Ama tupaaze sauti au tukae kimya milele!

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
Kuna jamaa yangu alinisimulia kisa cha abiria mmoja ambaye alikanyagwa mguu na abiria mwenzake kwenye daladala lililoshona abiria. Abiria aliyekanyagwa alipoinua macho yake kuangalia aliyemkanyaga, akabaini ni jitu la miraba minne. Akaingiwa na hofu, ujasiri ukamtoka akaishia kusema "Kaka, samahani mguu wako uko juu ya mguu wangu." Alitakiwa kueleza jinsi alivyokanyagwa badala yake akaishia kuomba radhi!

Watanzania tumeshakuwa kama huyo jamaa aliyekanyagwa, tunaibiwa rasilimali, watu wanafoji vyeti, umri, nchi inaendeshwa kama shamba la bibi na mambo kibao ya kusikitisha, hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika nasi tunabakia kuwaomba radhi watawala kwa kusema "samahani mguu wenu uko juu ya mguu wetu".

Ifike mahali ama tuseme "mnatukanyaga" au tunyamaze milele!
 
Mkuu ume toa mfano mzuri. Tunaishi kwenye jamii ambayo ina heshima kupita kiasi. Tuna heshimu wakubwa kwa sababu ya kutu pita kiumri, tuna heshimu matajiri kwa sababu ya kutu pita kifedha na tuna heshimu utawala kwa sababu ya kutuzidi madaraka. Nitoe mfano. Kwenye familia nyingi za Kiafrika baba au mama akisema kitu mtoto haruhusiwi kupinga hata kama ni wazi mzazi kakosea. Kwenye familia nyingi mtoto haruhusiwi kutoa mawazo yake bali ana fuata tu alicho ambiwa. Kwa sababu Watanzania wengi wame lelewa katika hali hiyo hata wakiwa wakubwa wana kua na ile hali ya kwamba kuna watu wakisema kitu basi mimi hata kama naona nima kosa sitaki kuzungumza. Hiyo hali ya kumuogopa huyo mtu wa miraba minne haitokani na aliye kanyagwa kuwa mdogo kiumbile bali kuogopa kuzumgumza dhidi ya mtu aliye mkubwa zaidi. Niamini kuna watu wapo hata wawe wadogo vipi wata jitetea dhidi ya aliye mkubwa kivipi.

Lakini mkubwa hata kwenye jamii yetu iliyo na heshima mtu akionewa sana ipo siku ata inuka tu. Mtoto anaye pigwa na baba ake pasipo sababu ipo siku atamkemea mzazi, masikini anaye nyanyaswa na tahiri wake ipo siku atasema ina tosha nk. Angalia hata historia ya ukoloni. Kwa nini tuli tawaliwa miaka mingi? Ni kwa sababu ya heshima liyo pindukia ya kwamba ni lazima tufuate amri ya mkubwa. lakini mateso yalipo zidi watu wakaamka na kusema basi ime tosha, sito nyanyaswa tena. Ndipo tukaanza kudai uhuru wetu.

Kwa hiyo mkuu yote unayo ona sasa hivi yanaendelea, watu kutoa mawazo yao dhidi ya viongozi wachovu ni hali ya kuchoshwa. Tume fika katika kipindi ambapo tume gundua tunaonewa, tuna taka kuzungumza lakini bado ule moyo wa kufanya kwa vitendo hatuna. Ikifika kipindi ambapo kweli Watanzania wame choshwa naku hakikishia hali ita badilika. Kwa hiyo ni kazi ya wale wenye sauti na ubavu kwa sasa kuwapa moyo wanyonge na kuwa ambia hakika wanaye muogopa ni mdogo kuliko wadhaniavyo. Huko ndipo tunapo hitaji kuelekea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom