Amenitongoza!

John na Sauda wamekuwa marafiki machoni kwa wanajamii kwa muda mrefu. Lakini hivi karibuni wamekuwa na ugomvi usiyo na maelezo. John alikuwa akishirikiana na Sauda kwenye biashara zao na hata tuliowengi tuliamini kuwa huenda ni wapenzi. Kama Mchungaji, John amekuja nishirikisha sababu ya ugomvi wao! Katika kuchakachua nini kilichotokea John anadai alimkopesha dada Sauda Sh 500,000 aongezee kwenye biashara yake, lakini kila akimkumbushia amrudishie imekuwa shida na anaambulia matusi. Na imefikia hata hawawezi kuongea tena. Kwa muda wangu nilimtafuta chemba Sauda kumuuliza kulikoni ugomvi na John, Sauda alinijibu huyo kaka amekuwa kama ndugu yangu, amenishangaza hivi karibuni amenitongoza kitendo hicho kimenikera sana sitaki hata kumsikia. Nikamuuliza hivi ni kweli alikukopesha pesa fulani? Sauda alibadilika rangi Rev Masanilo nakuheshimu mimi nitaifa kubwa kwa siku natumia 100,000 kwa vocha iweje nimkope huyo Shs 500,000/=? Mwambie anikome na asinifuate fuate mimi si wa hadhi yake. Wachungaji tuna viswali vyetu, baada ya kumbana sana alikuabali ni kweli alimkopa John na atafanya juhudi amlipe! Ameamua kumwaga radhi na kusingizia jamaa amemtaka kimapenzi ili kuuwa soooo!

NB Kina dada kwanini mnasingizia kutongozwa hata pasipostahili?

Rev Masa K

Kakosa busara huyo mdada... moyo wa mtu kiza kinene..
 
Hahahahahahah hivi ukimkopesha mdada na akawa hataki kukulipa cash utakubali yale malipo mengine?

Kama ni muumini wa hiyo kitu na biashara yenyewe ni poa/inalipa basi ruksa! Ila kuna wakati mikopo mingine inakaa kimtego mtego na mtu akiamua kuuvaa mkenge basi, na aubebe msalaba wote! Hata hivyo huwa kuna baraka kubwa tu kwa wale wanaoweza kusamehe. Mimi ningesamehe dada aende na hiyo lakini 500 ili nikwepe kugongwa mhuri wake. Nafasi zenyewe zilishajaa. Walau ni nisiharibu thamani ya ngozi kwa kuanza kuchakachua seheme nyingine za mwili.

Offt-topic: Huo wokovu umeuanza lini? Naona umepiga U-turn, kuanzia jina hadi trade marker! Au biashara ya zamani imechina?
 
Siku za mwisho hizi ndugu yangu! Aliyesimama aangalie asianguke
 
Ukimkopesha mdada ujue umempa na wala usitegemee kurudishiwa isipokuwa kwa wadada wachache sana. Wanapokuomba wanalialia sana, wakipata huanza sababu, iliyo kuu ni kutakwa au kutongozwa, utadhani ni ajabu. Wanasahau kwamba wanajidhalilisha wenyewe. Shame on women of the type!
 
Senkyu Sa....
Sasa mbona wanajifanya kuchukia wanapotongozwa???:confused2:

Zuga tu.. akikaa wiki hajapigiwa chapuo hata la salamu... bajet ya saluni na muda wa kukaa ktkt vioo vinaongezwa maradufu!!:smile-big:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom