Amfumania mke wake 'live' fundisho.

Dreamliner

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
2,035
213
WEWE ungefanyaje/.. REAL story...

Baada ya kufunga ndoa takribani miezi 6 hivi, jamaa yangu wa karibu alihisi kusalitiwa kwa ndoa yake. Akafanya mtego na siku hiyo kama kawaida aliaga anakwenda kwenye biashara zake mkoani.

Mke akamjulisha X B/F wake kama kawaida yao. Ilipofika saa 2 usiku, Mume akarudi ghafla na kufungua mlango na kukaa sitting room akihofia kwenda b/room ambako kulikuwa na shughuli inaendelea. Mume mwizi akamwambia yule mwanamke. Nimesikia kama mtu ameingia sebuleni. Mwanamke kwa sababu ana uhakika hakuna mtu wa kuingia kwake kwani mume alishasafiri, akatoka kama alivyozaliwa na kumkuta mume wake amejaa sitting room.

Mume akamwomba msamaha mke wake kwa kumtibulia starehe yake na kuingia chumbani ambako vilevile alimwomba msamaha mgoni wake. Na kumwambia.. ''Siku nyingine uwe unakwenda G/house sio kuja nyumbani kwangu.. Utauawa bure''. yule mwizi aliachia mkojo kitandani akijua ndio mwisho wake. Na mke alikuwa anasubiri kuona kitakachotokea baada ya mume wake kuingia b/room. Yule bwana akaingia bafuni kuoga, huku nyuma, mwizi akaingia mitini.

Mume hakumuuliza tena mke wake wala kumpiga na hakumweleza mtu yeyote yale yaliyomkuta.. Maisha yakaendelea lakini, hakuna huduma yoyote, hakuna mazungumzo, hakuna salamu wala hakuna mawasiliano yoyote na mke wake. Baada ya miezi 3, mume akaja na mwanamke mwingine na kulala nae nyumbani kwake huku mke wake anaona. Asubuhi, mke aliondoka bila kuaga na kurudi kwao. Huko alipoulizwa, akasema amefukuzwa.. Akiulizwa sababu, hana cha maana cha kueleza. Wazazi walimtafuta mume wake na alikwenda na kueleza kila kitu na kumwacha mke moja kwa moja..

Hiki ni kisa cha kweli kilichomtokea rafiki yangu wa karibu kama miezi 6 iliyopita... JE UNGEKUWA WEWE., UNGEFANYAJE?
 
Ningewauliza kama walikuwa wanatumia condom, pili ningejiangalia na mimi kama sina hio infedality xcter, tatu ningepima kama kiafya niko salama, nne ningekuwa jela kwa kosa la kuhamisha kiungo au viungo vya mwanadamu kutoka kwenye original place yake
 
Namuuomba Mungu bila kukoma mke wangu awe mwaminifu siku zote kwa maana sitaki kesi ya mauaji
 
Duuh hii ngumu sana eeeh huyo mwanamke alikuwa hatari hakuwa na mapenzi na mmewe hata kidogo..maskini ndoa changa alishaanza Usaliti wa hali ya juu.... miezi sita tu ndani ya ndoa anazua mabalaa...
 
Duuh hii ngumu sana eeeh huyo mwanamke alikuwa hatari hakuwa na mapenzi na mmewe hata kidogo..maskini ndoa changa alishaanza Usaliti wa hali ya juu.... miezi sita tu ndani ya ndoa anazua mabalaa...
=========

Dawa ya moto ni moto. Ningemwambia yule mme ageuke na yeye apate raha yake.
 
Unasemehe,afu unachunguza tatizo gani limemfanya mkeo a-acheat(inawezekana mwanaume ndio source labda alikuwa anakwepa majukumu)
 
Duuh hii ngumu sana eeeh huyo mwanamke alikuwa hatari hakuwa na mapenzi na mmewe hata kidogo..maskini ndoa changa alishaanza Usaliti wa hali ya juu.... miezi sita tu ndani ya ndoa anazua mabalaa...

Acha tu FL1.. Inawezekana alikuwa anafanya kabla ya ndoa..
 
Duh huyu mwanaume ana roho anayoijua yeye mwenyewe IN SUCH KIND OF SITUATION YOU WILL NEVER KNOW HOW YOU WILL REACT UNTIL IT HAPPENS TO YOU.
 
ni ngumu sana ZD labda uwe na maono ya kimungu zaidi
Unajua FL1,hii ni ngumu kama wanawake ndio wamefumaniwa.Mbona wanaume huwa wanasamehewa mara nyingi na maisha yanaendelea????.
Mnakumbuka tu viapo vya kanisani afu unafumba macho
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom