aliyeuza nchi kwa Karl Peters 1884, huyu hapa

bora enzi za hawa mababu zetu pamoja na kuingia mikataba mibovu viwanda na miundombinu vilijengwa na processign industry pia walijenga hata system ya elimu waliianzisha, sasa hawa wasomi uchwara wa sasa wao hata kitu hakiachwi, wanavuna kila kitu! kuku na mayai, na visomi vyetu uchwara vinawafagilia tena na heshima wanapewa eti wawekezaji!
 
Sisi tumesoma, tumesafiri sana, tunauelewa, Hivyo mwaka 2110 kizazi kijacho kitasemaje kuhusu Loliondo, Buzwagi, Bulyanhulu, Geita, Kahama na Ardhi wanayopewa wageni kwa kisngizio cha Kilimo kwanza? Na chochote watakachosema, kutakuwa na sababu ipi ya kusema vinginevyo?
Hii laana mimi sijashiriki, mlioshiriki muandae majibu maana makaburi yenu yatafukuliwa na vilembwe wenu na kuangalia mafuvu ya vichwa yenu kama yalikuwa yamejaa maji au matope
 
Are you mad, if someone puts a gun to your head (by directly doing it or giving guns to your enemies, utakataa wakumalize).. Hii mikataba ilikua null and void by the fact that the chiefs did not understand the legal basis of the agreements and thus just rubberstamped things that they did not even understand. Dr. Peters, (I'm so glad the worms have already eaten his brain..the mofo..) was a tyrant and he defiled our native women in Kilimanjaro and other places. He killed Africans like dogs and raped our grandmothers, in Germany he was demoted from the position of Reich Commissioner after it was discovered that he is a sadistic mean and inhumane person. His title and pension was reinstated by the Kaiser and later Hitler..

Karl Peters - Wikipedia, the free encyclopedia

Someone should exhume his body and feed it to the pigs.

Mkuu Kinyabiss nafikiri tuwe fair kwa Ngambo N.

Nilivyomuelewa mimi ni kwamba Mababu zetu walikuwa hawana elimu ya kutambua "Law of Contract" na hata kusoma maandishi. Hatuwezi kuwalaumu kwa hilo kwani kwao hawa utawala ulikuwa na mambo makuu matatu, "barter trade, agriculture & hunting", "safety of the society" and "Polygamism". Huenda kwa wao kudanganywa na kukubali kulikuwa na manufaa sana kwa sisi wa leo, hasa katika upande wa elimu na kujifunza kwa makosa yao. Our ancestors foward looking abilities were limited to"How much they expect to harvest next season, how many wives they'll add, who's planning to attack them", They didn't think about future generations. Sasa sisi leo hii miaka 126 tangu mkataba wa kwanza wa kilaghai na miaka 49 tangu tujiite tupo huru na pia tuna wasomi na wataalam wa kutambua mikataba mizuri na mibaya bado tunashindwa kuwa na forward looking ability for the benefit of our children, grand, grand, great... children on how they gona live and say about us on the mess we are doing for entering into "lousy contracts", borrowing for extravagance spending and personal benefits?
 
"In exchange of for a few shotguns one receives a paper on which some negroes have made their mark by way of signature" - Bismarck - the German Chancellor who convened the Berlin Conference - as quoted in Juhani Koponen's PhD cited above.

tofauti ni moja tu, wale walikuwa hawajaenda shule, kizazi hiki kimeenda shule na kina qualifications kibao lakini kinachofanyika ni madudu.
 
Natamani miongoni mwetu wawepo akina Kimweri, Mirambo, Isike, Mkwawa, Kinjekitile Ngwale, Chabruma and the likes.
 
Natamani miongoni mwetu wawepo akina Kimweri, Mirambo, Isike, Mkwawa, Kinjekitile Ngwale, Chabruma and the likes
Thubutu, hatuna tena watu kama hao kwenye Tanzania ya sasa, kizazi cha sasa sijui akili zetu zinapungua kila siku?
 
Nawalaumu wanaouza nchi yetu sasa wao wamesoma lakini bado wanauza nchi yetu, hao ndio wa kulaumu
.

Hao wako wengi. Tizameni Maafisa Ardhi wanavyouzia viwanja vya wazi na vya ufukweni. wanawakosesha haki ya wananchi kufika kwenye Beach katika nchi yao wenyewe. watoto wanakosa sehemu za michezo na mahali pa kumpumzukia. Mmeyaona yaliotokea kinondoni. kama wakiwekwa ndani kwenye wilaya tatu tu mabo yatakuwa safi
 
ukweli hata kama mababu zetu walikosea makosa yao si kama yanayofanywa na wasomi wetu leo hii na mpaka babu zetu kudanganyika aikuwa kazi raisi kama wasomi wetu tulowapa dhamana ya uongozi na babu zetu walipogundua walipigana mpaka tone la mwisho awakusema tumeshasaini tungoje mkataba uishe no walipigana wote tumesikia habari zao.
sasa vipi hawa walouza nchi bila kurubuniwa sana kama babu zetu ambao awakwenda shule kabisa mimi naona hawa wasomi tulowapa dhamana ya uongozi kwa sababu ya elimu zao za juu ni bora tuwanyima nafasi kisha tuwaweke wale ambao hawajasoma kabisa kwani wana akili za kuzaliwa na historia inaonyesha tangu awali wajerumani walipata tabu sana kuwadanganya
 
Thubutu, hatuna tena watu kama hao kwenye Tanzania ya sasa, kizazi cha sasa sijui akili zetu zinapungua kila siku?

Unataka kuniambia kuwa katika watu 40 millioni hakuna mwenye uchungu wa kina Mirambo, mkwawa,isike etc is that possible, wapo ila hawasemi, wakisema hawasikilizwi labda hawasemi sana inabidi sauti iongezwe, badala ya kusema mmoja watano au kumi tuseme wengi.
 
Hata mitemi wa zamani nao walikuwa na makosa yao. Kuna wengine walikuwa wanahasi askari walinzi makusudi ili wasije zaa na wake zao, kuna wengine waliuza wenzao katika utumwa na wengine walitoa mhanga watoto hasa wa kike. ( young girls were buried alive in the anticipation of becoming wives to the chief once the chief died) That is the part of history that we sometimes ignore.

Hata hivyo labda hatuwezi kuwa kama hao akina Isike na wengine, lakini tunaweza tukajitahidi kuiongoza nchi yetu, tunahitaji tu kuamua na kuachana na tamaa na maringo ( ego?) yanayotokana na kuwa na madaraka.
 
Nimeikuta hii michuzi blog, inasikitisha sana. Hii ilikuwa 1884 miaka 126 iliyopita karibu karne 1 na robo. Maskini Mbwela alikuwa hajasoma hivyo hata hiyo sahihi sidhani kama ilikuwa ya kwake na hata kama ilikuwa ya kwake katu hakujua anachosaini.

Humtendei huyu babu haki kwa kuweka heading inayosema "Aliyeuza nchi kwa Karl Peters huyu hapa" halafu kwenye thread umeandika hayo hapo juu.

Sasa unasema huyu babu hakujua alichosaini, halafu unasema aliuza nchi kwa Karl Peters, ameuza uzaje wakati hata kama saini ni yake hakujua alichosaini?

Contradiction.

You can't eat your cake and have it too, it is against the laws of nature. Huwezi kumkashifu huyu babu kwamba kauza nchi, halafu uka mu excuse kwamba hakujua alichofanya. Otherwise utaonekana kama unatumia tactics za magazeti ya tabloid kuuza nakala, kichwa cha habari kikubwa, halafu habari tofauti na kichwa cha habari.

Tuambie kwamba huyu babu aliuza nchi kwa kujua fika anauza nchi na ondoa hizo habari za hakujua anauza nchi.

Ama sivyo, ondoa hiyo heading yenye kashfa nzito, unaweza hata kusema "aliyedanganywa na Karl Peters huyu hapa".

Kamwe huwezi kumkashifu huyu babu Chifu halafu hapohapo ukatuambia hakujua alilofanya, alaa, sasa unamkashifu kwa sababu gani?

You just can't have it both ways.
 
mbona kikwete anajiuza marekani??????????
acha yaliyopita tujadili maisha bora kwa kila mtanzania na ajira zille tele yaaaniiiiii.....AJIRA 1,000,000....
 
Humtendei huyu babu haki kwa kuweka heading inayosema "Aliyeuza nchi kwa Karl Peters huyu hapa" halafu kwenye thread umeandika hayo hapo juu.

Sasa unasema huyu babu hakujua alichosaini, halafu unasema aliuza nchi kwa Karl Peters, ameuza uzaje wakati hata kama saini ni yake hakujua alichosaini?

Contradiction.

You can't eat your cake and have it too, it is against the laws of nature. Huwezi kumkashifu huyu babu kwamba kauza nchi, halafu uka mu excuse kwamba hakujua alichofanya. Otherwise utaonekana kama unatumia tactics za magazeti ya tabloid kuuza nakala, kichwa cha habari kikubwa, halafu habari tofauti na kichwa cha habari.

Tuambie kwamba huyu babu aliuza nchi kwa kujua fika anauza nchi na ondoa hizo habari za hakujua anauza nchi.

Ama sivyo, ondoa hiyo heading yenye kashfa nzito, unaweza hata kusema "aliyedanganywa na Karl Peters huyu hapa".

Kamwe huwezi kumkashifu huyu babu Chifu halafu hapohapo ukatuambia hakujua alilofanya, alaa, sasa unamkashifu kwa sababu gani?

You just can't have it both ways.

Kiranga sioni contradiction hapo:

1. Aliuza nchi na mkataba ukijuwa wa maadnishi

2. Hakujua kusona hivyo hakujua alisani nini

3. Baada ya kusaini asichojua wajerumani wakachukua nchi na kufanya koloni lao.

4. Kashfa ( kwa maana halisi ya neno hilo) iko wapi hapa kiranga
 
Then,Alipewa kioo akajiangalia kwenye kioo akacheka akaona ile reflection nayo inacheka , akanuau na reflection ikanuna jamaa akaona hawa watu wa ajabu sana, akakaa akatafakari wakampa shanga akachanganyikiwa, akamwita wife akaona anapendeza akampa bunduki akajaribu akaona du makabila mengine watanikoma basi hayo tu.

Now: wanapewa tiketi, wanapanda ndege na wake zao, wanaalikwa dinner, wanapewa dola wanaingiza kwenye offshore accounts , wanasaini mkataba bila hata kusoma, wanarudi nyumbani. THE END.

Mkuu si tiketi tu tu bali tiketi na wanawake siku chache kabala ya mazungumzo na baada ya mazungumzo.Practiced in France,India, Japan and Dubai.
 
Kiranga sioni contradiction hapo:

1. Aliuza nchi na mkataba ukijuwa wa maadnishi

2. Hakujua kusona hivyo hakujua alisani nini

3. Baada ya kusaini asichojua wajerumani wakachukua nchi na kufanya koloni lao.

4. Kashfa ( kwa maana halisi ya neno hilo) iko wapi hapa kiranga

Swala zima la kuuza nchi lipo katika mkataba wa maandishi, document ya kuuza nchi ni mkataba wa maandishi, kama alisaini mkataba wa maandishi bila kujua mkataba wa maandishi unasema nini, then huwezi kumlaumu kwamba kauza nchi.

Indeed swala la mtu kuuza nchi kwa kusaini kipande cha karatasi lilikuwa halijulikani kwetu wala katika legal system yetu. Sasa unachomshutumia ni nini wakati kasaini kitu asichokijua, kitu ambacho kimsingi ukiangalia utaona kadanganywa tu kama unataka kuamini kwamba alikuwa hajui kitu?

Hii inaitwa "blaming the victim", eti mtu katoka bush, kafika stendi ya basi na mzigo wake, watoto wa kihuni wamemuibia mzigo wake, wewe unamsema kauza mzigo.
 
Kiranga, hakuna mahali ambapo nimemlaumu huyo chifu, sanasana nimemuonea huruma:

"Nimeikuta hii michuzi blog, inasikitisha sana. Hii ilikuwa 1884 miaka 126 iliyopita karibu karne 1 na robo. Maskini Mbwela alikuwa hajasoma hivyo hata hiyo sahihi sidhani kama ilikuwa ya kwake na hata kama ilikuwa ya kwake katu hakujua anachosaini."

Ni wapi nimemlaumu katika hiyo paragraph, lawama zangu zote ziko kwenye uongozi wa sasa na hii iko kwenye paragraph 2. Isichukuliwe kuwa namlaumu chifu no way. Nalaumu ruling clique ya sasa.
 
Heading ya thread inasema

"aliyeuza nchi kwa Karl Peters 1884, huyu hapa".

Heading ya thread imebeba kashfa nzito. Mtu asiyejua akiona heading hiyo anasema "Yuko wapi huyo mshenzi".

Akija kufungua thread anakuta habari tofauti, kumbe jamaa alikuwa hata hajui deal linaenda vipi.

Sasa heading inasema jamaa kauza nchi, content zinasema jamaa hakujua deal, kipi ni kipi?

Ndiyo maana nikasema hii ni sawa na sensational tabloidism, watu wanaweka heading ya uongo ili tu kupata wasomaji, this is low.

Ongea na Mods ubadilishe heading potofu kama unaona Chifu hakujua deal.
 
Jamani, mbona kuna machifu wengine walipigana kiume na hao hao Wajerumani kama vile Mkwawa, Mirambo na yule wa Vita vya Maji Maji? Huyu wa Mbwela wa Wazihua alikuwa fisadi tu, kama hawa wengine tunao siku hizi.
 
Back
Top Bottom