Amkeni wajameni

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Mwezi mmoja uliopita wananchi wakiongozwa na wazee wa Dar walikusanyka na kumpongeza mheshimiwa baba mwenye mji, JMK, kwa kusitisha harakati za madokta kuibadilisha wizara ya afya. Wiki hii kamati ya bunge imeituhumu wizara kwa kushindwa kusimamia matumizi ya kodi za wananchi kwa kujenga nyumba ya gharama kubwa ya waziri pale Dodoma na kutumia pesa nyingi ati kwenye maonyesho ya nanenane, na kwa kulimbikiza dawa za mabilioni hadi expire dates zake wakati wananchi hawna dawa.
Wakati huo huo kuna tetesi kuwa huduma katika hospitali ya Taifa mhimbili zimedolola sana kwa kiwango cha kushindwa kuoperate watoto wagonjwa jana ati kwasababu hakuna tube ndogo za kutumika kuwapa nusu kaputi.
Wakati huohuo serikali inajiandaa kutumia gharama kubwa kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Arusha town, gharama za kujitakia kwa hila tu za kuwalazimisha wanachi waendelee kutawaliwa na watu wasiowapenda.
Wakati huo huo miradi mingi ya maendeleo, (achilia mbali ahadi za JK na ccm yake kwenye kampeni za 2010), ikiwa zimesimama kwa ukosefu wa fedha.
Maudhi yapo mengi wajameni, tuamke wote wenye nia njema tulikomboe taifa letu !!!!
 
acha nilie iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
wananchi wa igunga wanaamini chadema ilishinda uchaguzi mdogo,isipokuwa ushindi ulitekwa kwa gharama kubwa.tunashukuru mungu haki aipotei kesi inayoendelea sasa ya kupinga uchaguzi huo hapo nzega utaleta haki tu,kama ilivyotokea kesi ya mkuu wa wilaya hii dhidi ya wapiganaji ya kusema amedhalilishwa kwa kumvua hijabu iliyomtupa chini mkuu huyo hivi karibuni.tuungane dhidi ya magamba
 
ile kesi ndio iliisha hivyo mkuu!
 
Siyo Igunga tu, but Tbr as a whole, ila usikonde, siku 1 2takuwa km Mwanza, mby, Arsh au Umbungo. Come 2015
 
Back
Top Bottom