Amani ndani ya Kijiji cha kakola yatoweka gafla.

Serikali Ya Raisi Jakaya Kikwete ni mfu ndio maana imeziba masikio mabomu ya nini kwa watoto yote ni kuonyesha mabwana zao Barrick kwamba hakuna pua itakayonyenyuka kudai haki,mambo ya ajabu sana,Polisi wapambane na wanafunzi wasio hata na silaha yeyote
 
Chonde chonde polisi msije mkatuulia wanafunzi hao ni watoto wadogo sana na wana hoja yamsingi sana kamamnaweza kuleta noma kwa serikali ipeleke walimu hata kwa mabomu na rirasi za moto hapo ntawaunga mkono lakini kwa wanafunzi tena wanaodai haki zao ntawachukia mpaka siku ya kufa kwangu na laana yake itarudi kwa watoto wenu
 
Bugarama, Kakola, Nyanzaga...the list goes on...ni explorations za gold tu na watu wakuja. Kupigania elimu ni kitu cha kutia moyo sio kupigania vitu visivyo na manufaa kwetu na hata kwa watoto wetu. Mwisho wa siku tukiwa na elimu hiyo gold tutaitafuta wenyewe badala ya kusubiri kina Barrick na wengineo.

sasa hali hiyo haileti masikitiko tu bali inatia hasira kali. to hell with ccm, to hell with kiqwete, to hell with gold barricks. ccm siku zako zimehesabiwa na kubainika kuwa zimekwisha na badala yake unaishi na kupumulia muda wa mkopo
 
Mkuu tulipofikia haihitaji kusubiri, inatakiwa wazalendo kuchukua hatua za haraka

Inshalaa hatua zitaanza kuchukuliwa hapa Arumeru pale Magamba yatakapo iba kura zetu, safari hii utakuwa msako mpaka magogoni, ule usemi kuwa salvation shall come from north huenda ukatimia wait and see!!
 
Sasa kwa nini hao wanafunzi wanaandamana na kufanya fujo? maana naamini kwua polisi walikuja kutuliza fujo.

hv unafikir wewe kwa akil yako polis siku hz wanatuliza ghasia au fujo?.Faham kuwa polis ndo wanaleta fujo na wanaongoza kwa uvunjifu wa amani na haki za binadamu hap tz!.Huwez kutumia mabomu na maji washa kwa wanafunz wa kata!Ni aibu na ocd anatakiwa kutoa ufafanuz wa kina au afukuzwe kazi.

Ni aibu na dharau kubwa kwa shule iliyokaribu na mgodi wa dhahabu then inakosa waalimu na badala yake wanapewa kichapo!.The time will tell na wananch watayazoea hayo mabomu haki pamoja na uhuru kutoka kwa mkoloni mweusi vitapatikana.Naomba kuwasilisha!.
 
thats the problem of most of you tanzanian, you just sit there and write rubish, kama kweli mnataka mabadiliko tokeni humo maofisini na kwenye ma computer ingieni kwa street like arabs and others who managed kuitoa serikali madarakani. there are proper channel na si kuvictimize watu wengine ambao its non of their business

think outside the box and acquireknowledge buddy and dont sit there and blame, ask yourself what have you done personally?

Don't punch above your weight!! Your English proficiency is sickening, andika kiswahili huenda ukaonekana smart zaidi. Ukiachilia hilo, sioni ni watanzania wangapi unawalaumu kwa hili. Hii sio Siasa, ni dai la wanafunzi. Aliye Dar anatokaje nyuma ya tanarishi na kujiunga na madai ya waalimu wakati anahitaji kuwa na mshahara bora na mazingira safi ya kazi. Put the blame where it is due, not all over the place!!
 
Hivi kama Polisi wangetumia BUSARA ndogo tu ya MTOTO wa CHEKECHEA wakawalinda hao wanafunzi hadi huko wanako kwenda KUDAI WALIMU wa kuwafundisha POLISI wangepungukiwa na nini? Au Siku hizi RPCs na OCDs wanapandishwa vyeo kufuatana na idadi na mabomu waliowarushia RAIA?

NGUVU ZOTE hizo mabomu ya MACHOZI ni maana yake? Kwamba hatuna tena hata uwezo wa kufikiri kidogo?
Well said mkuu, utaratibu wa kuwateua wakuu wa asasi hii na nyingine za kiserikali umekaa kifisadi fisadi, na hauko transparent. Ndiyo maana juhudi binafsi za kujipendekeza na kujikomba serikalini zinahitajika la sivyo utabaki papo hapo mpaka ustaafu. Ukichungulia sana ni wajinga jinga tu ndiyo wanaopandishwa vyeo tena kwa misingi ya kisiasa, kikabila au kwa rushwa.

Idadi ya wananchi waliouwawa na Polisi kwa kipindi cha u IGP wa Mwema inazidi ya ma IGP woote tangu tupate Uhuru; kisha huyu jamaa anajinadi na Polisi Jamii yake, ni nini basikama si usanii tu huo? Shame on them all!
 
Ndugu wanaJF ni kwamba hali ya amani ndani ya kijiji cha Kakola kilicho jirani kabisa na mgodi wa dhahabu wa BARRICK BULYANHULU GOLD MINE imetoweka gafla baada ya polisi kuwatawanya wanafunzi wa shule ya Sekondari Bulyanhulu ambao walikuwa wanaandamana kudai walimu waletwe shuleni hapo ili waweze kufundishwa.

Shule mpaka sasa haina walimu wa kutosha.

In short hali ni mbaya mpaka sasa mabomu ya machozi na risasi za moto zinazidi kurindima kwenye anga la kijiji cha Kakola.

Polisi kufeli f4 ndo wameanzisha bifu na wanafunzi.
 
Hii ndio Tanzania chini ya J.K
1. Pesa ya posho za vikao, semina, warsha ipo.
2. Pesa ya kununulia magari mapya (VX new model, BMW, Mercedes Benz, Hummer) kila mwaka, zipo.
3. Pesa kuwalipa wafanyabiashara (Hewa?) waliopata hasara kutokana na msikitiko wa uchumi, imejaa we peleka mchanganuo.
4. Pesa ya kuajiri askari wapya, mabomu ya machozi, magari ya maji ya kuwasha, risasi za moto (badala ya plastick) za kuzuia maandamano, zipo kibao.
5. Pesa za sherehe kuuuuuuuubwa za uhuru kila mwaka, zipo mpaka zinamwaika (Nadhani za mwaka huu tutaoneshwa kukata chuma kwa meno).
6. Pesa za ziara za kuombea pesa hizo zipo bajameni mwe!
7. Pesa za miradi hewa, posho za safari hewa, mishahara hewa na hata za hewa yenyewe zimejaa.
8. Peshaaaaaa za kuwalipa akina Wasira posho za kupanda jukwaani kumwaga matusi kwa wapinzani wao, zimejaa tele.
HIYO NI SIDE A, SASA ANGALIA SIDE B YAKE!!!!!!
1. Pesa ya kununulia madawa, vifaa vya hospitalini, bajeti haitoshi wananchi vumilieni.
2. Pesa za mishahara kwa walimu hasa wale wapya, kuweni wazalendo bajeti ni ndogo sana.
3. Mishahara ya madaktari na wafanyakazi wengine kuongezwa walau kujikimu tu. Nyie madaktari sio wazalendo mnajipendelea ninyi tu, na wengine je? (Wamesahau charity starts at home)
4. Upungufu wa nishati ya umeme, serikali inajipanga kununua jenerator ya umeme wa dharula itakayotumia mafuta mazito, hiyo itafungwa mwanza!!!! Mayo nene, about 1200 kms from ports mtajenga pipe line, ama kuna visima vya mafuta vimegundulika Geita?
5. Miradi ya umeme mikubwa ya kudumu hela hakuna, as if Tanzania ita sease kuexist 2015!!! Maana akili ya serikali yetu imekomea 2015.
6. Wananchi wakilia hawapati maji mkong'oto, wakilalamika hawana umeme kichapo, mara jamani bei ya chakula imepanda, kipondo. Wakilalamika polisi tulindeni tunauawa, ndio kama vile waliokwisha kufa hawatoshi, maroboti yanafyatua risasi watu wafe zaidi ili yenyewe ndio yashike mahali pa wanadamu.
7. Wastaafu wanadai malipo yao kwa udhalilishwaji mkubwa, maroboti yanatumwa kuwatandika, simply wao hawatoki miongoni mwa wanadamu, hawana wazazi, hawaoni tofauti kati ya wazee, vijana wala watoto. Ni kupiga tu, kuua tu.
8. Hivi nyie mashine za mauaji, mtajisikiaje kwenda kwenye msiba wa mwanao, mkeo, baba, mama, dada, kaka yako (kama mnao), aliyeuawa wakati akienda sokoni kutafuta chakula chako wewe mwenyewe? Unajisikiaje kumzika nduguyo aliyeuawa kip....u..u.zi na askrai mweenzio aliyeamua kufyatua risasi hovyo, ati anawatawanya watu waliokusanyika stendi ya basi, wakiimba "serikali, komesha mfumuko wa bei"? Hilo ni kosa linalogarimu uhai kweli. Pamoja na kujifunza uharamia, kumbukeni nanyi pia mna damu na nyama kama sisi, mna roho kama sisi, mtakufa kama sisi. Tunahitaji kuishi kama hao waliowatuma, tafadhali msituue maana hatutawasamehe!!!!
 
Back
Top Bottom