Al-Shaabab/Maharamia wa Somalia wanabadilisha vipi fedha haramu Afrika ya Mashariki?

Hivi vikundi vya Al shaabab na venginevyo ni machine ya USA kwa ajili ya kuifanya Africa, MidEast kuwa mahali pa vita tu bila ya amani. Hii ndiyo inaitwa New World Order.

Mchina sasa hivi anaitaka Africa, na keshaichukua Africa kiuchumi-investments kwa asilimia kubwa sana. Hivi unadhani Wazungu-West watakubali hivi hivi tu waikose Africa?

Dawa- ni kuanzisha vita ili mikataba mipya ianze kusaigniwa. Tumeona Libya-Wazungu walipoona wameshaanza kuikosa kwa Mchina- dawa ni regime change. Sasa hivi Libya ipo mikononi mwao.

Sasa hivi wanaitaka East Africa. Kwa nini? Kuna port kubwa inayoingiza na kutoa mali kwenda na kurudi kutoka China na Asia. Dawa- anzisha vita. Kama hamna amani hamna biashara.

USA tayari wanazo Drones-Attack ktk East Africa ambayo inaweza kuattak popote pale kama wakipata target ya Al shaabab.

Kazi tunayo EA. Hatuna Amani tena

Kama kuna tatizo ambalo ni kubwa hapa Afrika ni kujaribu ku-link kila tukutanacho na watu wa Magharibi. Sasa tunakuwa kama tumesahau kuwa Somalia ni nchi isiyokuwa na serikali kwa miaka zaidi ya 20 na sisi waafrika tunaona sawa tu!. Nionavyo mie huu sasa ndiyo muda wa kuona matunda ya kutokuwapo serikali pale nchini Somalia. Wale usidhani ni US au China au nani...!

Wale wasomali waliozawa miaka ya 80 na 90 walikuta hakuna mfumo wa kielimu na kijamii, hawakupata fulsa kama unazopata wewe hivyo wamekua bila matumaini na sasa wanajaribu ku-survive. Tukiri makosa yetu kwa kuacha Somalia iangamie kwa miaka yote. Na kama hakutakuwepo na serikali pale Somalia kwa miaka ijayo basi tatizo la wasomali litakuwa kubwa kuliko tuonavyo sasa.

 
Kwamba Al Shaabab wamekuwa wakipata mamilioni ya dola kutokana na shughuli za uharamia huko Somalia. Lakini dalili zote zinaonesha kuwa fedha hizo huhamishwa na kuingizwa katika mifumo ambayo itazisafisha fedha hizo na kuzifanya halali. Hii ni pamoja na kununua viwanja na nyumba maeneo mbalimbali ya Nairobi na hata inadokezwa kuwa sehemu fulani za Tanzania.. Je, tunajua nini kuhusu kuingia kwa sympathizers wa Al Shaabab nchini?

Ni kweli kuwa ujenzi wa eneo moja huko maeneo ya Bahari Beach nje ya jiji la Dar yumkini unahusiana na masuala haya ya Al-Shaabab?

Kwa msimamo wa Al Shabab wa mwanzo ni against uharamia na waliweza kuonyesha hilo pindi walipoitwaa somalia kabla ya kufulushwa na majeshi ya Ethiopia. Walipoteka Mogadishu waliamuru maaramia kuachia meli zote walizokuwa wanashikilia bila kuomba hata vikombozi na wakawapa siku 3 baada ya pale waliwashambulia walioshindwa kutii hiyo amri yao na meli zote ziliachiwa bila vikombozi.

Hilo la utakatishaji pesa ktk nchi za EA limeongelewa sana na mimi naamini ni kweli. Kenya wanasumbuliwa sana na tatizo hili kwasababu ya kuwa na jamii kubwa ya Kisomali lakini na Tz nasi lazima hizo hela zinawekezwa hapa. Kwa nchi kama zetu ambazo unaweza kufanya lolote ukiwa na hard-cash ni rahisi sana kutakatisha pesa haramu!
 
Al-Shaabab ni kikundi cha Kiislam, kinachoendeleza mashambulizi zidi ya raia wema. Kilianzishwa na Marehemu gaidi Osama,na kinaenea kwa kasi wakifadhili na kujenga misikiti.

Hawa jamaa wanauwezo kifedha, waliingia Kenya kama wafanyabiashara na kununua majumba ya kifahari na wameanza kuja kwa kasi Tanzania.

Wanamajumba Mbezi, Masaki na hata Osterbay. Mifumo yetu ya kukumbatia wageni na rushwa hasa upande wa idara ya uhamiaji kuna siku tutakuja lia na kusaga meno.

Al-Shaabab wana hata passport za Tanzania
 
Hawa jamaa kama umebahatika kufanya nao biashara wanapenda sana kumaliza deal fasta, kawaida yao ukitaja bei wanaweza wakupe zaidi ya ile ili usiwe na muda wa kufikiria na biashara imalizike fasta. Kama wakitaka kupanga nyumba yako wanataka long term na watalipia hata miaka kumi na wewe usionekane pale hadi ule muda umekwisha, hizi zote ni dalili sio nzuri kuna siri kubwa pale. Pia kama ukiwachungulia vizuri hawa jamaa sio kwamba ni wasomi au wana mashamba makubwa na mazuri itakuwa vipi wapate utajiri...nwy
 
Nyepesi nyepesi zinadokeza kuwa wengi wa wale wasomali wanaouza used computer pale mitaa ya kariakoo ni members wa Al Shaabab wanaojaribu ku expand network ya Al Shaabab hapa Tanzania na tayari wameisha anza kumiliki mahekalu na ma estate ndani ya Tz, tena nyingi ya hizo used laptops & PC ni zile zilizo ibiwa uarabuni na kenya zikiwa zimechakachuliwa tena wengi wao hawawezi hata kuongea kiswahili ( according to bwana mdogo wangu anaewafanyia kazi za ku repair na kuzichakachua) sijui intelijensia authorities zetu kazi yake ni nini? ( ! zaidi ya kuwasaidia wamagamba kuiba kura tuu) wakati nchi tayari imeisha anza kuingiliwa, sitaki kuamini kuwa hawa jamaa wanatuzidi ujanja

''sasa kumbe mdogo wako mwenyewe ndio anasaidia hao wasomali wa Al shabab then unakuja kulalama kuhusu authorities, usalama unaanzia kwa wananchi ambao ni pamoja na wewe na mdogo wako''

 
Dobi mkubwa wa fedha chafu za Al- Shaabab hapa Tanzania ni AbdulRahmani Kinana, huyu ni kada mwandamizi na mweye ushawishi mkubwa katika siasa za CCM, hivyo utaona hapa kuna direct link kati ya hawa maharamia na serikali ya Tanzania inayoongozwa na CCM, hivyo ni kazi nyepesi kwa fedha chafu hizo kusafishwa hapa chini ya usimamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo kimsingi vilitakiwa kuzuia uhalifu huu. Waliosema kuwa CCM kuwa madarakani ni janga la kitaifa wako sahihi kabisa.Moja wapo ya njia hizo ni kuzitumia fedha hizo katika chaguzi mbali mbali kwa manufaa ya CCM, na CCM nayo huwatengenezea wafadhili wao hao mianya ya kufanya bishara halali kama vile mahoteli nk.
 
Kama kuna tatizo ambalo ni kubwa hapa Afrika ni kujaribu ku-link kila tukutanacho na watu wa Magharibi. Sasa tunakuwa kama tumesahau kuwa Somalia ni nchi isiyokuwa na serikali kwa miaka zaidi ya 20 na sisi waafrika tunaona sawa tu!. Nionavyo mie huu sasa ndiyo muda wa kuona matunda ya kutokuwapo serikali pale nchini Somalia. Wale usidhani ni US au China au nani...!

Wale wasomali waliozawa miaka ya 80 na 90 walikuta hakuna mfumo wa kielimu na kijamii, hawakupata fulsa kama unazopata wewe hivyo wamekua bila matumaini na sasa wanajaribu ku-survive. Tukiri makosa yetu kwa kuacha Somalia iangamie kwa miaka yote. Na kama hakutakuwepo na serikali pale Somalia kwa miaka ijayo basi tatizo la wasomali litakuwa kubwa kuliko tuonavyo sasa.


nakubaliana na hoja zako.
 
Sasa ni kwa kiasi gani TISS na taasisi zetu za Usalama zimeweza kuwa recruit Wasomali wa Tanzania kuweza kuinfiltrate Al-shaabab?
 
kumbe ami ni msomali


Mawazo ya kijinga tu na kichoyo na kutumwa kusema jambo usilolijua undani wake.
Kwa maelezo yako ni pesa gani hazifanyi hizo kazi ulizoziorodhesha.
Halafu unatilia shaka kazi za vyombo vya usalama. Ikiwa ni hivyo hiyo kazi tukupe wewe utuoneshe ushahidi wa kuhamishwa hizo fedha za utekaji meli.Usipoweza wewe ni mtu hataari na mbaya kuliko hata hao Alshabaab.Huna maana kabisa katika jamii ya watu wastaarabu.Ukiwa na nia mbaya naomba Mungu akudhibiti mapema kabla hujaleta balaa katika jamii.

Mwenye asili haachi huku tumevamiwa na wasomali, kila kona na hivi wameshawanunua viongozi wa juu sasa wanasubiri Sensa baada ya hapo tutajuta maana kila mahali wanajenga, Mbezi, Kariakoo na kote Mikoani sijui kwa nini kwao wamepaogapa, maana ukishainyea kambi uankimbilia kwa jirani
 
kwa sasa hivi wanunuzi wakubwa wa nyumba na viwanja ni wasomali zamani walikuwa wanapata pesa zao kutokana na ujangili wa kuuza pembe za faru na ndovu lakini sasa hivi kuna wafanyabiashara wengi ambao wanajihusisha na biashara kama za uuzaji magari ili mradi kuhalarisha hizo pesa ukienda kariakoo,chef pride wako wengi tembelea kawe,mbezi beach wao ndio wanunuzi wakubwa wa nyumba
 
Usiseme sana Mwanakijiji dhidi ya pesa chafu za Wasomali zinazoingizwa nchini kwa mabilioni katika jitihada zao za kuzitakasa. Watu hawatakawia kukuona mbaguzi wa rangi.

Kwamba Al Shaabab wamekuwa wakipata mamilioni ya dola kutokana na shughuli za uharamia huko Somalia. Lakini dalili zote zinaonesha kuwa fedha hizo huhamishwa na kuingizwa katika mifumo ambayo itazisafisha fedha hizo na kuzifanya halali. Hii ni pamoja na kununua viwanja na nyumba maeneo mbalimbali ya Nairobi na hata inadokezwa kuwa sehemu fulani za Tanzania.. Je, tunajua nini kuhusu kuingia kwa sympathizers wa Al Shaabab nchini?

Ni kweli kuwa ujenzi wa eneo moja huko maeneo ya Bahari Beach nje ya jiji la Dar yumkini unahusiana na masuala haya ya Al-Shaabab?
 
Mkuu gharama za kuteka meli moja ni around 500,000.USD. Hapo ni ununuzi wa silaha,ngazi,mishahara,vyakula,boti,mafuta na mengineyo. Zoezi zima huwa linaratibiwa hapo Eastleigh, Nairobi. Ebu fikiria wanapofanikiwa kuteka meli wanadai dau kubwa kuanzia 20m USD na kuendelea! Vipi hapo inalipa?
 
pia wanatumia sana watu wanaoibukia kwenye biashara, na ku-inject capital kiasi kikubwa tu, wao wanakua behind the scene. ila vilevile wanatumia circles za baadhi ya wanasiasa kufanikisha hayo
 
Sasa fedha hizo zinapotua katika nchi kama yetu yenye uchumi teke teke mifumuko ya bei ndo usiseme - nasi na ufahamu wetu tunasingizia uzalishaji mdogo wa kilimo bila kujua umesababishwa na nini ukiacha hujuma za Tanesco ambazo zimechangia katika kushusha tija za sekta mbali2 nchini.
 
Hata Mimi nikiwajua na wakiniamini napiga kazi (liwalo na liwe) nahisi tz ni Mimi na wewe tuu ndio tunebskia bila kitu na nshaona ahadi za JK hazitimii za maisha bora badala yake anasema tujitume ivo Mimi nikipata connection najituma kiukweli kuna mwenye contact zao jamani anipe? Maana bongo sasa imebaki get rich or die as slave...
 
Yes MMM, the guys just invest on real estate and wananunua most of things cash and they have strong circles na wamepenya hadi kwenye kiini cha salama yetu!!
Hapa tunarudi kwenye mduara wa kuchakachuliwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama!
 
Ukitaka kujua jinsi hela zinavyotakatishwa nusa pale Mcsoms Bureau de change.
 
MM afadhari umelianzisha hili. Napenyeza taarifa hii kwa ajili ya uchambuzi na uchunguzi kwa waliojikoni: Fuatilieni Mtu mmoja anaemiliki chains za hotel hapo jijini Dar es Salaam na pia Mzee mmoja anayejiita mshauri wa Chama fulani na katika chaguzi fulani zilizopita alikuwa kampeni manager... ambaye kiutaifa, anashabihiana sana na huyu mmiliki wa hayo mahotel, ndipo mtakapoelewa kwa nini hawa Al-Shaabab ni kama invisible..(Yaani hawaonekani ila wanasikika tu)
Waogopa nini kuwataja majina na huku umetumia jina bandia hapa JF? Wwataje ili tujadili hoja vizuri.
 
Mimi naona watu tupo mesmerized na discourse za nchi za magharibi kwa kuziita hizi fedha ni fedha chafu. Naomba tudiscuss zipi ni fedha safi, je ni zile tunazokopeshwa na World Bank na IMF kwa masharti magumu ya kuzirudisha?. Je tunajua nchi zinachangia fedha kwenye hayo mashirika zinakozitoa, kama siyo kwa biashara chafu za mafuta na vita kwa nchi maskini.

Hivi money laundaring inakuwa tu pale ambapo fedha zikiporwa kutoka nchi za magharibi kwenda nchi maskini na kwa nini haiwezi kuwa viseverser?. Watu wanapola fedha nchi zinazoendelea na kuzipeleka Uswisi kwenye mabank na huko zinakopwa na wafanyabiasha hiyo siyo money laundry?

Kwani hiyo fedha sio chafu?. Nani leo hajui kuwa Vatiacan ndio mji unaoongoza kwa money laundaring?. Kwa nini wasianze kusafisha fedha chafu zote zinazoporwa kutoka nchi maskini ambazo zinahifadhiwa Geneva, Zurich, Frankfurt, NewYork n.k
Hebu waafrica nasi tubadilike, hizi terminology zingine zimewekwa maksudi kuhakikisha kila fedha inayokuja nchi maskini lazima iwe 'halali' and not otherwise, wakati mali zetu zinaporwa kwa kila hali, ikiwa ni pamoja na kukwepa kodi na kupora madini huku hayo mambo tukiaminishwa ni halali.

Sipendi kitendo cha maharamia kuteka watu na kuwauwa kwa ajili ya fedha ila kitendo cha kuteka meli za mizigo na kutumia mzigo kublackmail nchi za magharibi na hizo fedha kuzitumia kujenga majumba ni kitendo cha kishujaa kama vile wapiganaji wa US wanavyopongezwa kwao baada ya kuisambaratisha Iraq na kuweza kumiliki uchimbaji wa mafuta kwa manufaa yao

Ifike kipindi tutambue kuwa miji mingi inayosifika dunia imejengwa kwa fedha chafu, refer to biashara ya utumwa na kushamiri kwa taifa la Marekani, what about plunder piracy during mechantalism na kukuwa kwa taifa la Uingereza, Netherlands etc.Pia tujaribu kusoma kitabu cha THE ECONOMIC HIT MAN jinsi kinavyoelezea kukuwa kwa miji ya Urabuni kama Dubai, Doha, hasa wakati wa Utawala wa Regan ili kuthibitisha jinsi gani fedha inayoitwa chafu inavyojenga miji
,

NB- Kwa anayehitaji softcopy ya The Economic Hitman anipm
 
Back
Top Bottom