Amina Chifupa

Apta Kayla

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
324
71
Ni miaka minne sasa tangu kifo kilipotutenganisha nawe tarehe 26.6.2007, tunashukuru kwa mchango wako juu ya madawa ya kulevya ulioutoa kule mjengoni. Ulitutoka siku ya kupiga vita matumizi mabaya ya dawa za kulevya, tulikulilia sana tukiongozwa na aliyekuwa Speaker wa Bunge letu Mzee 6.

Wakuu wa usalama wakatuambia walibahatika kufanya mahojiano nawe mara baada ya mchango wako ulioutoa Bungeni, wakatuambia uliwapa ile orodha ya Majina ya waagizaji wa madawa ya kulevya, wakatuambia wanaifanyia kazi ila mpaka leo hatujapata matokeo.

Pumzika kwa Amani Mpendwa.
 
washazaliwa wengine wapambanaje...hayo ndio maajabu ya Sir God!! RIP
 
Wapambanaji kama hawa huwa hawaishi maisha marefu i don know why!
Hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipoficha siri nzito ya uwezo wake juu yetu wanaadamu. Kama tungeijua siri ya kuzuia kifo, she would be here with us at a great cost, vijana kama huyu wangetusaidia sana kukemea uovu serikalini.
 
mala nyingi huwa ni hivyo,wapiganaji wa ukweli huwa hawadumu na wakidumu maisha yao huwa ni ya tabu sana

lala salama dada amina bado tunakukumbuka kwa ujasiri wako

lakini hata waliokutoa uhai hawawezi kudumu daima nao kifo kinawanyemelea tena watakufa mdomo ukiwa juu kama mbwa kichaa
 
siku ya leo "mpambanaji" "SITTO KABWE" ana majonzi kweli kweli...R.I.P AMINIA
 
siku ya leo "mpambanaji" "SITTO KABWE" ana majonzi kweli kweli...R.I.P AMINIA
Lazima, mpambanaji lazima amlilie mpambanaji mwenza. Halaf aliwahi kutuambia kabla hajafariki walikuwa wanaandaa kitabu abt Maisha ya Amina, akaahidi kusimamia utokaji wake, miaka 4 sasa, hatujaona matokeo.
 
AMINA CHIFUPA"MPAKANJIA"..REST IN PEACE.LEO UMETIMIZA MIAKA TAKRIBANI (3) TANGU UTUTOKE..Mpiganaji,mwanaharakati na Mwanasiasa kijana uliyelitumikia Taifa lako kwa moyo wa kizalendo,Mungu akupumzishe kwa Amani.
 
AMINA CHIFUPA"MPAKANJIA"..REST IN PEACE.LEO UMETIMIZA MIAKA TAKRIBANI (3) TANGU UTUTOKE..Mpiganaji,mwanaharakati na Mwanasiasa kijana uliyelitumikia Taifa lako kwa moyo wa kizalendo,Mungu akupumzishe kwa Amani.
 
Pole kwa kumkumbuka, japo mie sikuona chochote alichofanya kwenye siasa....Peleka kwenye celebrity forum mkuu.
 
Pole kwa kumkumbuka,japo mie sikuona chochote alichofanya kwenye siasa....Peleka kwenye celebrity forum mkuu.
mkuu tuko pamoja sana.... lazima tuandike historia bila kuweka usanii. hakuna kitu alichokifanya ... alikuwa msaniii mzuri
 
Alikuwa mwanasiasa na hili ni jukwa la siasa,So kama alifanya mabaya au mazuri ni kesi nyingine.Mm namuenzi kwa jukwa alilokuwa anasimama hadi umauti unamkuta.
 
Back
Top Bottom