kua hakufikishwa kotini.
Japokua bwa mdg kwa maelezo yake mwenyewe kwetu anakiri alimtoka ex tajiri yake.
 
Dhuluma huisha kwa dhuluma!mwanaume anayekubali mporomoko wa maisha na kwenda kuishi kwa wakwe au kwa mpnz wake hana cfa za uanaume bali kavulana na kufukuzwa na beg mkonon halali yake awapishe wanaume,ebo!

Pwenti
 
Pwenti ! Umefikiri!
 
Ili tuitendee haki fasihi andishi nadhani tuseme bwa-mdogo kaingizwa mjini ! Nachelea kumwita mwizi kwa kua hakufikishwa kotini.
Japokua bwa mdg kwa maelezo yake mwenyewe kwetu anakiri alimtoka ex tajiri yake.
Mwanzo umeandika aliiba ila sasa unachelea kumuita mwizi?
 
si uivae shingoni?
FlavorFlav_M_Tr_11064695_600.jpg
 
Uko msemo husemwa ukikosea kuchagua mke umekosea maisha.
Mwanamke sio nguo ukasema nikikaa nae mwaka 1 nikiona hatuendani namrudisha kwa fundi akamfumue amshone upya! Once you do a mistake is a mistake! To back on the rite path is incridible!
 
si alkua analala na kula bureee!!!???
kiburudisho je alkua analipia kila asubuhi??
nimeipendasana hiiii
hahahahaaaaaaaaaaaaa mwosha huoshwa
 
Ebwana usidanganyike hata siku moja kwenda kuishi ukweni, hutakuwa na kauli nafasi yako kama mume itakwisha zaidi hutakuwa na mamlaka, hutaweza kukoroma mkuu.
kuishi kwako hata kama mnalala chini ni uhuru.

Hunter ! Hili nalo NENO !
 
Back
Top Bottom