Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Mhusika mkuu wa kupanga ulipuaji wa balozi za Marekani huko Nairobi Kenya na Dar-es-Salaam, Tanzania imeripotiwa ameuawa huko Somalia Jumatano iliyopita. Fazul Abdullah Mohammed ndiye mtu aliyekuwa anatafutwa sana Afrika baada ya milipuko ile ya Augusti 8, 1998 ambayo ilisababisha vifo vya watu 220 na mamia wengine kujeruhiwa wakati magari yaliyojaa mabomu yalipolipuliwa katika malango ya balozi hizo.
Tukio hilo lilikuja baadaye kuhusishwa na kikundi cha kighaidi cha Al-Qaida na lilikuwa ni tukio kubwa la mashambulizi dhidi ya maslahi ya Marekani kabla ya mashambulizi ya kikundi hicho Septemba 11, 2001 huko Marekani.
SOMA ZAIDI FIKRAPEVU.COM