Amegundua vidonge vya ARV's chumbani kwa mpenzi wake

Dah............! Pole zake; mwambie akapime haraka na kwa kuwa keshajua ake na mpenziwe kwani ni dhahiri kutaonekana tofauti na kuondoa machungu zaidi wakae na mpenziwe waongee
 
kama hawezi kumuuliza mpenzi wake aende tu akapime mwenyewe kujua status yake. then akae na mpenziwe wavunje ukimya!!! amwambie wakapime binti akigoma abebe virago
 
Dah polen sana Waboyzia wenzangu....muhimu mkuu ni kuwa beneti na mshikaji katika hiki kipindi kigumu..Mshauri aende akapime na kupima kunaambatana na mambo mengi/ ushauri nasaha na awe tayari kukubaliana na matokeo ili afungue chapter mpya katika maisha yake. Nwdays ukijikeep fresh Maisha yanasonga tena kwa miaka mingi...
 
Hakuna cha alikuwa anasubili muda muafaka ili amwambie jamaa wakati walikuwa wanaendelea kungonoka ngono zembe. Mimi narudia tena hata kama hakuupata kwa njia ya zinaa bado dada ni muuaji. Kama angekuwa anampenda kijana angemlinda na the only way to do so ilikuwa kumwambia ukweli. Mpaka kufikia kutumia ARV ina maana ugonjwa anao siku nyingi maana hizo ARV huanza kutumiwa katika late stage pale CD 4 zinaposhuka. Kama aliona shida kusema ukweli basi at least angevunja uhusiano na jamaa. Ana roho mbaya huyo dada. Angekuta mwanume mwenye roho nyepesi mbona angemuua.
 
Dah polen sana Waboyzia wenzangu....muhimu mkuu ni kuwa beneti na mshikaji katika hiki kipindi kigumu..Mshauri aende akapime na kupima kunaambatana na mambo mengi/ ushauri nasaha na awe tayari kukubaliana na matokeo ili afungue chapter mpya katika maisha yake. Nwdays ukijikeep fresh Maisha yanasonga tena kwa miaka mingi...
Asante sana home-boy...tunaendelea na kujitutumua!ila jamaa ndo full ma-stress! Vp wa kulekule Berlin nin?kitu cha Warsaw hukuwekeza?
 
Mwambie jamaa akapime yeye kwanza. Kama yuko fresh, amshawishi huyo binti ili wakapime wote. Kama atakataa, hapo ndipo aachane naye completely. Inawezekana huyo binti akawa muathirika, lakini jamaa akawa fresh, regardless ni mara ngapi wame-do.
 
mwambie rafiki aende akapime, sio lazma aongozane na mpenziwe. Kama mungu kamnusuru na maambukizi mapya amwache upesi huyo dada cz ni muuaji.
 
kwakweli ni fundisho la gharama; makosa wanayo wote, mdada kwa kutokuwa wazi, pia na mkaka kwa kumuamini mtu bila kupima! Amefanya hivyo kwa wangapi? Huenda naye alishaathirika kitambo, angecheck afya b4 starting new relationship na asingefanya ngono nzembe bila wote kupima! Ukizingatia wenye mamlaka ya mwisho kwenye kujikinga ni wanaume!

Akapime, akikuta ameathirika waoane tu na mpenzi wake! Assume asingekuwa anatumia dawa angejuaje? Kaamua kuingia kichwa kichwa, waishi tu lawama hazisaidii!
 
Hakuna shaka kimwana yumo ndani ya Grid ya Taifa. Nashauri huyu Rafiki yako aende akapime, kama yumo ndani ya 'Grid ya Taifa ya Umeme' basi awe wa kwanza kumweleza mpenzi wake naye atatoa yaliyo moyoni mwake. Kwa kuwa wanapendana sio vyema kuruhusu VVU viwatenganishe. Wafuate ushauri wa wataalam na maisha yataendelea kuwa mazuri hadi hapo kifo kitakapowatenganisha.
 
ND; Nashukuru sana kwa hii mada, Jamani wana-JF hii ni somo pia kwetu sisi tulikwisha athirika na ambao bado hatujaathirika na hili janga, maana sawa siku hizindio hivyo unakuwa na mtu unamwita mpenzi na unakula peku bila hata kupima ndio kawaida yetu na ndio maisha yetu ya kila siku tunapima kwa machona iwe somo kwetu na mungu atusaidie hili somo liingie kichwani mwetu maana waliokwisha kuambukizwa hatuna jinsi bali kuwapenda na kuwalinda wapate maisha marefu lakini pia tunawajibu mkubwa sana wakuwalinda ambao hawajaambukizwa.

Fanya kuwa karibu na rafikio, husijionyeshe kama vile wewe ni watofauti sana mwonyeshe kuwa hata wewe unaweza kuambukizwa na kuwa haikuwa jinsi maana ni sehemu ya maisha yetu, pia mueleze kuwa kuwa naye yaweza kumpa maambukizi au yasimpe kwa hiyo kupima na kujuwa uhalisia ni muhimu, baada ya hapo ndio ataamua cha kufanya kutoka na jibu, sina huhakika labda wana-JF wengine kama wanajuwa iwapo unaweza kuwa naye na husiambukizwe!

Hii kesi sasa ni ya nne naisikia kuna jamaa pia alikuwa anaumwa tena siku nyingi sana akaenda kumchumbia dem mmoja na wakawa wachumba binti hakujuwa ukweli na watu walivyowanafki wapo waliojuwa lakini hawakumwambia binti wa watu, pia yupo dada mmoja nurse alikuwa na askali mmoja Dar, askali akafariki kwa huu ugonjwa dada akaanza dawa akawa mzima akaamia Tanga kufika Tanga kapata mchumba wakaowa dada kaficha lakini jamaa akawa analalamika kuwa mke hataki kushika mimba kabisa kila siku anasema wasubiri kwanza, mwisho wa siku akakutana na kadi na dawa hizo kwenye pochi, nakwambia jamaa alikuwa mzima na afya njema kabisa lakini alikufa ndani ya mwezi mmoja!
 
.........ni vema wapenzi kabla hamjafikia stage ya kuvuliana nguo kupima iwe ni priority ya kwanza, tena sio kupima mara moja ni zaidi ya mara 3.

Sasa basi kwa kuwa kapekenyua mkoba na kukuta hilo balaa, inabidi afanye maamuzi magumu ya kwenda kupima ukimwi ili ajue afya yake.
 
Hii situation ni 50|50. Ila binafsi naamini pana uwezekano mkubwa jamaa akawa hana HIV. Na kama angekuwa ameanzisha mahusiano na huyo dada wakati ameshaanza kutumia dawa uwezekano wa kwamba kaambukizwa HIV ungekuwa mdogo zaidi kama mwanamke angekuwa ana responde vizuri kwa dawa. Maambukizi ya HIV pia yategemea viral load. Mtu mwenye virusi kibao katika militre moja ya damu ana uwezekano mkubwa sana wa kukuambukiza ukilinganisha na yule mwenye virusi vichache ambavyo yamkini vimepunguzwa uwingi na dawa.Tafiti zimeonesha kuwa risk ya kupata HIV kwa mwanaume kwa kila tendo la ndoa moja analofanya (nazungumzia insertive vaginal sex) na mwanamke mgonjwa wa VVU ni asilimia 0.03 hadi 0.09 (yaani ni sawa na kusema katika matendo 1000 ya ngono na mtu mwenye VVU, mwanaume ana uwezekano wa kupata maambikizi katika matendo 3 hadi 9. Haya hayaongelewi, maana watu watajiachia). Hivyo kati ya magonjwa, HIV ina uwezo mdogo wa infectivity ukilinganisha na magonjwa mengine. Kwa wanawake risk inaongezeka sana kuwa asilimia 0.1 hadi 0.3 kwa kila tendo la ndoa (receptive vaginal sex) (yaani kwa mwanamke afanyaye mapenzi na mwanaume mwathirika, katika kila matendo ya ngono 100, ndani ya matendo 1-3 anaweza akapata maambukizi ya VVU).Kuna discordant couples kibao ambao mmoja wa mwenzi utakuta ana HIV na mwingine hana (wanaume wasiokuwa na HIV wakiwa wengi zaidi katika aina hizi za couples). Kama itakuwa walikuwa wakifanya mapenzi yale yasiyo ya kukamiana mpaka jamaa akapata michubuko; kama walikuwa wanatumia condom mara kwa mara; kama jamaa hakuwa ana magonjwa ya zinaa kama gonorrhea na kama jamaa katahiriwa; basi uwezekano wa kuwa ana HIV utakuwa mdogo zaidi. Asijisumbue na huyo dada, aende akapime afya yake then waanzie hapo.
 
Ni mshikaji wa muda mrefu!Tulifahamiana Tabora School(Boys) miaka iyooo.Tulipendana sana sbb 2likuwa tukiishi room moja,hata baada ya kumaliza tuliendelea na Elimu ya juu tena kwa Mafanikio makubwa. Jamaa yangu ni mtalaam wa i minara ya simu ktk kampun flani ya simu apa Tz,ana mpenz wake ambaye jamaa yng ana nia kabsa ya kuoa..uyu dada(shemej yangu)ni mkaguzi(Auditor)..."wanapendana sana"...lakn kama wiki imepta Mwanamke alpata likzo,akamua toka kwao kuja kukaa kwa rafk yngu kwa mda..ktk kipindi iki jamaa yangu aligundua ktk mkoba wa mpenz wake kuna "kadi",maelekezo na namna ya ku2mia vdonge vya kurefusha maisha,msichana hakuwah kumwambia jamaa wala ata sisi atukuwah kujua...japo kuna wakat walikuwa wanataka kwenda kupma ila mwnmke akawa relactant...jamaa anashndwa atamuanzaje mwanamke kumuliza mana alpekua tu mkobani bila ruhusa. Sabab mi n rakfye kanishrksha,jamaa kachanganyikiwa mpaka baadh ya kazi za kwenda kurekebsha minara watu wapate netwek kaziweka pending...yaan kachzka!TUNAFANYAJE?Mana mjini kushakuwa kuchungu..huzun yake n huzuni yangu! NAWASILISHA:
Nendeni mkapime tu. Poleni sana na Mungu atawasaidia
 
Hii situation ni 50|50. Ila binafsi naamini pana uwezekano mkubwa jamaa akawa hana HIV. Na kama angekuwa ameanzisha mahusiano na huyo dada wakati ameshaanza kutumia dawa uwezekano wa kwamba kaambukizwa HIV ungekuwa mdogo zaidi kama mwanamke angekuwa ana responde vizuri kwa dawa. Maambukizi ya HIV pia yategemea viral load. Mtu mwenye virusi kibao katika militre moja ya damu ana uwezekano mkubwa sana wa kukuambukiza ukilinganisha na yule mwenye virusi vichache ambavyo yamkini vimepunguzwa uwingi na dawa.Tafiti zimeonesha kuwa risk ya kupata HIV kwa mwanaume kwa kila tendo la ndoa moja analofanya (nazungumzia insertive vaginal sex) na mwanamke mgonjwa wa VVU ni asilimia 0.03 hadi 0.09 (yaani ni sawa na kusema katika matendo 1000 ya ngono na mtu mwenye VVU, mwanaume ana uwezekano wa kupata maambikizi katika matendo 3 hadi 9. Haya hayaongelewi, maana watu watajiachia). Hivyo kati ya magonjwa, HIV ina uwezo mdogo wa infectivity ukilinganisha na magonjwa mengine. Kwa wanawake risk inaongezeka sana kuwa asilimia 0.1 hadi 0.3 kwa kila tendo la ndoa (receptive vaginal sex) (yaani kwa mwanamke afanyaye mapenzi na mwanamke, katika kila matendo ya ngono 100, ndani ya matendo 1-3 anaweza akapata maambukizi ya VVU).Kuna discordant couples kibao ambao mmoja wa mwenzi utakuta ana HIV na mwingine hana (wanaume wasiokuwa na HIV wakiwa wengi zaidi katika aina hizi za couples). Kama itakuwa walikuwa wakifanya mapenzi yale yasiyo ya kukamiana mpaka jamaa akapata michubuko; kama walikuwa wanatumia condom mara kwa mara; kama jamaa hakuwa ana magonjwa ya zinaa kama gonorrhea na kama jamaa katahiriwa; basi uwezekano wa kuwa ana HIV utakuwa mdogo zaidi. Asijisumbue na huyo dada, aende akapime afya yake then waanzie hapo.
Ozziri:Umenifariji sana..umenitia Moyo!nimejfunza na umenipa darasa zuri sana!God Bless You!
 
ND; Nashukuru sana kwa hii mada, Jamani wana-JF hii ni somo pia kwetu sisi tulikwisha athirika na ambao bado hatujaathirika na hili janga, maana sawa siku hizindio hivyo unakuwa na mtu unamwita mpenzi na unakula peku bila hata kupima ndio kawaida yetu na ndio maisha yetu ya kila siku tunapima kwa machona iwe somo kwetu na mungu atusaidie hili somo liingie kichwani mwetu maana waliokwisha kuambukizwa hatuna jinsi bali kuwapenda na kuwalinda wapate maisha marefu lakini pia tunawajibu mkubwa sana wakuwalinda ambao hawajaambukizwa.Fanya kuwa karibu na rafikio, husijionyeshe kama vile wewe ni watofauti sana mwonyeshe kuwa hata wewe unaweza kuambukizwa na kuwa haikuwa jinsi maana ni sehemu ya maisha yetu, pia mueleze kuwa kuwa naye yaweza kumpa maambukizi au yasimpe kwa hiyo kupima na kujuwa uhalisia ni muhimu, baada ya hapo ndio ataamua cha kufanya kutoka na jibu, sina huhakika labda wana-JF wengine kama wanajuwa iwapo unaweza kuwa naye na husiambukizwe!Hii kesi sasa ni ya nne naisikia kuna jamaa pia alikuwa anaumwa tena siku nyingi sana akaenda kumchumbia dem mmoja na wakawa wachumba binti hakujuwa ukweli na watu walivyowanafki wapo waliojuwa lakini hawakumwambia binti wa watu, pia yupo dada mmoja nurse alikuwa na askali mmoja Dar, askali akafariki kwa huu ugonjwa dada akaanza dawa akawa mzima akaamia Tanga kufika Tanga kapata mchumba wakaowa dada kaficha lakini jamaa akawa analalamika kuwa mke hataki kushika mimba kabisa kila siku anasema wasubiri kwanza, mwisho wa siku akakutana na kadi na dawa hizo kwenye pochi, nakwambia jamaa alikuwa mzima na afya njema kabisa lakini alikufa ndani ya mwezi mmoja!
Very Constructive Advice....I appriciate and take it into account
 
Hakuna shaka kimwana yumo ndani ya Grid ya Taifa. Nashauri huyu Rafiki yako aende akapime, kama yumo ndani ya 'Grid ya Taifa ya Umeme' basi awe wa kwanza kumweleza mpenzi wake naye atatoa yaliyo moyoni mwake. Kwa kuwa wanapendana sio vyema kuruhusu VVU viwatenganishe. Wafuate ushauri wa wataalam na maisha yataendelea kuwa mazuri hadi hapo kifo kitakapowatenganisha.
Thanx kwa ushauri!mhmh "Grid ya Taifa?"....ni kama neno gumu lenye vimelea vya unyanyapaa!Usipende kulitumia
 
Pole zake kwa kweli! Naona wengi wamtoa ushauri mzuri sana, naamini utamsaidia rafiki yako! lets hope rafiki yako bado hajaupata! Lakini hata kama ameupata, sio mwisho wa maisha! He needs to be strong!
 
Back
Top Bottom