Aliyemuibia Malima ana umbo la kitutsi; Juu mwembamba chini mnene

'kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali'.

hata malima ni mwizi tu kwanini mali zote hizo.
Mimi hapa sielewi yani waziri mzima alikuwa anaanzisha kundi lake la uhaini kaamua kwenda mstuni??mbona alikuwa na asset nyingi sana kwa morogoro ina maana Bungeni uhamisha nyumba yake dodoma!!Kuna zaidi ya swali hapa!
 
hii natosha malima ang'atuke uongozi haihitaji tena ushahidi mpya
 
Tuichambue hii habari na tukio lenyewe kama ifuatavyo:

1 - Inaonekana mwizi alikuwa ndani ya chumba cha huyu fidhuli na si nje.

2 - Kutokana na maelezo ni kwamba nyayo zilionekana ambazo inaelekea ni za mtu mmoja; lakini je, ina maana nje ya chumba cha bei yote hiyo mwenye hoteli ameshindwa kusakafia na kuacha mchanga na vumbi mpaka nyayo zionekane? Kama kuna sakafu, je, inawezekana miguu ya huyo mwizi ilikuwa imelowa mpaka aache alama za nyayo?

3 - Idadi ya vitu vilivyoibiwa ni kubwa kulinganisha na uwezo wa mtu mmoja kuvibeba kwa mara moja; je, huyo mwizi alirudia hivyo vitu, na kama alirudia ni wapi alikoegesha gari au wenzie walijificha umbali gani kumuwezesha kurudia vitu kama upo uwezekano kuwa alirudia?

4 - Miongoni mwa vilivyoibiwa ni mabegi ya nguo; je, mwanamke mwizi katika hali ya kawaida atahitaji kubeba mabegi ya nguo za kiume ambazo si mpya?

5 - Huyo mwanamke kwenye Defender inasemekana amekutwa na simu tatu na laptop, ingawa habari haisemi ni laptop zote au moja. Je, katika hali ya kawaida, inawezekana kweli hao wanaume wote waliokamatwa waondoke na vitu vingine kama hela, kadi za benki, pete na nguo halafu wamuachie mwizi mwenzao wa kike simu za bei mbaya na laptop?

6 - Je, nyayo zilizoonekana zimepimwa na kufanana na za yeyote kati ya hao waliokamatwa?

7 - Ulinzi katika hoteli hiyo ukoje mpaka vitu vyote hivyo viibiwe, dirisha livunjwe, mtu akimbie na kuacha nyayo - yote haya bila hata walinzi kusikia chochote?

8 - Upo pia uwezekano kwamba aliyekuwepo mle chumbani na Malima ni mwanaume ndiyo maana pengine mabegi yake ya nguo yaliibiwa. Kusema kuwa Malima ana mke hakumaanishi yale mambo ya nanihii hayawezekani, maana wapo waliooa ili kujificha wakati kumbe huwa wanashughulikiwa na wanaume wenzao.

Haya ni ya msingi kuzingatia.
Mkuu hapo namba 8 mmh!panahitaji tafakari ya kina sana
 
malaya tu kamzidi akili huyu penda penda, kwani vyote hivyo anatembea navyo amekua mwana CIA?????????
kilaza tu yule au kwa vile hvyo vitu hajavipata kwa jasho la chumvi?????????
 
Hivi kuna Blackberry inauzwa milioni 5.5? Na kama ipo japo sijui, ni ulimbukeni au laa? ina nini cha ziada kilichomfanya Malima kuwa nayo. Kumbe kwa hali hii kulilia posho bungeni hakutakwisha kamwe
 
malaya wana vinywa vilivyojaa asali, Malima alikosa namna ya kumuepuka shangazi uyu.
Nadhani ni sifa ya kuwa kila kionekanacho chema hawezi kikosa mbele ya wapambe...kajamaa kalivyo kafupi katakuwa na taabu nyingi. km kaliweza sema kuwa kalitaka jamaa aondoke ktk chumba chake alichokizoea.Si ajabu pia na huyo demu kalisema ni wake na wengine wale kona.
 
Malima naye bana! Amenyonya matiti weeeeeeeeeeeeeeee bila kujua yamepakwa dawa ya usingizi!
Ona sasa yaliyomkuta!
Kikwete anasubiri nini kumfukuza huyu mzinzi mwenzangu?
 
alijichimbia ili afanye ngo no yakamkuta,
si amezee tu.

tatizo la kupenda kunyonya vichuchu na vile visembe ulaya wanavitegeshea pale pale kwenye vichwa we ukinyonya unajisikia uko kwenye ilee nchi ya ahadi na kausingizi hapo hapo...
 
huyu waziri ni mse........................ network seacrh........................
 
Mimi sitaki kujua aliibiwaje wala thamani ya vitu alivyoibiwa au mwizi ni nani. Ninachotaka kujua Laptop tatu za kazi gani? Wataalamu wa magonjwa ya akili na wale wa IT hebu tujuzeni ni ugonjwa wa aina gani anaugua huyu jamaa hadi kumiliki Laptop tatu kwa wakati mmoja!!
 
Tuichambue hii habari na tukio lenyewe kama ifuatavyo:

1 - Inaonekana mwizi alikuwa ndani ya chumba cha huyu fidhuli na si nje.

2 - Kutokana na maelezo ni kwamba nyayo zilionekana ambazo inaelekea ni za mtu mmoja; lakini je, ina maana nje ya chumba cha bei yote hiyo mwenye hoteli ameshindwa kusakafia na kuacha mchanga na vumbi mpaka nyayo zionekane? Kama kuna sakafu, je, inawezekana miguu ya huyo mwizi ilikuwa imelowa mpaka aache alama za nyayo?

3 - Idadi ya vitu vilivyoibiwa ni kubwa kulinganisha na uwezo wa mtu mmoja kuvibeba kwa mara moja; je, huyo mwizi alirudia hivyo vitu, na kama alirudia ni wapi alikoegesha gari au wenzie walijificha umbali gani kumuwezesha kurudia vitu kama upo uwezekano kuwa alirudia?

4 - Miongoni mwa vilivyoibiwa ni mabegi ya nguo; je, mwanamke mwizi katika hali ya kawaida atahitaji kubeba mabegi ya nguo za kiume ambazo si mpya?

5 - Huyo mwanamke kwenye Defender inasemekana amekutwa na simu tatu na laptop, ingawa habari haisemi ni laptop zote au moja. Je, katika hali ya kawaida, inawezekana kweli hao wanaume wote waliokamatwa waondoke na vitu vingine kama hela, kadi za benki, pete na nguo halafu wamuachie mwizi mwenzao wa kike simu za bei mbaya na laptop?

6 - Je, nyayo zilizoonekana zimepimwa na kufanana na za yeyote kati ya hao waliokamatwa?

7 - Ulinzi katika hoteli hiyo ukoje mpaka vitu vyote hivyo viibiwe, dirisha livunjwe, mtu akimbie na kuacha nyayo - yote haya bila hata walinzi kusikia chochote?

8 - Upo pia uwezekano kwamba aliyekuwepo mle chumbani na Malima ni mwanaume ndiyo maana pengine mabegi yake ya nguo yaliibiwa. Kusema kuwa Malima ana mke hakumaanishi yale mambo ya nanihii hayawezekani, maana wapo waliooa ili kujificha wakati kumbe huwa wanashughulikiwa na wanaume wenzao.

Haya ni ya msingi kuzingatia.

Namba 3 nimeipenda.Huyu waziri limbukeni sana.Safari kidogo tu unabeba makorokoro kibao,si ushamba huu.
 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro | Global Publishers

WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima (pichani) mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.

Hapa shigongo na Magazeti yako mmejaribu kuongea ukweli kuliko lile gazeti la Mwananchi jana liliudanganya umma

Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.

Alirejea wapi huyo mwanamke?

“Kuna jamaa yangu amewahi kuibiwa katika hoteli moja na mwanamke huyo tunayedhani kuwa kamuibia Waziri Malima. Inasemekana ana ‘funguo malaya’ na hata dawa ya usingizi.

Hana funguo malaya Bana huu ni uongo usiofichika ina maana hapo morogoro hotel zote rock za milango zinafanana? sema wanaume ndio huwa wanamshobokea halafu toto inaonekana linalipa, na kuhusu dawa ya usingizi huo ni uongo sema jimama huwa linatoa dozi ya nguvu mpaka mteja anazima:wink2:

“Siku aliyoibiwa jamaa yangu mwanamke huyo aliingia katika chumba chake akajifanya kuomba simu, baadaye jamaa yangu akajikuta amelala fofofo, akakombwa kila kitu. “Nadhani alitumia dawa ya usingizi, sasa sijui mazingira ya chumba na hoteli aliyolala naibu waziri yalikuwaje,” kilisema chanzo hicho.

Hapa kulikua na makubaliano maalumu baada ya jamaa kupiga mzigo na kushindwa gemu akaangusha na Jimama ikabidi lijisevie kila kitu, na hii ni style ya machangudoa wote wapo kikazi zaidi, nakumbuka kuna kipindi 2004 wakati nipo Azania SS nilienda Jolly Club night moja, kuna baharia wa kireno alipigwa Euro 4000 na malaya..

Mwandishi wetu alizungumza na mlinzi mmoja wa Hoteli ya Nashera na kumuuliza kama alimuona mwanamke yeyote siku hiyo ya tukio hotelini hapo ‘akimzengea’ waziri lakini akakataa kuzungumzia suala hilo.

Mlinzi hawezi akaongea chochote, si atapoteza kibarua chake

Aidha, Naibu Waziri Malima alipozungumza na gazeti hili alisema hamjui mtu aliyemuibia na hakuwahi ‘kuzengewa’ na mwanamke yeyote siku hiyo.

Malima hawezi kumtaja aliyemwibia ni aibu lakini inajulikana kabisa kua aliibiwa na Mwanamke
 
Tanzania ni zaidi ya uijavyo.Hii nchi kila kitu kinafanyika kiselakisela (bila kufuata professional husika), huyu anaongea hivi yule anaongea hivi..Tutafika kweli jamani? roho inaniuma kuona watu kama polisi ambao moja ya kazi zao ni kulinda usalama wa raia na mali zao wanakuwa chanzo cha kuficha uozo uliopo kwenye jamii hasa linapotokea jambo limemgusa mtu mkubwa ama mwenye pesa...iko siku wataumbuka na watoto wetu watawauliza nini maana ya kwenda shule??inaniuma sana,,,
 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro | Global Publishers

WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima (pichani) mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.

Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.

Habari zinasema, mwanamke huyo haikujulikana aliondokaje katika hoteli hiyo, hivyo watu kumlenga yeye kuwa ndiye mwizi baada ya habari za naibu waziri kuibiwa fedha na mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 kuzagaa.

Mpasha habari wetu mmoja amedai kuwa mwanamke huyo ambaye amekuwa akihusishwa na wizi pamoja na utapeli mbalimbali mkoani hapa, amekuwa akionekana katika baadhi ya hoteli kubwa.

“Kuna jamaa yangu amewahi kuibiwa katika hoteli moja na mwanamke huyo tunayedhani kuwa kamuibia Waziri Malima. Inasemekana ana ‘funguo malaya’ na hata dawa ya usingizi.

“Siku aliyoibiwa jamaa yangu mwanamke huyo aliingia katika chumba chake akajifanya kuomba simu, baadaye jamaa yangu akajikuta amelala fofofo, akakombwa kila kitu. “Nadhani alitumia dawa ya usingizi, sasa sijui mazingira ya chumba na hoteli aliyolala naibu waziri yalikuwaje,” kilisema chanzo hicho.

Wajihi wa mwanamke huyo ambaye inadaiwa ana kundi la uhalifu ambalo hudiriki kuvunja sehemu wanayodhani ina mali au fedha, ni mweupe, mrefu, ana umbo mithili ya wanawake wa Kitutsi, juu mwembamba, chini mnene na inasemekana hupendelea kutembelea pia jijini Dar es Salaam na Mwanza.

Mwandishi wetu alizungumza na mlinzi mmoja wa Hoteli ya Nashera na kumuuliza kama alimuona mwanamke yeyote siku hiyo ya tukio hotelini hapo ‘akimzengea’ waziri lakini akakataa kuzungumzia suala hilo.

Aidha, Naibu Waziri Malima alipozungumza na gazeti hili alisema hamjui mtu aliyemuibia na hakuwahi ‘kuzengewa’ na mwanamke yeyote siku hiyo.

ALIYEIBA ALIKUWA PEKUPEKU
Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani ambaye siku ya tukio alikuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa mkoa, alisema uchunguzi wao wa awali ulibaini kuwa aliyeiba hakuwa amevaa viatu, yaani alikuwa pekupeku.

“Nyayo za mtu huyo zilionekana nje ya chumba namba 125 alichokuwa amelala naibu waziri,” alisema Kamanda Selemani.

ALICHOSEMA RPC
Alipoulizwa juzi na gazeti hili juu ya changudoa huyo anayedaiwa kufanya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, (RPC) Adolfina Chialo alisema hajajua kama changudoa huyo anahusika lakini akakiri kuwa tayari watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

“Kuna vitu vya Naibu Waziri Malima vimepatikana isipokuwa fedha lakini tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Maneno Juma (25), Juma Athumani (23) ambao ni wakazi wa Chamwino, Kwa Mgulasi, Ramadhani Athumani (24) na Abdallah Hassan (25) wakazi wa Mafiga.

Kamanda alimtaja mwanamke Halima Ramadhani (37), mkazi wa Kichangani Morogoro ambaye alisema alikutwa na simu tatu na Kompyuta mpakato (Lap Top), mali za Naibu Waziri Malima.

MALI ALIZOIBIWA
“Tumefanikiwa kukamata mali za waziri kwa asilimia 90 nikimaanisha kwamba vitu vyote vimepatikana isipokuwa fedha,” alisema Kamanda Chialo bila kufafanua zaidi.

Malima alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kubembelezwa kwa saa tano, alitaja mali alizoibiwa na thamani yake katika mabano kuwa ni Kompyuta mpakato tatu aina ya Dell (Sh. Milioni 5.6), Digital Recoder mbili na head phone zake (Sh. Milioni 1), simu tatu aina ya Nokia S6 ( Sh. 500,000), Nokia E200 (Sh. 250,000) na Blackberry ambayo hakutaja thamani yake.

Vingine ni pete mbili za madini ya fedha, fedha taslimu Dola za Kimarekani 4,000 (Zaidi ya shilingi milioni 6.3), shilingi milioni 1.5, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo na nyaraka mbalimbali za serikali, zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 23.25.

CHANZO: ALIYEMUIBIA WAZIRI MALIMA NI CHANGUDOA - Global Publishers

Hawa majizi hawana dini wanachafua Uislamu. Waislamu tunajisikia vibaya kuona majina yote ya dini yetu yakihusishwa na kumwibia Malima Mwislamu wenzetu. Hii haina maana asiye mwislamu ndiye wa kumuibia. Dhambi ni dhambi mbele ya mwenyezi Mungu haina dini.
 
Back
Top Bottom