Alart;wizara ya afya mbona ilichanganya mambo

PAFKI

Senior Member
Sep 30, 2011
116
38
Naomba tukumbushane kidogo sakata la wizara ya afya kutangaza vipimo feki vya VVU,katika aya ya pili kwenye taarifa yao walioichapisha kwenye mtandao wao kuna sentensi hii ¨Ninapenda kuwafahamisha kwamba, vitendanishi hivi vilivyo na hitilafu havitoi majibu (invalid results) na sio kwamba vinatoa majibu yasio ya kweli´´ Kwani majibu yasiyokweli ni yapi? kama sio hayo yaliyotolewa hasa zaidi mwezi desemba ambao ndio watu wengi walihamasishwa kupima nchini kote hasa ktk kilele cha sikukuu ya ukimwi duniani?

Wasiwasi wangu kwa wale waliopimwa mwezi huo kwa kutumia vipimo hivyo waliambiwa ni negative kutokana na kipimo kutotoa majibu (kwa mujibu wa wao) na kumbe ni positive inakuwaje?

Kwanini haikuwashauri watu waliotumia vipimo vya aina hiyo kurudia maana kuna watu wengine hujiridhisha na kupima mara moja au mbili tu, na pengine hata mtu ilikuwa ni mara yake ya tatu na vipimo vikasema uongo inakuwaje?

NAWASILISHA
 
Hiyo statement yao ni uzushi.....invalid results pia ni majibu lakini siyo majibu halisi na kama ni kweli basi siyo majibu ya kweli....tofauti na no results...NIL. wanachezea watu, vitendanishi havifai tu.
 
Back
Top Bottom