AMIMI USIAMINI - Hii ndiyo fomu ya kuombea viza ya kuja Tanzania!

Vitu vinavyotakiwa kujazwa vinatosha na wala havina tofauti kubwa na vitu vinavyojazwa kwenye fomu za viza za nchi nyengine.

Cha muhimu nadhani ni kuangalia ili kuifanya iwe neat zaidi na iweze kuwa filled online, japo kama mtu atalazimika kwenda kuiwasilisha ubalozini kwa mkono
 
Binafsi sioni tatizo, aliyeona tatizo tunaomba mtueleze tatizo ni nini?
Naomba uprint halafu jaza sehemu zifuatazo:
-Title......
-Date and Place of Birth....
-Place of issue.......
-State Your Employer/University/College....
Kwa kweli hata wenzetu nadhani ndo chanzo cha kutudharau make unapojaza hii form inadhihilisha uhalisia wa nchi yenyewe kwa ambaye haijui!!
Ni aibu kwa idara husika kuendelea kutumia form hii!!!
 
we ****, ingekuwa vema kama ungetuwekea na visa application za nchi nyingine angalau mbili ili tuone tofauti. kwa sisi ambao hatujawahi kuziona fomu za nchi nyingine tunaweza kudhani hii ya tanzania ndo the best form ever
Kiongozi huo sasa utakuwa ni uvivu, mbona zipo online tu??google utaziona ukitaka kuziona.
 
Naomba uprint halafu jaza sehemu zifuatazo:
-Title......
-Date and Place of Birth....
-Place of issue.......
-State Your Employer/University/College....
Kwa kweli hata wenzetu nadhani ndo chanzo cha kutudharau make unapojaza hii form inadhihilisha uhalisia wa nchi yenyewe kwa ambaye haijui!!
Ni aibu kwa idara husika kuendelea kutumia form hii!!!

Mkuu, nimei-print na kujaza..Japo nina mwandiko mdogo lakini kuna maeneo nimeshindwa kujaza vizuri vipengele kwenye bold hapo juu kutokana na ufinyu wa nafasi ya kujaza.
Mtazamo wangu, fomu iko clear ila mpangilio kwenye kujaza mambo kadhaa ndiyo tatizo. Sidhani kama tunahitaji kuwa na page 3 au 4 ndiyo tuonekane tupo serious na hili suala. Ila marekebisho kidogo kuifanya fomu iwe na mpangilio mzuri yanahitajika.
Natumaini wahusika wanatusoma na kuchukua hatua.
 
Kiongozi huo sasa utakuwa ni uvivu, mbona zipo online tu??google utaziona ukitaka kuziona.

Mvivu mimi au mleta mada. Yeye mdo alitakiwa a google ili alete taarifa kamili. Utasemaje kitu fulani kibaya bila kulinganisha na kitu kingine.
 
Nafikiri mleta hoja alitakiwa aje na hoja ya kipi muhimu ambacho hakipo kwenye visa application form badala ya kusema ni page moja tu. Kama yeye anapenda au anafurahia kujaza page kumi anapokwenda nchi za watu ajue vile vile kuna watu kibao huwa wanahoja umuhimu wa hizo page kibao zisizo na maana kwa applicants!!
 
mnashanga nini?,niliwai kusema hapa nchi ya wajinga wengi mkabisha.nenda kwenye tovuti ya tanesco pia na company policy ya tz,utalia
 
Sioni tatizo zaidi ya email na website waliotumia.

Form ni nzuri, simple, haina complications.

Kwani mlitakaje?
 
Kuna nani aliyesoma/tembea nchi nyingine huko Immigration? Wote wapo wapo tu. Wakitoka nje ya nchi, hubebwa kama maboga kwa shughuli za kiserikali tu. Hawajawahi safiri kwa nguvu yao wenyewe!!!
 
Nmeisoma hiyo form nimekumbuka na hotuba moja ya mwalimu alipata kunena hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa fikra,enzi za mwalimu kiongozi alikuwa ni tajiri wa fikra masikini wa mali lakini sahzi ni tajiri wa mali lakini masikini wa fikra, we unafikiri kwa mtindo huu fursa za ajira zitatoka wap?
 
Hiyo ni form ya visa tu, ni tofauti kabisa form ya kuomba residence permit. Mimi nilishaiona form ya kuomba permit ina maelezo mengi kuliko hayo. Hizo za visa hata Kenya, Uganda hata Burundi ni za kawaida sana, tena sehemu zingine unaja hata mpakani tu, ni kikadi kidogo zaidi ya hiyo form. Au unataka kuwe na form tofauti kwa ajili ya wachina tu?. Huo utakuwa ni ubaguzi kwa wachina
Hivi kinacho jadiliwa hapa umekielewa au umekurupuka?
 
Mvivu mimi au mleta mada. Yeye mdo alitakiwa a google ili alete taarifa kamili. Utasemaje kitu fulani kibaya bila kulinganisha na kitu kingine.
Hakuna sababu ya kujaza sever hapa kwaajili ya umaamuma, wewe tafiti kujua ukitaka kwenda uk, usa, canada, australia, japan, nk ni nini unaulizwa kwenye visa form zao..
 
Binafsi sioni tatizo kwani cha msingi ni pale mtu akitaka residence permit, hapo lazima maelezo ya ziada yatolewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom