ambazi lakimbia na pingu za polisi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MTU mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi wilayani Maswa, amewakimbia polisi waliokuwa wamemkamata kwa tuhuma za ujambazi huku akiwa na pingu mikononi.
Tukio hilo lilitokea juzi wakati kundi la watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wapatao watano walipovamia nyumbani kwa mfanyabiashara, Edward Charles, maarufu kwa jina la Mika.

Majambazi hayo yalivamia nyumbani kwa mfanyabiashara huyo yakiwa na bunduki moja pamoja na silaha nyingine za jadi na kufanikiwa kuiba simu 72 za mkononi na vocha za thamani ya sh 160,000.

Pia majambazi hayo mbali ya kupora vitu hivyo pia yalipora fedha taslimu sh 860,000 na kisha kutokomea nazo kusikojulikana.

Baada ya tukio hilo kutokea mfanyabiashara huyo alitoa taarifa kituo cha polisi wilayani hapa na jeshi hilo lilianza msako na kufanikiwa kumkamata mmoja akiwa eneo la sokoni.

Baaada ya kumkamata jambazi huyo na kumpekua walimkuta na vocha za simu pamoja na simu mbili na fedha taslimu sh 50,000.

Jambazi huyo baada ya kuhojiwa alieleza aliuziwa vitu hivyo na rafiki yake ambaye hakufahamika jina na kwamba anapatika eneo la njia panda.

Kutokana na maelezo hayo, askari hao walimtaka mtuhumiwa huyo kuwapeleka na walipofika eneo hilo waliwakuta watuhumiwa watatu wakinywa pombe akiwamo mwanamke mmoja.

Hata hivyo, baada ya majambazi kuwaona polisi walikimbilia porini; ndipo yule mtuhumiwa aliyekuwa na pingu alipompiga askari teke na kuanguka na kisha na naye kutokomea porini.

Polisi wilayani hapa bado wanaendelea kuwasaka majambazi hayo pamoja na aliyekimbia na pingu.
 
hata mimi nilikuwa nataka kuuliza ila ni typing error anaweza akarekebisha.
 
Majambazi ya miaka hii hayana mzaha. Linalala mbele na pingu baada ya kumpiga kininja polisi!! Kuna kazi kweli.
 
Majambazi ya miaka hii hayana mzaha. Linalala mbele na pingu baada ya kumpiga kininja polisi!! Kuna kazi kweli.

ninachowaza hapo atakayemfungua hizo pingu ni nani maana wananchi watagoma na kupeleka taarifa polisi!!!may be atumie mbinu za kikomandoo!
 
ninachowaza hapo atakayemfungua hizo pingu ni nani maana wananchi watagoma na kupeleka taarifa polisi!!!may be atumie mbinu za kikomandoo!
si hayo majamazi wenzake waliotokomea wote porini ndiyo yatakayomfungua!ila hii kali du majambazi yana mbinu zaidi ya polisi,kazi iko!
 
Back
Top Bottom