Alama za No Entry Jijini Dar

nkosikazi

JF-Expert Member
Mar 11, 2010
361
336
Wakuu nimeona alama nyingi sana kwenye bararabara za Dar ambazo wanataka kuintroduce ili magari yasipite pande hizo. Zinatisha sana! Zimewekwa kila mahali na kama zitatekelezwa hivyo hakutakuwa na barabara inayopitika! Pamoja na kwamba alama za no entry zimewekwa lakini hakuna driver anayezijali na wala hamna anayefanya kazi ya kuzisimamia. Nani kazitengeneza na kwa gharama gani? Kuna utafiti wowote ulitumika kabla ya kuziweka?
 
Mimi nashangaa, katika barabara ya Garden Avenue; kuna alama ya ano entry imewekwa, ila haifuatwi!! Watu wanapeta tu, hii ni nchi inaoyoongoza kuwa nchi yenye "law less-ness"

Maana situation ya barabarani hapa TZ inatisha...
 
Wapendwa wana Jamii forum,
Jambo wote.
Ni mara yangu ya kwanza kusema nanyi kwa mtandao.
Inatia moyo kuona tunajali jamii inavyoendesha mambo ya jamii yetu.
Ni kweli kabisa kumekuwa na vibao vingi vimewekwa na mamlaka husika kubadili matumizi ya njia hizo.

Zipo sababu nyingi, lakini nataja moja ambayo ni msongamano wa magari unaosababishwa na watumiaji kuegesha magari upande mmoja na kuacha njia nyembamba kwa njia zote kutumika.

Kutokana na hali hiyo huenda mamlaka imeona ijaribu njia hii.

Nani asimamie, ni swala linalohitaji elimu kwanza kwa watumiaji kabla ya kuanza kuadhibu wakosaji. Kikubwa tunatakiwa tukumbushwe na kuelekezwa kwa njia mbalimbali za vyombo vya habari, ramani zitolewe kwa watumiaji n.k.

Tukumbuke, mabadiliko ni jambo lenye kuleta sura mpya katika jamii; hivyo si vibaya kujaribu njia hii ya one way; siyo no entry, maana kama hii ni no entry, basi ipo inayoruhusu upande wa pili.
Kwa leo nawasilisha.

Simosi
 
Nani asimamie, ni swala linalohitaji elimu kwanza kwa watumiaji kabla ya kuanza kuadhibu wakosaji.
"Elimu kwanza kabla ya kuadhibu" ndio nini? Ukikamata mwizi utampa "elimu kwanza kabla ya kuadhibu"? Utaratibu ukitangazwa kuanza kutumika lazima uanze kuwa enforced immediately, wacha kuchemka we babu!
 
Sasa hivi tanzania kila kitu ni komedy show kwa kwendambele,

tatizo ni kuegesha magari, jee ikiwa njia moja watu hawataegesha magari?

wamaeno wajaribu? experiment itagharimu kiasi gani na nani atabeba gharama hizo?
 
Nilipopeleleza nimeambiwa hizo alama hapo Dar city center hazijaanza kutumika bado. Mkandalasi alikuwa amezifunika kwa magazeti bali mvua zilizonyesha karibuni zimefunua alama.
 
Wapendwa wana Jamii forum,
Jambo wote.
Ni mara yangu ya kwanza kusema nanyi kwa mtandao.
Inatia moyo kuona tunajali jamii inavyoendesha mambo ya jamii yetu.
Ni kweli kabisa kumekuwa na vibao vingi vimewekwa na mamlaka husika kubadili matumizi ya njia hizo.

Zipo sababu nyingi, lakini nataja moja ambayo ni msongamano wa magari unaosababishwa na watumiaji kuegesha magari upande mmoja na kuacha njia nyembamba kwa njia zote kutumika.

Kutokana na hali hiyo huenda mamlaka imeona ijaribu njia hii.

Nani asimamie, ni swala linalohitaji elimu kwanza kwa watumiaji kabla ya kuanza kuadhibu wakosaji. Kikubwa tunatakiwa tukumbushwe na kuelekezwa kwa njia mbalimbali za vyombo vya habari, ramani zitolewe kwa watumiaji n.k.

Tukumbuke, mabadiliko ni jambo lenye kuleta sura mpya katika jamii; hivyo si vibaya kujaribu njia hii ya one way; siyo no entry, maana kama hii ni no entry, basi ipo inayoruhusu upande wa pili.
Kwa leo nawasilisha.

Simosi

Karibu sana kwa magretisinka.Umenena vema uliposema "nadhani mamlaka husika zimeamua hivyo ili kupunguza msongamano"eneo linalopigiwa kelele kuwekwa hizo sign ndilo ambalo mamlaka zinaongoza kwa kukusanya tozo ya parking sasa iweje wasimamie kuchukua pesa tu wasiweze kusimamia matumizi sahihi ya barabara?na hii inamaanisha wanachukua tozo pasipostahili,no entry no parking
 
Back
Top Bottom