Aliyejichoma majimoto afunguliwa mgahawa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAMKE mmoja [32] mkazi wa jijini Dar es Salaam, aliyeweza kujiunguza na maji ya moto ili aweze kuomba barabarani apatiwe mtaji, nduguze wamfungulia mradi wa kuendesha mgahawa eneo la Buguruni.
Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, ndugu waliomkataza aachane na kuomba barabarani kwa pamoja walishirikiana kumtafutia mtaji na kumfungulia mgahawa ikiwa ni kumtaka aendeshe maisha yake pasipo kuomba.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo tayari ameshaanza biashara hiyo mwanzoni mwa wiki hii na kudaiwa kuwashukuru ndugu zake waliojitolea kumfungulia biashara hiyo.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo anaapa kutokuwa na hamu ya kuolewa kwa kuwa tayari alishapata mateso kutoka kwa mtalaka wake ambaye alimtelekeza na mtoto na kuishi maisha magumu yaliyompelekea kuomba ili ndugu zake waweze kumsaidia.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alitumia mbinu ya kuomba barabarani ili aweze kupatiwa msada na ndugu zake kwa kuwa ndugu hao hakuna aliyeamini kama angekosa mtaji kwa kuwa ilidaiwa alikuwa na maisha ya juu alipokuwa na mumuwe huyo
 
masikini, yaani mwanadamu anajiunguza kwa maji ili aombe!! jamani, nyie, maisha haya??

hii dunia sijui tunaenda wapi. ndugu hawapendani kabisa, heri hata marafiki!!

yaani hadi mtu ajiunguze kwa maji ndio muone haja ya kumsaidia?? very sad, sad, sad indeed!!

loo, Mungu tuhurumie watoto wako
 
kaazi kwelikweli mafisadi wanaliona hili?

kweli ipo kazi kwelikweli hapo.

ukiona magari ya serikali au misafara ya JK akisafiri nje ya mnchi, unaweza kufikiri ni rais wa nchi yenye kila kitu, hapo hujasikia majigambo yao kuwa "uchumi unakua" ukijua thamani ya nyumba ya gavana wa benki kuu ya umma, kamwe huwezi kuamii habari kama hizi. hapo hujauliza posho ya siku ya waheshimiwa!!, sikiliza basi hadithi za kujivua magamba na angalia misururu ya mashangigi yanayohudumiwa na fedha za umma inavyopishana huko dodoma wakati wa ccm kujivua magamba!!

jamani jamani, nchi gani hii, watu waliopewa dhamana za uongozi hawawajali kabisa wapiga kura wao?

nafikiri hata ndugu wamechekwa kwanza na majirani zao ndio wakajikosha kutoa hako kamsaada, yaani ili wafiche nyuso zao, lakini upendo miongoni mwao ni ziro kabisa!!
 
kiongozi mwenye vyeo 2 chamani na serikalini unakuta kila cheo na gari lake anafanya kubadilisha tu

Back
Top Bottom