Amenipa zawadi ya kipigo cha mbwa koko baada ya kumfumania akirojoka!!

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Jamani kweli hii ni njia panda kwangu, nilimfuma boyfriend wangu akiwa na mrembo mwingine, kwa upendo wangu nilimfuata na kumuuliza je hapa ndiyo safari uliyoniaga ya kuwa utakuwa mkoani for some weeks? Basi badala ya kuanza kunielezea kwanini amenidanganya kuwa yupo safari angali namuona na binti mwingine kwa bar!alianza kunipiga na kuniona kama mimi ni mgomvi kwa kumuuliza kwanini unanidanganya na kuwa na wanawake wengine? Je hii ni sahihi kwa alichokifanya kwangu? Naombeni ushauri wenu nami nitaufanyia kazi

Chanzo: Gonga hapa!
 
Jamani kweli hii ni njia panda kwangu, nilimfuma boyfriend wangu akiwa na mrembo mwingine, kwa upendo wangu nilimfata na mkuulza je hapa ndiyo safari uliyoniaga ya kuwa utakuwa mkoani for some weeks?basi badala ya kuanza kunielezea kwanini amenidanganya kuwa yupo safari angali namuona na binti mwingine kwa bar!alianza kunipiga na kuniona kama mimi ni mgomvi kwa kumuuliza kwanini unanidanganya na kuwa na wanawake wengine? Je hii ni sahihi kwa alichokifanya kwangu? Naombeni ushauri wenu nami nitaufanyia kazi

Chanzo: Ladies Chat Blogspot

umeshawahi kusikia ule wimbo wa ngwasuma ukisema kuwa kwani kila mwanamke anaeingia bar anajiuza au ni malaya!we ulijuaje kuwa yule ni demu wake?
 
Kipigo halali yako. Hiyo tabia si nzuri. Siku nyingine usifanye hivyo!
 
Huyo hakufai alitakiwa akueleze ni kwanini yupo pale badala ya safari sio kukimbilia kipigo tena ingekuwa mie ningemshtaki polisi kwani siku hizi wanawakwe hawapigwi kuna ujumbe ulitolewa na TAMWA -"PIGA NGOMA USIMPIGE MWANAMKE". hinyo nenda kamshtaki ili iwe fundishwo na kwa wengine.
 
we nawe unauliza nin sasa?
hakupend uyo wewe sepa au unampenda sana?
achana nae ebu sepa
 
Jamani kweli hii ni njia panda kwangu, nilimfuma boyfriend wangu akiwa na mrembo mwingine, kwa upendo wangu nilimfuata na kumuuliza je hapa ndiyo safari uliyoniaga ya kuwa utakuwa mkoani for some weeks? Basi badala ya kuanza kunielezea kwanini amenidanganya kuwa yupo safari angali namuona na binti mwingine kwa bar!alianza kunipiga na kuniona kama mimi ni mgomvi kwa kumuuliza kwanini unanidanganya na kuwa na wanawake wengine? Je hii ni sahihi kwa alichokifanya kwangu? Naombeni ushauri wenu nami nitaufanyia kazi

Dada yangu waswahili husema msema pweke hushinda maana hapa umeongea peke yako ingekuwa vizuri kama na huyo mtuhumiwa naye tungemsikia, hapa inakuwa ni vigumu kwa mtu kutoa ushauri kwa kuwa mtu mwenyewe ulimkuta bar inawezekana labda na yeye alikuwa ndio anasubiria muda ufike au labda huyo aliyekuwa naye ni mfanyabiashara mwenzake na wewe inawezekana ulimfikia bila heshima wakati yeye wala hakuwa na nia mbaya ndio yote hayo yakatokea.Ni bora mkatafuta mtu aliye na umri mkubwa zaidi yenu na kila mtu kati yenu aeleze ukweli wa tukio lenyewe na uamuzi ufikiwe.Ni bora kutazama pande zote kabla ya kulaumu na kushutumu.Siku zote ukweli humuweka binadamu huru na ukisema ukweli usikimbie bali simama na utetee kile kilicho cha kweli.
 
Just kick him out,, if you can handle that shamefull issue the you can't keep live with him...

Please don't get me wrong but there is no love and the risk of getting desease is bigger, so why killing your self...

Love is about trust, respect, fear God and comitiment.. those are missing in your love life then go out and make your own life.
 
uache kumchunguza mkeo, kaa nyumbali, ulikuwa unatafuta nini huko, ndo hasara za kuchunguza chunguza badala ya ktulia, utajuta sasa umeona na umepata stahili yako..
 
uache kumchunguza mkeo, kaa nyumbali, ulikuwa unatafuta nini huko, ndo hasara za kuchunguza chunguza badala ya ktulia, utajuta sasa umeona na umepata stahili yako..

Wakati mwingine siyo lazima uchangie mada ikiwa huna cha kumsaidi mhusika...

Pole sana dada kwa yaliyo kukuta, hii inaonesha wazi kuwa huyo mtu wako haukupendi hata chembe. Amekupiga akidhani ndo njia yake ya kujihami.

Mwanume anayekupenda hawezi kukupiga hata siku moja. Hicho kiburi alikipata wapi wakai hata hajakuoa?

Mpita njia tu huyo hawezi kukufaa kwa maisha yako ya baadaye.
 
Back
Top Bottom