Alphonce Mawazo akabidhi kata ya Sombetini rasmi kwa Ally Bananga

Mathias Lyamunda

JF-Expert Member
Apr 4, 2013
1,369
558
Jana Chadema Arusha ilifanya uzinduzi wa kihistoria wa uchaguzi wa kata ya Sombetini na le Captain Mawazo alitoa Hotuba kali iliyowaliza wana Sombetini wakikumbuka jinsi alivyowatumikia kwa uaminifu.

Jana akisikilizwa na Maelfu ya wananchi wa Sombetini Captain Mawazo alimpa wosia mzito Bananga kuwa anakwenda kuwatumikia watu masikini kwahiyo watoto wa masikini ni watoto wake, wakifukuzwa shule kwa kukosa Ada wasiende nyumbani kwa wazazi wao waende kwa Ally Bananga, yeye ndo baba na Mama wa watoto wa Sombetini.

Hotuba yake ili acha Visio kwa watoto na akina mama waliokuwepo kwa wengi mkutano. Nukuu: "Leo kwa moyo wa UJASIRI na unyenyekevu mkubwa na kumkabidhi Bananga kitu pekee kilichonifanya nijulikane kama mwanasiasa Arusha na nje ya Arusha, na kumkabidhi heshima ya kuigwa Mh. Diwani, MAMLAKA siyo kitu kidogo, nimeshuhudia watu wakiloga na kuua ili kuwa madiwani, hiyo na kuacha maana najua wewe ni diwani sasa, pili na kuacha posho wewe na wa wananchi wote WANAJUA kwamba sina hela na nina familia na mahitaji mengine, lakini hivyo vyote haviniumi, kinachoniuma kabisa ni kukua chia MPENZI wangu wa pekee ambayo ni kata ya Sombetini, MACHOZI ya kina mama hawa si kwasababu NYINGINE Bali ni upendo walionao kwangu uliotokana na utumishi na upendo usio na ubinafsi kamwe, niliwahi kutangaza watoto wote wa Sombetini ni watoto wangu, wakifukuzwa shule wasiende nyumbani kwa wazazi wao WAJE kwangu na divyo ilivyokuwa na wananchi ni mashahidi" mwisho wa kunukuu.

Alimsihi Bananga Avae viatu vyake kisawasawa.

Pia aliwashangaa WANASIASA wanaohutubia udini na ukabila aliwauliza wananchi ni nani anayeteseka nchi hii zaidi ya mkulima na mfugaji? Alikumbushia matukia ya kiteto ya wafugaji na wakulima walivyo uana kutokana na chuki za kikatil a zinazopandikizwa na watawala wa CCM, ni SERIKALI ya ccm ndio iliyoua Ng'ombe za wamasai kwenye operation tokomeza ujangili, alisema, nanukuu:

"Tanzanite iko kwenu, mbuga za wanyama ZIKO kwenu, mbaya zaidi wamewageuza kuwa Sehemu ya utaki kwa kuwapiga picha na kupiga picha umasikini wenu, na imewapelekea vijana wenu KUKIMBILIA mjini kuwa walinzi wao kwa kukosa ardhi ya kulima na mails na malisho ya Ng'ombe kwahiyo ndugu zangu wa Maasai adui yenu siyo MCHAGA wala mdengeleko adui yenu ni CCM".

Aliwaomba wananchi wote wa sombetini wamchague Bananga na waichague Chadema.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    57.9 KB · Views: 906
Captain Mawazo akihutubia Maelfu ya wakazi wa Sombetini
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    100.9 KB · Views: 685
  • image.jpg
    image.jpg
    77.7 KB · Views: 646
Adui yenu si mchaga ila ni ccm inayopelekea nyie kuwa walinzi wake. Dah! Inauma lakini mh
 
Kamanda Mawazo ataenda lini Mtae............huko CCM imepita bila kupingwa!
 
Huko walevi wa gongo wamejaa huko.,hakuna cha kushangaza

asante muuza gongo, tupe na eneo lingine la wateja wako, vp lumumba pale si mmeshawamaliza vijana akili zao kwa biashara yako? wapi kwingine kizota au? acha watu wafanye kazi wewe baki na porojo.
 
Mawazo alimwomba Bananga avae viatu vyake, na ampende mpenzi wake awe wake, na kweli watu wa Sombetini walimpenda sana Mawazo kwakuwa ni mchapa kazi wa kweli...............

Mkuu picha zimegeuzwa kichwa chini miguu juu
 
Kazi imeanza mwigulu atakuja ar kipindi hiki jamani?kapata ulaji kawa waziri mdogo kafungwa mdomo sasa wabunge watammaliza kwa maswali!!! au amewekwa hapo ili ccm ipate pesa za kampeni the coming year!!
 
Wanafanyia usodoma nawugomora wao pale ngusero gest house kwanini mkae gest bananga huna kwenu
 
baada ya ufunguzi wa kampeni hiyo jana chama cha demokrasia na Maendeleo leo kimeendejra na kuwashukru wananchi wa sombetini kwa kuipigia kura chadema..
jukwaani amepanda Alphonce Mawazo anawauliza wangapi wanamlaumu kwa kuhamia chadema hakuna hii inamaanisha wote walioko hapa walifurahishwa na kitendo chake cha kukihama chama cha wauwaji majangili, wauwazi anasema kazi aliyonayo kwa sasa ni kupigania haki za wanyonge, anasema alipokuwa kanda ya ziwa alikuwa na ugomvi na marpc, maocd wakimwita ni mkorofi na ndiyo ilivyo nchi hii ukidai haki zako unaitwa mkorofi mhuni....nina raha sana tangu ni hame ccm, ccm ni zaidi gereza.. anasema polisi wameanza kushilikiana na green guard kupiga watu mitaani anasema safari hii hatutakubali watu wetu kufa/kuumizwa na maccm na polisi ccm...
 
Kamanda wa Chadema ameshambuliwa na Green Guard wa CCM amelazwa hospital ya kaloleni kwa muda kwaajili ya uchunguzi na baada muda anaweza kuamishiwa mout meru kutokana na maumivu makali kwenye mbavu na mgongo baada kupigwa na marungu akipita na toyo barabarani.uongozi wa Chadema unaendelea kuwafuatilia wahusika wa tukio hili la kikatili.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    85.3 KB · Views: 330
Hivi kweli Tanzania yetu hatuwezi kufanya kampeni za kistaarabu bilia kupigana? Huu utamaduni ukiendelea kukumbatiwa utaliangamia taifa hili kwa hakika
 
hao ccm sikuhizi wanatembea na pisto viunoni mwao halafu kutuambia tusichezee amani ya Tanzania. Kama ipo tahadhari ya nini?
 
Mi nasema apigwe tu, uhuni umeifanya ARUSHA irudi nyuma kimaendeleo kwa SIASA za ovyo ovyo za LEMA wanywa viroba wenzake.
 
Mungu ailaze mahali pema peponi enzi hii ovu ya CCM. When the darkness increase, know that the morning is near. Get well soon kamanda.
 
Last edited by a moderator:
ahhhh,mbona huyu hajaguswa,ana sura yake nzur kabsa,huyu alipaswa akamatwe na vice!!huyo anachelewesha tu wagonjw kutibiwa
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom