Alivyokuoa amepunguza vituko

Wa Nyumbani

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
438
65
Wiki moja baada ya harusi, Jamaa akaanza kurudi nyumbani akiwa ananuka sigara. Mke wake akakasirika na kumweleza kuwa mbona kabla ya harusi alisema havuti sigara? Kesho yake jamaa akarudi amelewa sana. Mke wake akazidi kukasirika na kulalama.

'Ulisema hunywi pombe, mbona unakunywa?"
Siku iliyofuata kukazuka zogo mtaani. Mwanamke alipokwenda kwenye tukio akakuta jamaa amefumaniwa na mke wa mtu. Mke akabaki ameduwaa!

Mwanamke mmoja jirani yake akamwambia,
"Shoga usishangae, huyu mume wako ni mtu wa vituko hapa mtaani. Hivi alivyokuoa tunaona amepunguza vituko, ni mlevi kupindukia, mvuta bangi na ni mzinzi mkubwa. Ametembea na wanawake karibu wote hapa mtaani. Usituone hivi, wenzako tunajuta!!"
 
hahahahahaahahha nshashuhudia kisa kama hiki kinondoni,ila kuna gumegume liliingia na mlango siku ya tano tangu bidada kaingia ndani,kila siku vikao kwa mjumbe mume anasutwa na waume za watu kwa kuwala tigo wake zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom