Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Wananchi wenye gazab ya kufa mtu ktk kijiji cha Igombe wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza juzi walimtandika ile kisawasawa mkazi wa mmoja kijiji hicho kwa tuhuma za kumla uroda binti yake wa mika 17 tena bila idhini (kubaka).

Taarifa kutoka jiji hilo maarufu kwa jina la Rock City,mtuhumiwa Bozi Benjamini (45) anadaiwa kumbaka binti yake juzi majira ya saa 11:00 alfajiri wakiwa nyumbani kwao mbele ya wadogo zake wawili bila kuona aibu na kumsababishia maumivu makali ktk nyeti zake.

Taarifa hizo ziliendelea kueleza kuwa dingi hilo lenye uchu linaishi bila wife na inadaiwa kuwa sio mara ya kwanza kumwingilia binti yake kwa nguvu ambaye siku za nyuma alilazimika kutoroka nyumbani hapo kutokana na vitendo vichafu vya baba yake.

Inaelezwa kuwa siku ya tukio wakati dingi akifanya ufirauni huo binti huyo na wadogo zake walipiga kelele na ndipo wananchi walipojitokeza kuwasaidia na kwamba wananchi hao walianza kumshushia kipigo cha nguvu na baadaye kumpeleka kituo cha polisi.

Binti huyo alikimbiziwa hospitali ya mkoa ya Sekou Toure kwa ajili ya matibabu na kwamba hali yake kwa sasa inaendelea vizuri.

http://www.darhotwire.com/home/news/2009/08/22/aliyefumwa_akibaka_bintiye_ala_kichapo.html
 
kuku kula mayai yake hiyo,,,,,,,,,,,,mtu chake sio???????ooops did i say that????
 
Back
Top Bottom