Amenitongoza!

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
John na Sauda wamekuwa marafiki machoni kwa wanajamii kwa muda mrefu. Lakini hivi karibuni wamekuwa na ugomvi usiyo na maelezo. John alikuwa akishirikiana na Sauda kwenye biashara zao na hata tuliowengi tuliamini kuwa huenda ni wapenzi. Kama Mchungaji, John amekuja nishirikisha sababu ya ugomvi wao! Katika kuchakachua nini kilichotokea John anadai alimkopesha dada Sauda Sh 500,000 aongezee kwenye biashara yake, lakini kila akimkumbushia amrudishie imekuwa shida na anaambulia matusi. Na imefikia hata hawawezi kuongea tena. Kwa muda wangu nilimtafuta chemba Sauda kumuuliza kulikoni ugomvi na John, Sauda alinijibu huyo kaka amekuwa kama ndugu yangu, amenishangaza hivi karibuni amenitongoza kitendo hicho kimenikera sana sitaki hata kumsikia. Nikamuuliza hivi ni kweli alikukopesha pesa fulani? Sauda alibadilika rangi Rev Masanilo nakuheshimu mimi nitaifa kubwa kwa siku natumia 100,000 kwa vocha iweje nimkope huyo Shs 500,000/=? Mwambie anikome na asinifuate fuate mimi si wa hadhi yake. Wachungaji tuna viswali vyetu, baada ya kumbana sana alikuabali ni kweli alimkopa John na atafanya juhudi amlipe! Ameamua kumwaga radhi na kusingizia jamaa amemtaka kimapenzi ili kuuwa soooo!

NB Kina dada kwanini mnasingizia kutongozwa hata pasipostahili?

Rev Masa K
 
Rev. Masa wewe uu mchungaji mwema....yaan umetumia muda mwingi kum-interrogate Sauda ilhali kwa John ulitumia sekunde chache?
BTW: Hivi kutongozwa ni kukosewa heshima???
 
Kwani hujui kuwa hayo mambo hayana ushahidi? Usingekuwa mchungaji ngoma ilikuwa imetoka hiyo. Ungepataje ukweli kwamba kweli huyo dada alikopa pesa ya watu na hiyo ndo gia anayotumia kuruka viunzi?

Ni heri mambo ya unyumba na ngono yabaki siri. Kama kila unapopitia ungechapwa mhuri usoni, basi wengine ngozi ingeshakuwa kama chatu kwani siyo uso tena bali hata kwenye unyayo nafasi isingetosha!!

DC
 
Rev. Masa wewe uu mchungaji mwema....yaan umetumia muda mwingi kum-interrogate Sauda ilhali kwa John ulitumia sekunde chache?
BTW: Hivi kutongozwa no kukosewa heshima???

Kijana unajua hata sisi wachungaji tunafeelings! Kwanza alivyokuwa amevaa dada Sauda ni mtego kweli kweli.........wadada wanapenda sana kusingizia wametongozwa ili wapate sympathy!
 
Kwani hujui kuwa hayo mambo hayana ushahidi? Usingekuwa mchungaji ngoma ilikuwa imetoka hiyo. Ungepataje ukweli kwamba kweli huyo dada alikopa pesa ya watu na hiyo ndo gia anayotumia kuruka viunzi?

Ni heri mambo ya unyumba na ngono yabaki siri. Kama kila unapopitia ungechapwa mhuri usoni, basi wengine ngozi ingeshakuwa kama chatu kwani siyo uso tena bali hata kwenye unyayo nafasi isingetosha!!

DC

Hahahahahahah hivi ukimkopesha mdada na akawa hataki kukulipa cash utakubali yale malipo mengine?
 
Rev. Masanilo naona sasa unakiuka kiapo ulicholishwa cha kuficha siri za waumini wako unakuja kuzianika hapa JF nakuonya dhambi unayofanya ni kubwa sana na utaishia pabaya (motoni)
 
Ndio maana mimi siwashirikishi wanawake mbali na mke wangu kwenye mambo ya pesa au business yoyote. Mfano ofisini kwenu wewe ni meneja wake nae hajiwezi kikazi uwe mwangalifu sana - atakuzushia tu! Kwanza ukute yeye ndio alitaka kulipa hiyo pesa kwa kutaka John apite hapo chini ya arch yake! In kind!
 
Kijana unajua hata sisi wachungaji tunafeelings! Kwanza alivyokuwa amevaa dada Sauda ni mtego kweli kweli.........wadada wanapenda sana kusingizia wametongozwa ili wapate sympathy!

Ungemwita mjengo kisha ukomee pepo alafu unamega kwa maana anakuwa tayari umesha mtakatifuza.
 
Rev. Masanilo naona sasa unakiuka kiapo ulicholishwa cha kuficha siri za waumini wako unakuja kuzianika hapa JF nakuonya dhambi unayofanya ni kubwa sana na utaishia pabaya (motoni)

Ni muda gani hiki kiapo kinaapwa? Kwa RC padri hatakiwi kusema dhambi alizotubu muumini - kumtaja jina na dhambi hizo. Lakini huyu mchungaji anaongelea shauri lililopelekwa kwake na sio siri na ana-share na sisi ili tupate somo!!!!!!!! Huyu mchungaji ni mpatanishi na mkweli!! Heri wapatanishi kwani ufalme wa mbingu ni wao!
 
Ungemwita mjengo kisha ukomee pepo alafu unamega kwa maana anakuwa tayari umesha mtakatifuza.

Masuluhisho haya mama mchungaji huwa anashirikishwa mpwa! Ila nilichukua namba yake....!
 
Ni muda gani hiki kiapo kinaapwa? Kwa RC padri hatakiwi kusema dhambi alizotubu muumini - kumtaja jina na dhambi hizo. Lakini huyu mchungaji anaongelea shauri lililopelekwa kwake na sio siri na ana-share na sisi ili tupate somo!!!!!!!! Huyu mchungaji ni mpatanishi na mkweli!! Heri wapatanishi kwani ufalme wa mbingu ni wao!

Umebarikiwa sana wewe na uzao wako!
 
Hawajafikiria hata siku moja kuwa akisingizia ametongozwa imemaliza issue .Kumbe anaonekana limbukeni na mwongo. Kutongozwa ndio sifa ya demu. Otheriwise she is a man.
 
Rev. Masa wewe uu mchungaji mwema....yaan umetumia muda mwingi kum-interrogate Sauda ilhali kwa John ulitumia sekunde chache?
BTW: Hivi kutongozwa ni kukosewa heshima???
ni compliment... anaetongozwa ajue kwa kiasi flani anaa...TBS!!:A S 8:
 
Back
Top Bottom