Ala kichapo kwa ulawiti

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,083
3Mtuhumiwaakichezeakichapo.jpg ALAKICHAPO.jpg mtuhumiwahuyoakipatakipigo04.jpg MtuhumiwawakulawitiMtoto05.jpg 4.Mtuhumiwawakualwiti03.jpg

Na Mashaka Baltazar, Mwanza
MCHUNGA ng’ombe, Johnson Abdul, mkazi wa Sweya Nyegezi, katika Kata ya Mkolani, wilayani Nyamagana Jijini Mwanza, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 6 na kumsababishia maumivu makali.

Tukio hilo lilijiri Machi 31, mwaka huu, majira ya saa 4:00 asubuhi katika moja ya kilima cha eneo hilo ambako mtuhumiwa alikuwa akichunga mifugo yake.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Abdul ambaye anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 26, alimwita mtoto huyo (jina linahifadhiwa) na kwenda kumwingilia kinyume cha maumbile.

Ilielezwa kuwa baada ya mtoto huyo kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama, alikwenda kwenye genge la biashara analofanyia mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la mama Kelvi, akilalamika kuumwa tumbo na baadaye kutoa kinyesi chenye aina ya makamasi.

Hali hiyo ilimshtua mama yake na kumhoji kulikoni ambapo mtoto huyo aliweka wazi kuwa aliingiliwa na mchunga ng’ombe Johnson.
“Mwanangu alikuja majira ya saa 9:00 alasiri kibandani ninakofanyia shughuli zangu akilalamika kuumwa tumbo, lakini cha kushangaza alipoenda

haja kinyesi kilikuwa kama mlenda mlenda au makamasi na hakuwa na raha, hali hiyo ilinishtua,” alisema mama huyo.
Akaendelea: Kufika saa tatu usiku kijana mmoja aitwaye Eden alimweleza mdogo wangu kuwa tumuulize vizuri mtoto ili atuambie ukweli kwani kuna mtu alimwita waende kuchunga ng’ombe kwa ahadi ya kumlipa fedha.

“Mtoto alipoulizwa alikiri kuitwa na Johnson na kusema alimwingilia kinyume na maumbile mara baada ya kufika machungani,” alisema mzazi wa mtoto huyo.

Alisema, Machi 31, mwaka huu (Jumamosi) mtuhumiwa alimwita tena mtoto huyo akamtaka ampelekee watoto wenzake, ndipo mtoto huyo alipokwenda kutoa taarifa kwa mama yake ambapo walimfuatilia mtuhumiwa na kumnasa akiwa na mtoto mwingine.

Mtuhumiwa alipomwona mtoto aliyedaiwa kumlawiti yuko na mama yake alitimua mbio, ilibidi mwanamke huyo apige mayowe ya mwizi ambapo watu wakajitokeza na kumsaidia kumfukuza hadi walipomkamata na kumpa kipondo.

Johson alikiri kumwingilia mtoto huyo lakini akajitetea kuwa alishawishiwa na mtoto mwenyewe kwa kumfanyia kitendo hicho.
Baada ya mahojiano hayo, polisi waliitwa kumchukua mtuhumiwa huyo na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Igogo kwa hatua zaidi huku mtendewa huyo akipelekwa kupimwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ambapo ilibainika alilawitiwa.
ALA KICHAPO KWA ULAWITI - Global Publishers
 
Back
Top Bottom