Aliyeongoza Kidato cha Nne ni Yatima. "Watanzania Tumpe Pongeza Dada Yetu"

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
116
Wednesday, 26 January 2011 20:22

Mussa Juma, Arusha
MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha mne kitaifa mwaka 2010, Lucylight Mallya (18), amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote walifariki dunia miaka minne iliyopita.

Akizungumza katika mahojiano maalum, akiwa nyumbani kwa baba yake mkubwa kijiji cha Nguruma wilayani Arumeru, binti huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ya Marian, iliyoko Bagamoyo, mkoani Pwani alisema anamshukuru Mungu, walimu na walezi wake kwa kumwezesha kufaulu.

"Sikutegemea kuwa wa kwanza namshukuru sana Mungu, walimu, walezi wangu hasa baba mkubwa na mama na wote walionifikisha hapa ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenzangu....," alisema Lucylight.

Lucylighty ambaye ni kwanza kati ya watoto, wanne walioachwa na marehemu wazazi walofariki dunia mwaka 2006 na (2007), alisema malengo yake ni kuwa daktari.

Binti huyo alisema wakati anafanya mtihani huo, somo aliloona gumu lilikuwa ni fizikia, lakini anamshukuru Mungu kuwa amefaulu vizuri na kuwa wa kwanza hapa nchini.

"Mimi nilikuwa napenda sana Kemia, Bailojia na Fizikia na nilikuwa nimejiandaa sana hivyo namshukuru Mungu kunisaidia kutimiza ndoto zangu," alisema Lucylighty.

Baba Mkubwa wa Lucy ambaye ndiye anamlea, Dominick Mallya alisema anashukuru Mungu kwa binti yake huyo kuongoza kitaifa.

Hata hivyo, Mallya alisema binti huyo amesoma katika mazingira magumu kwasababu hakuwa na fedha za kutosha hivyo alimwomba mmiliki wa shule hiyo, Father Valentine Bayo kumtafutia mfadhili.

"Mamshukuru Father Bayo kwani tangu mtoto huyu akiwa kidato cha pili hadi kumaliza kidato cha nne alikuwa analipiwa na wafadhili,"alisema Mallya.

Hata hivyo, aliomba wafadhili wa kumsaidia, ili aweze kuendelea ya masomo ya kidato cha tano hadi sita na chuo kikuu kwasababu yeye (Mallya) hanafedha za kutosha kuwasomesha watoto wote alionao.

"Baba yake Lucy ambaye ni mdogo wangu alifariki dunia mwaka 2006 na mkewe alifariki mwaka 2007, waliacha watoto wanne na mimi nina watoto watano hivyo tunashindwa kumudu gharama za kuwasomesha," alifahmisha Mallya na kuongeza:

"Tungependa kupata tena ufadhili wa Lucylight ili aweze kuendelea na masomo ya juu katika shule ambayo alikuwa akisoma".

Lucylight alizaliwa Jijini Dar es Salaam, miaka 18 iliyopita alisoma Shule ya Msingi St Mary's Tabata na baada ya alihitimu la saba mwaka 2006 alichaguliwa kwenda Shulea ya Sekondari ta Wasichana Tabora lakini aliamua kwenda Marian Girls alikohitimu kidato cha nne mwaka jana.

Taarifa za maendeleo yake zinaonyesha kuwa akiwa kidato cha kwanza alishika nafasi ya tatu, lakini kuanzia kidato cha pili hadi cha nne alikuwa akishika nafasi ya kwanza.
lucymallya.jpg

- Kitu muhimu sana katika hii article ni kwamba huyu msichana ameweza kufanya vizuri sana katika masomo na sisi kama Taifa tujitahidi kuwaweka vijana kama hawa mbele ya Taifa wajulikane na kusaidiwa kifedha bila kupelekwa shule za serikali ambazo hazina walimu. Hii imetokea kwa familia nyingi Tanzania na vipaji kama hivi Kitaifa vimekufa au vinatoweka bure. Nchi nyingi wanainvest sana kwenye elimu na kuna "Honor Programs nyingi za Kuhakikisha Wanafunzi kama Hawa Wanajaliwa"
-Je Kikwete na Pinda wanajua hili? Wamesikia au wanaendelea kusukuma kulipa Dowans?
-Wizara ina mipango ya kusaidia Wanafunzi kama hawa?

"Let's Invest in the Future of Tanzania not the Few Theives"
 
nawapenda sana watoto kama hawa niwajibu wetu kuwasaidia,iwekwe account ambayo tuweze kuchangia ili mtoto wetu huyu akamilishe ndoto zake atakua na mchango mkubwa kwa tanganyika ya badae.
 
Naomba tutafute namna na kama Jamii forums tumsaidie naamini siku msaada ukipelekwa kama Jamii forums she will know kuna watu wenye vipaji wengine huku walio tayari kusaidia watu. Tukitumia MPESA account/NMB account itakuwa vema. pls make this be a motto huyu hatakiwi kupata shida jamani ameonyesha njia
 
lucymallya.jpg

Mungu ni Baba wa wajane na Yatima. Ameitimiza ahadi yake kwako, Ombi langu ni hili, Ongeza juhudi heshima na umakini katika masomo yako. Sala zako zisikome bali zisidi. Achana na Ma-boyfriend watakuchafulia nafasi yako.
Mungu akupe nguvu ya kushinda Vishawishi vya Ujana. Pia kumbuka janga la ukimwi lipo.
 
nawapenda sana watoto kama hawa niwajibu wetu kuwasaidia,iwekwe account ambayo tuweze kuchangia ili mtoto wetu huyu akamilishe ndoto zake atakua na mchango mkubwa kwa tanganyika ya badae.

Tayari amesha kuwa celebrity utakuta mibaba inanyatia inataka kumpiga mimba kwa kigezo nitakusaidia ada.

Ole wenu tuone ametepeta akashindwa kwenda form V lazima tutaandamana
 
Wednesday, 26 January 2011 20:22

Mussa Juma, Arusha
MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha mne kitaifa mwaka 2010, Lucylight Mallya (18), ...................................................

.................................. binti huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ya Marian, iliyoko Bagamoyo, mkoani Pwani ..................................

Hebu tuwe wawazi!

Sijui ni kwa nini neno Yatima limepewa nafasi kubwa ktk kuelezea ushindi wa binti huyu.
Angekuwa shule ya kata ningeona ni maajabu lakini hakuna uhusiano kati ya ushindi wake na kuwa Yatima. Shule aliyosoma ni inajulikana. Basi!

Lakini nina wasi wasi na shule hii ambayo sasa hivi naisikia mara ya tatu ikitoa mwanafunzi bora mfululizo. Marian ni shule isiyo kuwa na waalimu wazoefu ktk ufundishaji, ukilinganisha na shule zingine kiasi cha kuleta tofauti hiyo.

Hivi kweli hawa ni bora? Wanaweza kuwa bora lakini kiasi tunachoambiwa. Miaka ya nyuma imetoa wanafunzi bora lakini huko mbele hawajasikika tena! Siyo form 6 wala vyuo vikuu na baadhi tunawafahamu. Hiyo shule kuna namna.

Siri ya 'father' huyo ipo. Former mwalimu wa shule hiyo alidokeza kwamba kikifika kipindi cha mitihani kuna waalimu hupewa 'tasks' za kuhakikisha mitihani ya masomo fulani yanapatikana. Wanafunzi uliwauliza hawajui kama walionyeshwa mitihani lakini watakwambia sehemu kubwa ya maswali ya final tuliyapitia na mwalimu darasani.
 
Hongera sana Lucylight Mallya!

Huu ni mwanzo, safari ni ndefu mbele, ongeza bidii....usibweteke, usishawishike wala kukata tamaa.

MUNGU kubariki, akulinde.
 
Hebu tuwe wawazi!

Sijui ni kwa nini neno Yatima limepewa nafasi kubwa ktk kuelezea ushindi wa binti huyu.
Angekuwa shule ya kata ningeona ni maajabu lakini hakuna uhusiano kati ya ushindi wake na kuwa Yatima. Shule aliyosoma ni inajulikana. Basi!

Lakini nina wasi wasi na shule hii ambayo sasa hivi naisikia mara ya tatu ikitoa mwanafunzi bora mfululizo. Marian ni shule isiyo kuwa na waalimu wazoefu ktk ufundishaji, ukilinganisha na shule zingine kiasi cha kuleta tofauti hiyo.

Hivi kweli hawa ni bora? Wanaweza kuwa bora lakini kiasi tunachoambiwa. Miaka ya nyuma imetoa wanafunzi bora lakini huko mbele hawajasikika tena! Siyo form 6 wala vyuo vikuu na baadhi tunawafahamu. Hiyo shule kuna namna.

Siri ya 'father' huyo ipo. Former mwalimu wa shule hiyo alidokeza kwamba kikifika kipindi cha mitihani kuna waalimu hupewa 'tasks' za kuhakikisha mitihani ya masomo fulani yanapatikana. Wanafunzi uliwauliza hawajui kama walionyeshwa mitihani lakini watakwambia sehemu kubwa ya maswali ya final tuliyapitia na mwalimu darasani.

duuuuh!
 
Hongera mdada, maana wengine wangechukulia uyatima kama excuse ya kutofanya bidii.
 
nawapenda sana watoto kama hawa niwajibu wetu kuwasaidia,iwekwe account ambayo tuweze kuchangia ili mtoto wetu huyu akamilishe ndoto zake atakua na mchango mkubwa kwa tanganyika ya badae.

Hapo aliposimama ni kwao. Sio kila yatima ni maskini.

Hata aliyekuwa wa tatu S. Mutoka (Shule ya Bablo-Johson) naye ni yatima . Binti huyu wa tatu ameondoka juzi kwenda Sweden, kama zawadi kwa performance yake nzuri shuleni kwake. Kabinti aka ni Kahaya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom