Ali Kiba kurekodi video Marekani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
Ali Kiba kurekodi video Marekani
2190210.jpg

Ali Kiba Monday, June 08, 2009 12:46 PM
MSANII wa Bongo Fleva, Ali Kiba anatarajiwa kufanya video mbili za nyimbo zake huko Marekani. Akizungumza mtandao huu mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Ali Kiba alisema ameamua kufanya video zake Marekani ili kuzipa ubora unaotakiwa kimataifa.

Msanii huyo alisema yuko katika maandalizi ya mwishomwisho kuelekea nchini humo na picha za video zinatarajia kuchukuliwa katika miji ya Los Angeles na Seattle.

“Nina nyimbo mbili ambazo nitazifanyia video Marekani, Tell Me Why nitaurekodi Los Angeles na 1st Single nitaifanyia Seattle,” alisema.

Ali Kiba ambaye alipata kutamba na nyimbo mbili za Cinderella na Mackmuga, alisema vibao vyake viwili vya Los Angeles na 1st Single vitakuwamo katika albamu yake mpya ya Msiniseme
 
Haha eti kuzipa ubora wa kimataifa, kinachoipa video yako ubora wa kimataifa ni bajeti.

Mods tafadhali peleka hii kwenye entertainment. Ahsante.
 
King Kiba....

Enzi hizi Dimond anaosha vyombo studio kwa bob Junio
Hivi huoni aibu kwamba, pamoja na huyo mwingine kusema alikuwa anaosha vyombo lakini ndie ambae Kiba ana-struggle kumfikia? Hivi huoni aibu kuona kwamba, ingawaje huyo mwingine alikuwa anaosha vyombo lakini nyayo zake hivi sasa ndio zinafuatwa?! Hivi huoni aibu kusema kwamba enzi hizo Diamond alikuwa muosha vyombo wakati statistics zinaonesha yeye ndie yupo juu kwa kila idara?!

Ungejisikiaje umeripoti Form I January halafu mwingine anaripoti April lakini kwenye terminal exam anakuacha kwenye kila somo huku wewe ukibaki kujivunia "...lakini mimi ndie mwenye mwandiko mzuri kuliko yeye!!!!"
 
Kiba kilaaaza tu muongoo sanaaa ndo manaaa atazidi kuitafuta bifu na Mondi ili apate
 
Hivi huoni aibu kwamba, pamoja na huyo mwingine kusema alikuwa anaosha vyombo lakini ndie ambae Kiba ana-struggle kumfikia? Hivi huoni aibu kuona kwamba, ingawaje huyo mwingine alikuwa anaosha vyombo lakini nyayo zake hivi sasa ndio zinafuatwa?! Hivi huoni aibu kusema kwamba enzi hizo Diamond alikuwa muosha vyombo wakati statistics zinaonesha yeye ndie yupo juu kwa kila idara?!

Ungejisikiaje umeripoti Form I January halafu mwingine anaripoti April lakini kwenye terminal exam anakuacha kwenye kila somo huku wewe ukibaki kujivunia "...lakini mimi ndie mwenye mwandiko mzuri kuliko yeye!!!!"
Mbona povu tena?!

Kwa hiyo hakuwa anaosha vyombo Kwa Studio Kwa bob Junior?!
 
Back
Top Bottom