Amchana mwanae na viwembe mdomoni

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAMKE Salima [28] amejikuta akipelekwa kituo cha polisi na mume wake baada ya kumchana mwanae na kiwembe mdomoni.
Salima alipelekwa kituoni baada ya mumewe kukasirika na kitendo alichokifanya cha kumuadhibu mtoto kwa kumchana na viwembe

Salima alichukua umamuzi huo, baada ya mtoto wake huyo kumtukana tusi la nguoni na kushikwa na jazba na kumuadhibu kwa nia hiyo ili iwe fungisho kwa mtoto huyo asirudie kutamka tusi hilo

Alichukua uamuzi huo wa kumuadhibu mtoto huyo wa kumzaa mwenyewe kwa kukasirika na kutamka tusi ambalo hakutegemea kama angetamka mtoto wake huyo

Aliagiza kiwembe dukani na kuanza kumchana na kiwembe katika midomo yake hali iliyopeleka kuzua varangati kati ya wazazi hao wawili baada ya baba kushindwa uvumilivu kuona mwanae anaugulia kwa maumivu ya vidonda

HAta hivyo mume wa mwanamke huyo aliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na mwanamke huyo kutakiwa kufika kuituoni kwa mahojiano

Mtoto aliyejeruhiwa na mama yake huyo alitambulika kwa jina la Ramadhani [6.5]
 
Back
Top Bottom