Aliyekufa kwa ukimwi alikuwa ni hawara yake!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,395
Hebu tuchukulie kwamba, umepata taarifa kuwa, kuna dada binamu wa mumeo ambaye alikuwa ameolewa na kuachika amefariki. Na amefariki kwa ukimwi. Wewe na mumeo mnakwenda kushiriki kwenye mazishi. Mnapofika huko unasikia minong'ono kuwa huyo binamu alikuwa ni hawara wa mumeo, na hata mtoto wake wa mwisho inasemekana ni wa mumeo.

Kumbukumbu zako zinaonesha kwamba, mumeo alikuwa karibu sana na binamu yake huyo na alikuwa akimpa misaada mingi tangu aachike na hata kipindi cha kuumwa kwake alikuwa mstari wa mbele kumsaidia.

Baada ya mazishi unafanya uchunguzi wa kimya kimya na hatimaye unathibitisha pasi na shaka yoyote kwamba, jambo hilo lina ukweli kwa asilimia 100.

Hebu niambie kama ni wewe umepata taarifa kama hizo ungefanyaje?
 
Natulia, nakwenda kupima afya, nikigundua
nimeathirika, namshauri na huyo mwenzangu akapime akikubali nitashukuru kwa sababu wote tutajitahidi kuishi kwa tahadhari, akikataa basi najinda na kwa kula vizuri, kutumia dawa ili niweze kutimiza malengo kadhaa kabla sijapumzika. Hakuna kulaumu wala kujilaumu kwani kwa kufanya hivyo hakupunguzi kitu. Najipa moyo ktk Mungu kwani kwa kumtegemea yeye atayafanya maisha yawe marahisi.
 
dah, kwa mara ya kwanza kusikia nitaishiwa nguvu bt nitajikaza nikapime baada ya hapo nitajua cha kufanya
 
hapo mwana naenda zangu kupima na kama najikuta nina ngoma...direct mahakami kufuguwa kesi dhidi ya mume wangu....asilete zakuleta hapa mie ajilinda alafu yeye na taamaa zake aje kuniletea gonjwa...cha moto atakiona.....

alafu mie nashindwa elewa mtu kutoka nje ya ndoa siku hizi kawaida and should be expected lakini cha kushangaza ni kwamba kwa nini watu wanashindwa tumia kinga jamani?
 
Hebu tuchukulie kwamba, umepata taarifa kuwa, kuna dada binamu wa mumeo ambaye alikuwa ameolewa na kuachika amefariki. Na amefariki kwa ukimwi. Wewe na mumeo mnakwenda kushiriki kwenye mazishi. Mnapofika huko unasikia minong'ono kuwa huyo binamu alikuwa ni hawara wa mumeo, na hata mtoto wake wa mwisho inasemekana ni wa mumeo.

Kumbukumbu zako zinaonesha kwamba, mumeo alikuwa karibu sana na binamu yake huyo na alikuwa akimpa misaada mingi tangu aachike na hata kipindi cha kuumwa kwake alikuwa mstari wa mbele kumsaidia.

Baada ya mazishi unafanya uchunguzi wa kimya kimya na hatimaye unathibitisha pasi na shaka yoyote kwamba, jambo hilo lina ukweli kwa asilimia 100.

Hebu niambie kama ni wewe umepata taarifa kama hizo ungefanyaje?
unambania unyumba hadi vipimo vifanyike zaidi ya mara tano................
ushauri kwa akina dada.............
 
Hizi tabia za kujifanya mnatoa mifano wakati wewe ndio muhusika mtaacha lini? maana kuna tabia imeshajengeka hapa kwa members kutumia third part. njoo hapa kama wewe na sio kusingizia eti kwa mfano!
 
Natulia, nakwenda kupima afya, nikigundua
nimeathirika, namshauri na huyo mwenzangu akapime akikubali nitashukuru kwa sababu wote tutajitahidi kuishi kwa tahadhari, akikataa basi najinda na kwa kula vizuri, kutumia dawa ili niweze kutimiza malengo kadhaa kabla sijapumzika. Hakuna kulaumu wala kujilaumu kwani kwa kufanya hivyo hakupunguzi kitu. Najipa moyo ktk Mungu kwani kwa kumtegemea yeye atayafanya maisha yawe marahisi.
Umesha sema yote. Ndio hivo tu. labda ambacho mimi binafsi ningefanya ni kukasaidia pia kale katoto ka marhem sababu ana damu moja na wanangu na pia yeye ni victim kama mimi (ikkiwa nina ukimwi)
 
Ni kwenda kupima tu siku hizi ukiwahi mapema na kufata masharti wanayotoa washauri unaishi maisha marefu tu
Ila nitakosa imani na mume sana na lazima kikao cha ndugu kiitishwe pia, wakiendelea na uhusiano naanza maisha mapya mwenyewe
 
inatakiwa kutuliza akili kupima na kujua hali halisi basi mshauri mwenzako mkapime then mjipange jinsi ya kuishi kwani tayari tatizo litauwepo
 
Back
Top Bottom