Amchinja Mkewe Kwa Kunyimwa Unyumba Kwa Miaka 21

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Mwanaume mmoja wa nchini Ufaransa amemchinja mkewe kwa kutumia kisu kidogo cha jikoni baada ya kukasirishwa na mkewe ambaye aliamua kuitunza bikira yake na kukataa kumpa unyumba kwa miaka 21 ya ndoa yao kwasababu ya alikuwa hataki kupata watoto.Philippe Cousin mwenye umri wa miaka 53 alimchinja mkewe wa ndoa ya miaka 21 Nicole Cousin mwenye umri wa miaka 47 baada ya Nicole kuendelea kukataa kufanya naye mapenzi kwa kuhofia kupata watoto.

Nicole alikutwa amefariki kwenye nyumba yao katika mji wa Calais kaskazini mwa Ufaransa.

Philippe aliwaambia polisi kuwa mkewe alikataa kufanya naye mapenzi kwa kipindi chote cha ndoa yao akisema kuwa anahofia watoto watakaozaliwa watarithi ugonjwa sugu wa multiple sclerosis (ugonjwa unaosababisha madhara kwenye ubongo na uti wa mgongo) ambao umekua ukimsumbua baba yake Nicole.

Uchunguzi wa maiti ya Nicole ulithibitisha kuwa hadi wakati anafariki Nicole alikuwa kweli ni bikira ingawa alikuwa kwenye ndoa kwa miaka 21.

Siku ya tukio hilo ugomvi ulizuka kati ya Philippe na mkewe ambapo Philippe alichukua kisu na kumwekea mkewe shingoni kabla ya kukikata na kukinyofoa kabisa kichwa chake.

Baada ya tukio hilo Philippe aliwapigia simu polisi na kuwaambia "Samahani kwa kuwasumbua, nimemuua mke wangu".

Phillippe alipandishwa kizimbani jana kwa mauaji hayo aliyoyafanya mwezi aprili mwaka juzi.

Wakili wa Philippe alisema kuwa Philippe alifanya mauaji hayo kutokana na kuchanganyikiwa kimawazo kwa kushindwa kuwa baba.

Philippe ambaye hivi sasa anapatiwa matibabu ya kisaikolojia ndani ya jela huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.
 
hayo ni madhara ya hamu ya ngono ya muda mrefu............. kujinyima ni vyema lakini iwe kwa kiasi................
 
kwa mtazamo wangu nadhani jamaawalikuwa wanaoendana sana maana wangekuwa hawaoendani na si waamninifu to each aza,mwanamke angetoka nje so bikira isingekuwepo n mwanamme angeweza hata kuzaa nje so asingekuwa na msongo kiivyo na stress zingepungua but zoz pple wea zea for each aza
 
Mhh!! 21 damn years...
Kweli jamaa alivumilia na masikini huyu mama!! yaani alijali sana watoto ambao angewapata.
Hakuna kama mama!!
 
Mbonea mbona unapenda habari dizaini hii mara "mwanamke asababisha ajali kwa kunyoa sehemu ........." maajabu wewe sio bure
 
Mimi ningekaa kwenye ndoa miaka 21 hamu zingeniua mimi kwanza, nikikaa masaa 24 bila hiyo namna na vibrate kama simu ya nokia 2010,
 
Hiyo haikuwa ndoa. Ndoa gani ambayo tendo lenyewe la ndoa mnanyimana?
 
dah!,kweli dunia ina mambo, sasa huyu wife kama aliogopa magonjwa ya kurithi, why akubali ndoa?,kama vp angetumia kinga kuliko kumfanya msela padri..ril astonishment!!!!!!!!!
 
That's a very patient man! Lazima alimpenda sana mkewe or else asingemvumilia miaka yote hiyo. I'm trying to imagine angekuwa mwanamume wa kibongo ingekuwaje!
 
Hiyo haikuwa ndoa. Ndoa gani ambayo tendo lenyewe la ndoa mnanyimana?

mkuu, kama ingekuwa wananyimana, isingefika miaka 21 na wala wasingeuana! hapo ndipo penye shughuli kuelewa!!!!!!!!!!!!!!!!!

ni hivi, kama wangekuwa wananyimana wangekwisha gombana zamani sana nadhani hata miezi sita isingefika wakiwa pamoja!!!!!!!!!!!!!!!!!

inaonekana hawa walikubaliana lakini baada ya muda curiousity ilianza kutafuna akili za mume na ikapelekea mental disorder................ hatimaye murder!!!!!!!!!!!!!!!!

ni suala la kuagalia sana......... wakubwa zetu walikuwa better off kwani hawakuwa na abstinence zenye longer terms........... ndoa zilifungwa na vijana sio izi watu wanaoana wakiwa kwenye 30s !!!!!!!!!! na ukizingatia kuwa walipevuka kwenye late teens!!!!!!!!!!! majaribu natupu!!!!!!!!!!
 
Masanilo angekuwepo hapa angetoa ushauri mbadala. Wapi Masanilo? njoo mkuu ulete wazo mbadala maana mambo ya kuuana eti kuogopa kuzaa! ah!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom