aliyeenguliwa kwenye kugombea ubunge mbeya vijijini

Ticha

Senior Member
Aug 26, 2007
135
8
aliyeenguliwa kwenye uchaguzi wa UBUNGE kwa tiketi ya CHADEMA,katika uchaguzi mdogo wa MBEYA VIJIJINI mwaka jana.Advocate Sambee Shitambala.Sasa awa MWENYEKITI WA CHADEMA WA MKOA WA MBEYA.
na anaenderea kutikisa mkoa hasa Mbeya vijijini,
 
I have known the lad for 23 years. Bright and determined. The issue is whether he can make a good politician and whether he can withstand and resist temptations that few other opposition leaders have been unable to resist i.e. being lured to dump the opposition bandwagon in favour of the ruling party.
 
aliyeenguliwa kwenye uchaguzi wa UBUNGE kwa tiketi ya CHADEMA,katika uchaguzi mdogo wa MBEYA VIJIJINI mwaka jana.Advocate Sambee Shitambala.Sasa awa MWENYEKITI WA CHADEMA WA MKOA WA MBEYA.
na anaenderea kutikisa mkoa hasa Mbeya vijijini,

Hayo maneno yana ukweli Ndugu? Thibitisha.
 
Ndugu zangu wa Chadema niliwaambia hivi: "Hata muwe na Operation Mijebuka kamwe hamtapata Jimbo la Mbeya Vijijini".

Nyie endeleeni kutwanga maji tu.

Ninawashauri mng'anganie majimbo mliyonayo kwanza maana la Kigoma Kaskazini tutalirudisha CCM mwaka huu.
 
Utabiri wako utaendana na mgombea ambaye CCM watamweka. Kama ataendelea kutetea jimbo mchungaji Luckson Mwanjali, basi Shitambala atashinda! Believe me!
 
Kwa Mbeya Vijijini CCM wenyewe wanamwelewa vizuri sana Sambwee, ndo maana walitafuta kila njia ya kumzuia wakati ule, na kweli akaonekana amechemsha.
Lakini kwa sasa patakuwa na patashika kubwa sana, maana yule bwana anauzika hadi vijijini, na amefundisha shule kadha kabla ya kwenda chuo kikuu.
Mimi regardless ya mtu atakayewekwa na CCM,namtabiria ushindi!
 
Nilisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kampeni zake, ilikua imejaa tumaini, uelewa ,uweledi na hamasa..! hakika kazi iko kwa wananchi wa mbeya, kazi kwenu kuchagua lililo bora..! Binafsi namkubali..!
 
Kazi njema mpaka kieleweke na huko mbeya
kigoma kaskazini ng'o hata kama mmefanya umafia wa kuipunguza saizi
siku yenu yaja japo mna uzoefu mkubwa kuiba kura
 
Kwa Mbeya Vijijini CCM wenyewe wanamwelewa vizuri sana Sambwee, ndo maana walitafuta kila njia ya kumzuia wakati ule, na kweli akaonekana amechemsha.
Lakini kwa sasa patakuwa na patashika kubwa sana, maana yule bwana anauzika hadi vijijini, na amefundisha shule kadha kabla ya kwenda chuo kikuu.
Mimi regardless ya mtu atakayewekwa na CCM,namtabiria ushindi!

PJ,
Kwa watu wasioijua vema Mbeya Vijijini ama mijini wanaweza kudhani tunnachokiongea hapa ni mzaha.
Kumbuka mwaka 1995, CCM walimteua Mzee Bruno Mpangala, aliyekuwa katibu Mkuu wa iliyokuwa OTTU, kugombea ubunge Mbeya mjini. Vigogo nyeti wa CCM wa mkoa wa Mbeya kwa wakati huo, akina Mzee Cosmas Kadeghe, Mwaji n.k. walitupwa nje. Wananchi hawakuridhika na chaguo hilo (Mpangala), hivyo wakampigia kura Polisya Sikumbula Mwaiseje wa NCCR Mageuzi, aliyekuwa mwalimu wa chuo cha biashara TIA pale Mafiati. Hii inaweza kutokea pia iwapo CCM hawatachanga karata zao vema kwenye kuchagua mgombea wa kushindana na Shitambala. Jamaa anauzika!
Lisemwalo lipo.
 
Mpaka kieleweke!!!!!!!!!! Chichiemu endeleeni tu na ndoto za miaka mitano iliyopita cha moto kiko mbele yenu. Nasema cha moto!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom