Amazing: Form iv leaver wawa ma-house girl

Mshaara wa house girl ambaye ana elimu kuanzia form four ni TShs 150,000/- na pia ana marupurupu ikiwa pamoja na sehemu ya kulala na chakula pia anakatwa NSSF, Hapo itakuwa imetulia na wala hakutakuwa na shida ya kuwapata


shida ni pale housegirl/houseboy anapolipwa mshahara kiduchu.

Hata hivyo ........... mtu hata kama kafika form VI wacha form IV - lakini kasoma kijijini sana (very remote) halafu likizo hajawahi kuja mjini - na mjini kwenyewe akaingia kwenye nyumba za watu wenye maisha ya kisasa - nina maana atakuwa hajui a) kutumia micro-wave au kujua hata ni nini
b) kutumia rice cooker
c) kutumia breadmaker
d) blender
e) water dispenser
f) washing machine
g) dish washer
h) kutumia pass ya umeme etc.

tutofausishe kati ya elimu ya darasani na elimu ya maisha - maisha ya level mbali mbali -

Hivyo tuchukulie kazi ya housegirl - ni mojawapo ya kujifunza aina fulani ya maisha - na kama ana akili - anaweza kutoka tu - kwani ufahamu unafunguka tunapopata changamoyo za maisha - kama yuko smart - kichwani
 
Ulitaka ukawaopoe pale sinza afrika sana loh
too late mabinti kaeni uko uko mungu ana makusudi ya nyie kuwepo huko ipo siku milango itafunguka na wanaoshangaa awataamini....ninavyoongea mke wa mawaziri wawili wa tanzania walikuwa ma hgirl na leo wanakohoa kwenye mashangingi ya kodi zetu ...msikate tamaa jiheshimun uko uko penden kazi zenumbaya msiachie kwa mabosi zenu mtaharibu kabisa
 
:spy: Tuna Hitaji Ma-house girl wasomi katika karne hii hakuna cha kushangaa hapo,unategemea form iv leaver afanye kazi gani? nafikiri wakati umefika iwe ni fani rasmi inayotambulika na watu wapate kozi na walipe vizuri.
 
Mimi pia ni mwalimu kama wewe, lakini sioni mantiki ya kutumia neno 'amazing'. Kuna ajabu gani mimi sielewi.

Mtu akimaliza kidato cha 4 anatakiwa afanye kazi gani? Nimewahi kuishi Spain kidogo na nimekutana na watu wenye shahada ya uzamili wakifanya kazi zinakaribu kufanana na hizo ulizotaja.

Ukiwa kama mwalimu ulitakiwa utuambie kuwa katika kazi yako unadhani unawaandaa wanafunzi wako wawe akina nani katika jamii. Je, unawapa elimu inayowapa 'ujuzi' fulani? Endapo wewe ni mwalimu wa shule za upili unayetumia mtaala huu wa MoEVT unalo jibu!

Tunahitaji wasaidizi wa nyumbani WASOMI, na si mbumbumbu!


aiseee... we mtu hauna uruma na watanzania wenzako. sidhani kama waimaanisha hiyo red... kama waimaanisha basi wwndio MBUMBUMBU
 
Back
Top Bottom