Aliyesambaza meseji za kumkashifu Slaa ni....

Hivi Mkurugenzi wa TCRA anasubiri nini kujiuzulu!!!!! Ni aibu kubwa kushindwa kukamata wanaofanya upuuzi huo. Pamoja na propaganda zote hizo watanzania wengi hivi sasa wamepevuka. Sisiem haina chake mwaka huu na Dunia itashangaa.
 
CCM wana tatizo la kutoelewa madhara ya kufikiri, kuishi na kutenda ki-analogue katika digital era. Wanaumbuka vibaya sasa

hapo kwenye nyekundu naomba niweke sawa hili, sina interest wala sio mwanachama wa CCM, lakini ni ukweli usiopingika kuwa cCm hawahusiki na hili, Kampeni za JK zipo tofauti kabisa na chama, yeye amefungua ofisi yake sehemu nyingine kabisa na hapo ndipo anapoendesha kampeni zake bila kushirikisha chama zake, KINANA, TAMBWE HIZA, MAKAMBA, MSEKWA, NA VIONGOZI WOTE MAARUFU WA CCM WAKO PEMBENI WAKIMWANGALIA jK AKIPAMBANA KIVYAKE KUTOKEA UPANGA OFISI AMBAYO SIO OFISI RASMI YA CCM
 
Baada ya kampuni ya simu za mikononi VODACOM kuanza kuchezea namba yangu ambayo nimekuwa nikiitumia kwa zaidi ya miaka 10 sasa kuanzia leo sintoitumia tena namba hiyo.

Wamechezea namba yangu kwa kumpa na kumruhusu ndugu Rashid Shamte kunitumia ujumbe nisioutarajia mnamo tarehe 9/10 saa 8.25 usiku mwaka huu.

Usumbufu nilioupata na nitakaoupata ni pamoja na kuwajulisha ndugu na jamaa zangu wote niliowapa namba hiyo kuhusu uamuzi wangu wa kubadili namba ya simu.

Naitakia VODACOM na wateja wake wote biashara njema.

Asanteni.
 
6 telecoms T ltd inaonekana ni kampuni kubwa tu Kulingana na taarifa zao kwenye website yao invyojieleza Six Telecoms-Home Records za TZNIC zinaonesha kuwa hawa jamaa ndio wana host domain ya kikwete2010.co.tz. Kwa kuwa hawa jamaa biashara yao ni telecoms haikosi wana access ya customer database za mobile networks wa Tanzania. kwenda kwenye Internet wanaunganishwa na I-way Africa. ni kweli hii kampuni iko pale barclays house ohio street floor ya 5. Kwa kweli inasikitisha kampuni kama hii kuruhusu umafia mkubwa kama huo kwa watanzania kufanyika kupitia wao.

Ama kweli fedha ni chanzo cha maovu duniani.
 
Hili ni thibitisho lingine kwamba Tanzania ya jana siyo ya leo, na kama mtu anafikiri mtu aliyesoma vizuri lazima awe ameenda Havard tu anakosea. Maana Havard watoto wa wakulima hawaiwezi ada ya kusoma huko. Ila wakiamua kusoma wanasoma na kuelewa haswaa wanachosoma.
Jamani, haya mambo ya udini na ukabila na siasa za chuki ndio muhimili wa wana mtandao. Wameingia kwenye madaraka kwa mizwengwe na wanaishi madarakani kwa mizengwe na wanataka kurudi madarakani kwa mizengwe pia. Naona wanasahau kuwa wanaweza kuiharibu nchi kama wanaendelea kubomoa bomoa mihimili mikubwa ya utulivu na amani ya Tanzania
 
Hongera Kikwete na wanao kwa kutengeneza meseji za kumchafua Dr. Slaa
Hongera Makamba na Kinana kwa kumchafua Dr. Slaa kuhusu ndoa yake
HOngera Akwilombe kwa kueleza Uchaga wa CHADEMA
Hongera CCM kwa kuelezea Ukatoliki wa Dr. Slaa na CHADEMA
Hongera CCM kwa kuelezea Uislamu wa CUF

Sasa tuazishieni ubeti wa Yale mtakayowafanyia mafisadi walioipora nchi yetu

Halafu ufuate ubeti wa namna rasilimali za nchi yetu zitakavyowafaidisha wananchi wote kwa ujumla.

Mwisho mfunge na ule ubeti wa namna mtakavyolinda amani ya kweli bila kutanguliza vitisho na propaganda
 
Nani anasema CCM Mgombea Urasi wa CCM hana mkono katika hizi meseji.... Ushahidi wa kimazingira huu hapa: Uki-fatilia domain 6telecoms.co.tz, iliyotumika utaona wazi share the name IP ya Kikwete2010co.tz na JK web site yake na nyingine za mafisadi wa papa ziko hosted nao.
Angalia maandishi mekundu!
"
Kikwete2010.co.tz is a domain controlled by two name servers at co.tz. Both are on different IP networks. The name server kikwete2010.co.tz stated in SOA record is not in the list of name servers. Incoming mail for kikwete2010.co.tz is handled by two mail servers also at co.tz. Both are on different IP networks. kikwete2010.co.tz has one IP number (41.77.226.253).
212.233.84.in-addr.arpa, 229.77.41.in-addr.arpa, 228.77.41.in-addr.arpa and 227.77.41.in-addr.arpa share name servers with this domain. 6telecoms.co.tz share mail servers with this domain.
Ndio maana wanahamia vijijini, eti ndo ngome yao!! Mjini watu wameenda shule; hao waliofikiri IT wanajua wenyewe wamevuliwa vyupi hadharani; vijijini nako wameamka, ngome zimebaki kwa waganga wa kienyeji na wapiga ramli!!
 
Nami nimehamasika. Sio kwa huyo jamaa tu hata CCM wananitumia mamesege ya k****nge. najitoa leo rasmi . Bye bye
 
Mimi nimesema, huyo jamaa wa TCRA kwa nini aendelee kukalia ofisi wakati siyo smart?
Let him stp down and smart people take over bwana.
hakuna ubabaishaji kwenye masuala nyeti kama haya. Achomoke fasta, kama hataki asubiri tutadeal naye mmoja baada ya mwingine baada ya kampeni.

hakuna maana kuendelea kula kodi zetu bila kuwa na uwajibikaji katika ofisi nyeti kama hiyo wakuu.
 
May be this needs to go further to connect the culpt with CCM and rtake nexessary steps. Because I believe that he is not doing ot for himself but unde the auspius of CCM.
 
pole sana, ni ujumbe upi huo, maana inawezekana ni wengi tumetumiwa ila hatujui
 
hapo kwenye nyekundu naomba niweke sawa hili, sina interest wala sio mwanachama wa CCM, lakini ni ukweli usiopingika kuwa cCm hawahusiki na hili, Kampeni za JK zipo tofauti kabisa na chama, yeye amefungua ofisi yake sehemu nyingine kabisa na hapo ndipo anapoendesha kampeni zake bila kushirikisha chama zake, KINANA, TAMBWE HIZA, MAKAMBA, MSEKWA, NA VIONGOZI WOTE MAARUFU WA CCM WAKO PEMBENI WAKIMWANGALIA jK AKIPAMBANA KIVYAKE KUTOKEA UPANGA OFISI AMBAYO SIO OFISI RASMI YA CCM

Kituko wewe ni kituko kwelikweli. Unawezaje kumtofautisha Kikwete na CCM? Kikwete anagombea urais kupitia chama gani? Wananchi wa Tanzania hawamtaki Kikwete na CCM yote. Utetezi wako ni kituko.
 
Okay Guys,

Motto ya JF ni a place where we dare to talk openly.
Leo nitasukuma hii bahasha (push the envelop) mbali zaidi kwenye hii issue ya text messages zinazotumwa kwenye mobile phones Tanzania.

Kama tujuavyo, hizi texts ni za kichochezi na zenye nia ya kuamsha chuki dhidi ya kabila moja kubwa Tanzania (la wachagga) na dhehebu moja kubwa Tanzania (la wakatoliki). Hizi texts kama zikiachwa tu hivi bila kukemewa kwa lugha ya ukali kabisa, zitapelekea genocide. Zitapelekea mauaji ya kutisha kama yaliyotokea Rwanda na Burundi.

Kwa mujibu wa interview aliyofanya na mbunge wa singida Mohamed Dewj (credit kwa member wa JF- Dingswayo aliyevuta hii news kutoka maktaba), January Makamba alisema yafuatayo:

Yupo pia rafiki yangu Rashid Shamte na vijana wenzake pale Push Mobile – mambo wanayofanya kwenye telecoms sector si madogo. Wapo vijana wengi hapa mjini, ...

Hii interview (credit again kwa Dingswayo) ambayo originally iliwekwa na MO kwenye blog yake, kwa sasa ipo kwenye blog ya u-turn ya mange (fuata link hapa chini kama unataka kusoma interview yote):

JANUARY MAKAMBA AHOJIWA NA MBUNGE MH.MOHAMMED DEWJI

Ukisoma thread ya member mwenzetu wa JF (macho mdiliko) ambayo ipo hapa kwenye jukwaa la uchaguzi, utaona habari toka kwa gazeti la guardian ambayo imemtaja Rashid Shamte kama kinara na mhusika mkuu wa hizi texts za kichochezi zinazotumwa Tanzania nzima. Napendekeza sana wewe msomaji ufuatilie hiyo thread ya macho mdiliko. Hakikisha pia kuwa umesoma post ya member wa JF (aitwaye Zed) ambaye ameweka link kati ya Rashid Shamte na website ya Kikwete2010.

Link ya hiyo thread ni hii:

https://www.jamiiforums.com/uchagu...liyesambaza-meseji-za-kumkashifu-slaa-ni.html

Swali ninalojiuliza hapa ni kuwa, urafiki wa January Makamba na Rashid Shamte unaanzia na kuishia wapi?

January Makamba amekuwa mfanyakazi wa ikulu ya Kikwete for a while kabla ya kuamua kugombea ubunge. January Makamba ni mhusika katika kampeni ya Kikwete (unakumbuka picha za bumbuli?). Hizi texts message zinatumika kuwachafua wapinzani wa Kikwete katika uchaguzi huu. Kuna uhusiano wa kiaina kati ya hizi texts na speeches za Kikwete kwenye kampeni.

Swali la nyongeza, January Makamba na Rashid Shamte wanahusika kwa asilimia ngapi katika hii kampeni ya kutisha dhidi ya kabila moja na dini moja iliyoanzishwa? Wanategemea kupata nini iwapo kutakuwa na vita kati ya makabila mengine dhidi ya wachagga? wanategemea kupata nini ikitokea vita ya kidini Tanzania?

Ombi kwa mods wa JF, hii thread ina nia moja tu - kukemea na kupinga vikali genocide in making inayoendelea Tanzania. Sikutegemea hata siku moja kuwa nitasema hili hapa JF but I will say it. Mimi ni mchagga na ni mkatoliki. Familia yangu imeingiwa na woga sana baada ya kusoma hizi texts zenye maneno ya kutisha dhidi ya kabila langu na dhehebu langu la dini.

Naomba sana haya maneno yakomeshwe mara moja. Naomba hii thread iachwe hapa kwenye jukwaa hili ili itumike kutuma message kwa January Makamba, Rashid Shamte, na vijana wa IT wa kampeni ya JK kuwa haya mambo wanayofanya si mazuri na inabidi yaachwe mara moja.

Wenu katika wasiwasi na hofu kuu,

Solomon David.
 
May be this needs to go further to connect the culpt with CCM and rtake nexessary steps. Because I believe that he is not doing ot for himself but unde the auspius of CCM.

Hiki kilichofanyika ni sawa na uhaini kwa watanzania. Chadema lichulieni suala hili ki-sheria, kimataifa, na pia iwe katika kampeni zilizosalia. Watanzania pia tuzidi kuwaelimisha ndugu zetu popote walipo uhaini unaofanywa na CCM dhidi ya watanzania
 
Duu, hii nimeiona ONLINE:

--Rashid Shamte, CEO, Six Telecoms Company Limited (TZ)

Kwenye ile makala ya DEWJI akicheza ngoma, niliandika wazi kuwa tutawachukia Wahindi na Waarabu bure tu ila wabaya wetu ni hawa Mipingo wenzetu. Junius mtani wangu, utakuwa unakumbuka hayo maneno ingawa ulicheka, hilo halikuwa jambo la kucheka ila kulia.

Nazidi kuamini kuwa Serial Killer, siku zote huuwa watu wa RANGI ZAO.

Uchaguzi ukiisha, wote hao akina January Makamba et el wana kesi ya kujibu au kusaidia upande wa mahakama. Hata wakikwepa mwaka huu, mwaka 2015 tunao na kibaya zaidi watakuta mwenzao ana Kinga ya Urais ila wao watakuwa na hali mbaya sana.

Nyie Wajinga, someni alama za nyakati na mjitakase maana mna bahati ya kujua SAA NA WAKATI.
 
Mimi nilifikiri mchaga ndiye angekamatwa maana tumeaminishwa ndiyo Wabaguzi. Nina hakika Malaria Sugu hajaiona hii post.
 
Nina mshauri Dr. Slaa katika kila mikutano ya kampeni atakayokuwa akifanya awaulize halaiki swali moja muhimu: "Ni wangapi wamepata meseji za Rashid Shamte (na Kikwete)? Kama watakuwepo kwenye mkutano husika, basi atumie fursa hiyo kueleza upotoshaji ulio kweye ujumbe huo na athari zake kwa Watanzania kama ulivyoelezwa kwenye aya mbili za mwisho za The Guardian on Sunday ya Tarehe 17 October 2010.

Wasaidizi wake wa Karibu, Wagombea Ubunde na Udiwani wa Chadema, Watanzania wenye upeo na tunaotaka mabadiliko pia tufanye hivyo hivyo.

Walisambaza ujumbe huo kwa siku mbili tu. Tunaweza kuuzima vizuri sana kwa wiki 2 zilizobaki.

Mabadiliko Lazima.

Dr. Slaa For Life!!!
 
we need changes,tusiwe wapuuzi na wapumbavu,kenya kanu iliwazingua wakaitema,kwann sisi jmn tusiiteme? wanatuletea maisha magumu kila kona.rostam mwizi kikwete alipofika jimboni kwake igunga,akaawambia wananchi wamchague,inamaana aje aendelee kutuibia? tumchague slaa awafilisi wote mali walizoiba. dr. slaa is the choice for better tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom