Ama kweli nchi hii imekaa kifutuhi futuhi, TBC wamtaja Lyatonga Mrema kwa cheo cha Dokta

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Haka kanchi sasa kanaelekea kubaya. Ni juzi tu nimesikia Lyatonga Mrema ametunukiwa udokta na jamaa fulani kutoka Afrika Kusini. Sherehe ya kutunukiwa udokta ilihudhuriwa na Mrema mwenyewe na mkewe pamoja na huyo jamaa nae akiwa na mkewe. Cha ajabu leo kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku mtangazaji wa TBC amemtaja Mrema kama Dr. Lyatonga Mrema. Mambo hayo! Itafika mahali waheshimiwa wote bungeni watakuwa ni madokta. Kwa sasa Mhe. Mrema na Mhe. Mwakyembe sasa ni ngoma droo.
 
mbona hata ww unaweza kuwa "RAISI" nn udokta.
:D:D
 
Nadhani TBC1 kuna tatizo la msingi pale.Sisi kama wamiliki wa chombo hiki(kwa maana kuwa ni cha umma)yatupasa kuchukua hatua mapema....mambo yanayofanyika kwa sasa TBC1 ni vituko,kuanzia vipindi na mambo mengine.Nadhani mzimu wa Anko TIDO MHANDO bado unawanyemelea hawa watu......
 
Mnashangaa nini mbona kuna wabunge ni maprofesa kama Profesa Maji marefu? Katika CCM fani zinadhalilishwa Yakima mfano.
 
Back
Top Bottom