Aliyesambaza meseji za kumkashifu Slaa ni....

Waendelee na mipango yao hiyo ya kuchafua nchi, lakini wakae wakijua kuwa iwapo tome moja la damu ya mtanzania itamwagika kwa ajili ya wao kuingia madarakani, hakika, damu hiyo itawalilia toka juu
 
Shamte atakwenda underground kuanzia leo.Naamini CCM inatupeleka kubaya,why all these?
Push mobile inahusishwa na fisadi aliyekuwa BOT na akahamishiwa TIB kupokea pesa za EPA zinazorudishwa.Kweli wakubwa wanatuona tu wajinga kiasi hiki?
 
Hakuna siku nimeshasoma thread kwenye jf nikajisikia machozi kunilenga.I cant believe this is happening in Tz,kwamba imefikia watu wanaishi kwa hofu kwa sababu tu wameunga mkono chama fulani cha siasa.Halafu hii kitu ya kubagua kabila fulani ni mbaya sana maana mbegu imeshapandwa na kama haitang'olewa mapema itaota na kuzaa matunda ambayo ni genocide.Hapa hamna namna nyingine ya kung'oa mbegu hii isipokuwa kwa kuwafikisha wahusika wote kwenye vyombo vya sheria.

Hivi Kikwete amelaaniwa kiasi hicho kweli?Ubinafsi ndo umefikia hapa kweli.Madhara ya kuwa na kiongozi ambaye analeta mzaha katika kila jambo ndo haya.Hakufikiri hili suala ni nyeti kiasi gani.
 
Duu, hii nimeiona ONLINE:

--Rashid Shamte, CEO, Six Telecoms Company Limited (TZ)

Kwenye ile makala ya DEWJI akicheza ngoma, niliandika wazi kuwa tutawachukia Wahindi na Waarabu bure tu ila wabaya wetu ni hawa Mipingo wenzetu. Junius mtani wangu, utakuwa unakumbuka hayo maneno ingawa ulicheka, hilo halikuwa jambo la kucheka ila kulia.

Nazidi kuamini kuwa Serial Killer, siku zote huuwa watu wa RANGI ZAO.

Uchaguzi ukiisha, wote hao akina January Makamba et el wana kesi ya kujibu au kusaidia upande wa mahakama. Hata wakikwepa mwaka huu, mwaka 2015 tunao na kibaya zaidi watakuta mwenzao ana Kinga ya Urais ila wao watakuwa na hali mbaya sana.

Nyie Wajinga, someni alama za nyakati na mjitakase maana mna bahati ya kujua SAA NA WAKATI.

Kinga ya Urais labda kwa mahakama za Tanzania ikiwa mambo yatabaki kama yalivyo, LAKINI nakuambia kinga chovu kama hizo hazipo kwenye mahakama za kimataifa. MILOSEVIC, KARADZIC, MILUTINOVIC wote WAKIWA MARAIS wa Jamhuri ya Kisoshalist ya YUGOSLAVIA ya zamani WALINYEA na mmojawao anaendelea KUNYEA ndoo kule Uholanzi kwenye mahakama za uhalifu wa kivita. Pia ikumbukwe, kuwa WAZIRI MKUU wa zamani wa RWANDA wakati wa GENOCIDE Mh. JEAN KAMBANDA alinyea ndoo kwenye mahakama ya mauaji ya kimbari ya pale ARUSHA, na kwa sababu alipatikana na hatia na KUFUNGWA MAISHA, ataendelea kunyea ndoo ile hadi mwisho wa maisha yake. CHARLES TAYLOR wa LIBERIA naye kama kawa....

Hao WOTE ( Rashid SHAMTE, Januari MAKAMBA, MTANDAO, NA WALIOMTUMA) wanaojenga uchochezi kwa MANENO na MATENDO yao wajue kitu kimoja cha msingi -MANENO na MATENDO yao yanaacha nyuma yao MTIRIRIKO wa USHAHIDI DHIDI yao, na Jumuiya ya kimataifa kupitia INTERNATIONAL CRIMINAL JUSTICE SYSTEMS( ijapoonekana kuwa kimya) inafuatilia mwenendo wa mambo yalivyo hapa Tanzania, na ENDAPO amani ya Tanzania itatoweka katika uchaguzi wa mwaka huu kwa msingi nilioutaja hapo juu, BASI HAO WOTE WAJUE KWA UHAKIKA KUWA WAMEKWISHA IBIPU SHERIA YA KIMATAIFA na hivyo wamejihakikishia NAMBA ZAO JELA.
 
Waendelee na mipango yao hiyo ya kuchafua nchi, lakini wakae wakijua kuwa iwapo tome moja la damu ya mtanzania itamwagika kwa ajili ya wao kuingia madarakani, hakika, damu hiyo itawalilia toka juu

I don't understand the guys at all. Kwanini madaraka wanafanya kama ni mali yao na kuwasahau kabisa watanzania? Halafu JK na Makamba eti ndio wako mstari wa mbele kukemea watu wanaotaka kuleta machafuko! Unafiki wa aina gani hii jamani kwa hawa viongozi wetu???
Hawa wakina Shamte wanafanya haya kwa niaba ya nani? Nani kawaambia udini ndio utampeleka ikulu raisi anayekuja? Nasikitika kuona kuwa those at the helm of this country have started loosing their mind because of tough election campaign!
 
Natamani angepata huu ushauri,sijui kama mitaa hii anafika jamani wadau jaribuni kumfikishia kwenye viwanja vyake
 
Mimi ni mmoja wa wachaga waliotishika toka mwanzo juu ya kauli mbalimbali za uchochezi dhidi yetu. Na kama nitapona hili sidhani kama dini nitapona kwani ni mkatoliki wa kikatoliki hasa.
Inaniuma kwani mke wangu ni Msukuma na wiki iliyopita ilibidi nimsafirishe kwenda kwao na watoto hadi uchaguzi upite kwani sijui kama ndugu zangu watamuacha likitokea lolote (Mungu apishe mbali). Ilibidi niondoke Mwanza kabla jirani zao hawajanigundua.
Inaumiza kukosa amani nyumbani,vipi ndugu zangu walioko mikoani hasa huko kwa Wakwere?
 
Kaka Solo, mie wa kule milimani, lakini ondoa HOFU, tumweke Mungu mbele na kutimiza majukumu yetu kusimama imara na kupiga kura sahihi siku ya uchaguzi, kulinda kura na kuwa tayari kumpokea rais wetu mpya baada ya uchaguzi tarehe 31 Oktoba. Hakuna kulalama na kulala usingizi tusubirie Mungu atume Malaika wake aje atusaidie kutenda bila ya sisi kujishughulisha. Tukapige kura ya mabadiliko. Hakuna cha ukabila wala udini, wala silaha au jeshi litakaloweza kuzuia mabadiliko yajayo kwa Tanzania. LAANA inayoikumba CCM na Kikwete kwa sasa hauzuiliki. Tutakumbuka kuwa hata Nyerere day wameikimbia kutokana na kusutwa mioyo yao, na badala yake waeenda kuitumia siku hiyo rasmi kuzima mwenge kisanii kumbe kumsaidia JK kukampeni ktk jimbo ja Zitto Kabwe...ila HAKUNA KITU, its nothingness indeed! Nyerere anatuombea naye, nchi itapata kiongozi makini kwa amani na utulivu. Itabadilika Oktoba 31 hadi Nov 4, Tutakuwa na Rais wetu Mpya, Mteule Dr Slaa!
 
Inasikitisha sana,...........HILI SIYO LA KUACHWA LIENDELEE HATA KIDOGO hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa!
 
Kinga ya Urais labda kwa mahakama za Tanzania ikiwa mambo yatabaki kama yalivyo, LAKINI nakuambia kinga chovu kama hizo hazipo kwenye mahakama za kimataifa. MILOSEVIC, KARADZIC, MILUTINOVIC wote WAKIWA MARAIS wa Jamhuri ya Kisoshalist ya YUGOSLAVIA ya zamani WALINYEA na mmojawao anaendelea KUNYEA ndoo kule Uholanzi kwenye mahakama za uhalifu wa kivita. Pia ikumbukwe, kuwa WAZIRI MKUU wa zamani wa RWANDA wakati wa GENOCIDE Mh. JEAN KAMBANDA alinyea ndoo kwenye mahakama ya mauaji ya kimbari ya pale ARUSHA, na kwa sababu alipatikana na hatia na KUFUNGWA MAISHA, ataendelea kunyea ndoo ile hadi mwisho wa maisha yake. CHARLES TAYLOR wa LIBERIA naye kama kawa....

Hao WOTE ( Rashid SHAMTE, Januari MAKAMBA, MTANDAO, NA WALIOMTUMA) wanaojenga uchochezi kwa MANENO na MATENDO yao wajue kitu kimoja cha msingi -MANENO na MATENDO yao yanaacha nyuma yao MTIRIRIKO wa USHAHIDI DHIDI yao, na Jumuiya ya kimataifa kupitia INTERNATIONAL CRIMINAL JUSTICE SYSTEMS( ijapoonekana kuwa kimya) inafuatilia mwenendo wa mambo yalivyo hapa Tanzania, na ENDAPO amani ya Tanzania itatoweka katika uchaguzi wa mwaka huu kwa msingi nilioutaja hapo juu, BASI HAO WOTE WAJUE KWA UHAKIKA KUWA WAMEKWISHA IBIPU SHERIA YA KIMATAIFA na hivyo wamejihakikishia NAMBA ZAO JELA.
LOGARITHM umenena kina January watacheka leo na kudharau lakini kesho si mbali wamesha weka doa kimataifa wako monitored kwa sababu wamehusisha nchi ya nje (Finiland) ukizingatia umri wao ni mdogo bado wana safari ndefu waombe tanzania iendelee kama ilivyo endapo kutatokea la kutokea they will be answerable.
 
Congratulation for those who took part to uncover the person involved to smear such hateful text messages
 
Hii imefika mbali sana. Hatuwezi kuangalia na kushabikia kina Shamte waiharibu nchi yetu na sisi tuangalie tu. Hivi hakuna uwezekano wa kumkamata huyo mtu na kumchukulia hatua za kisheria? Naamini kuwa kama kuna kipengele kinachoweza kutumika basi huyu jamaa mwisho wake umefika. Watumike wataalamu kuliangalia hili jambo na kuprove kuwa hizi sms zimetoka kwa Shamte na wakomeshwe vizuri.
 
Aliyehamisha hii thread toka kwenye jukwaa la uchaguzi ana lake jambo.
Hii forum muda mwingine inaudhi hadi basi
 
Mimi ni mmoja wa wachaga waliotishika toka mwanzo juu ya kauli mbalimbali za uchochezi dhidi yetu. Na kama nitapona hili sidhani kama dini nitapona kwani ni mkatoliki wa kikatoliki hasa.
Inaniuma kwani mke wangu ni Msukuma na wiki iliyopita ilibidi nimsafirishe kwenda kwao na watoto hadi uchaguzi upite kwani sijui kama ndugu zangu watamuacha likitokea lolote (Mungu apishe mbali). Ilibidi niondoke Mwanza kabla jirani zao hawajanigundua.
Inaumiza kukosa amani nyumbani,vipi ndugu zangu walioko mikoani hasa huko kwa Wakwere?
Isaac ni kweli mambo yameshafikia huko?Ina maana tensions na chuki za kikabila ziko that high?Wahindi na vibaraka wao lazima watakuwa wanafurahia sana tu
 
Back
Top Bottom