Alichojifunza Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kuhusu Nchi za Magharibi

Yeah, asingekuwa fisadi angekwenda kwenye buku la historia kama mojawapo wa mabrilliant leaders tuliowahi kuwa nao.
 
The question that Mkapa ought to be asked is did he make his money the old-fashion way? ...LOL
 
ulaghai tu.. kwamba amejifunza kutoka nchi nyingine suala la upuuzi wa kutegemea fedha za watu wengine kwa maendeleo inashangaza. Hivi hakusoma azimio la arusha ambalo liliandisha kitu ilichokiita "Kutegemea fedha kama msingi wa maendeleo"?
 
anajitahidi ili historia ya tanzania isimsahau, atahangaika sana

Kama yeye atahangaika Kikwete atafanya nini? Hebu jaribu fikiria na kutafakari kauli anazozitoa Kikwete anapotembelea wizara mbali mbali. Kwa Mheshimiwa Makufuli alisema tuangalie vizuri zoezi la bomoabomoa wananchi wasijeichukia serikali. Je wanaendesha nchi wapendwe na wananchi badala ya kufikiria maendeleo? Jana Maendeleo ya Jamii wanawake na watoto ameagiza swala la watoto wa mitaani lishughulikiwe haraka. Je tangu ameingia madarakani 2005 hakuliona hilo? Na je waziri atatumia njia ipi kutatua swala ambalo liko tangu wakati wa mwalimu ili hali serikali yenyewe inashindwa kulipa hata mishahara ya wafanyakazi wake kwa wakati unaostahili? Jana vile vile ameagiza hifadhi ya taifa ya chakula imwage chakula kwa wingi Dar ili mfumko wa bei ya chakula ushuke. Je hifanyi ya taifa ya chakula iko kwa ajili hiyo? Je kama watamaliza akiba kwa lengo la kupunguza mfumko wa bei njaa itakapokuja tutakula nini? Msimu huu mvua zimekuwa za shida sehemu nyingi na kuna uwezekano mkubwa wa kutokea upungufu wa chakula mwaka huu na mkuu wa nchi hii anatoa agizo akiba ya chakula itumike kupunguza mfumko wa bei ya chakula bila kufikiria siku za baadaye. Namna hii si itafikia mahali tuanze kuomba mahindi Malawi, bulga Marekani na mchele China na Japan. Huyu na Mkapa ni yupi zaidi japo kila mtu ana mapungufu yake?
 
Kama yeye atahangaika Kikwete atafanya nini? Huyu na Mkapa ni yupi zaidi japo kila mtu ana mapungufu yake?

Mkuu hii inanikumbusha 'Mrs Rat anamcheka Mrs Agama(reptile) kuwa Mr Agama ana mkia'. Hakuna kikwete wala mkapa, wote wameliangamiza taifa! (hakuna afadhari wote wameharibu ustawi wa nchi)
 
Back
Top Bottom