Al-Shaabab/Maharamia wa Somalia wanabadilisha vipi fedha haramu Afrika ya Mashariki?

Maswali mazuri kabisa, unafikiri yawezekana wanatumia fedha zote hizo bila kuwa na faida maana itakuwa ni biashara uchwara hii. Baada ya gharama zote hizo za msingi (kwa maoni yao) kinachobakia wanafanya nacho nini na hata kama ni chakula wananunua wapi, magari yanaingiaje. Hapa kwa kweli unaingiza elements muhimu sana. Thanks
...Labda tujiulize, je, wapiganaji wa kiislamu wenye siasa au mtazamo mkali wenye ujuha, wanafikiria faida katika maana ya fedha? au wanaamini kuwa wanapigana vita takatifu au wanapigania maana takatifu?

...Kama wanafikiria faida katika minajili ya fedha, basi "cause" yao haina maana na wao ni watafutaji tu, kama wafanyabiashara au majangili wengine, ila, wanafanya kimafia zaidi kabisa na imani ya uislamu imechukuliwa mateka.
 
Al-shabab hawana ugomvi kabisa na Kenya wala serikali za Ukanda huu. Kwani hata hao watalii waliotekwa huko mpakani mwa kenya na somalia upande wa kenya haukufanywa na Al-shabaab, hizo ni mbinu za serikali ya kenya walizopewa na marekani ili wapate support kutoka kwenye nchi za Magharibi. Kwa ujanja wa America, hawakuruhusu kwenye jaribio hilo atekwe raia wao, na kuwarushia mpira mataifa ya ulaya. Kwa sasa America wametulia na kuwaangalia hao wafaransa waingie kwenye vta hiyo ya hasara!
 
Jamani Watanzania wenzangu,wapendwa wana JF,yanayofanyika hapa TZ nyuma ya pazia ni makubwa sana na laiti tungebahatika kuyaona,sijui ingekuwaje.Siwezi kupinga kabisa suala la kuwepo fedha haramu za maharamia na maharamia wenyewe ama ndugu zao hapa Tanzania,nina rafiki yangu jina ( ) anafanyia Uhamiaji hapa DSM makao makuu kule posta,amenipasha wanapo piga doria au wakipata ramani au taarifa ya kuwepo kwa watu hao,huwa wanafuatilia na wanahongwa hela nyingi sana,jamaa anamaisha safi lakini mshahara wake haufiki hata laki 3,wanao leta ligi na walete lakini habari ndo hiyo.
 
Kwa sababu swali kubwa ni kwamba hawa jamaa wanalipwa hayo mamilioni ya kuachilia mateka wao wanazitumia hizo fedha wapi? kwa uhakika sidhani kama itakuwa Ethiopia...
Yes Wasomali wengi wanainvest Ethiopia siku hizi lakini wako strict kujua katoka wapi na hela katoa wapi e.g. hawa wanaorudi Africa kutoka Ulaya/Marekani,Waliokimbia vita,Uarabuni.

Maswali mazuri kabisa, unafikiri yawezekana wanatumia fedha zote hizo bila kuwa na faida maana itakuwa ni biashara uchwara hii. Baada ya gharama zote hizo za msingi (kwa maoni yao) kinachobakia wanafanya nacho nini na hata kama ni chakula wananunua wapi, magari yanaingiaje. Hapa kwa kweli unaingiza elements muhimu sana. Thanks
Mwanakijiji hata western intelijence wameshindwa kuwa-link Al-shabaab na piracy,piracy bases nyingi ziko kuanzia maeneo kama 300km north of Mogadishu mpaka mlango wa Red Sea nje ya eneo lao ambao ni kuanzia Mogadishu mpaka mpakani na Kenya,na pia Al-shabaab wameonyesha wazi kuwakataa pirates kwenye ports wanazo miliki kama Kismayu.
Yes Al-shabaab are linked to al-qaida,yes Al-shabaab are dangerous tuwe waangalifu na watu/mali inayoingia lakini tusi-wavictimize watu wenye nia njema ya ku-invest na kufanya biashara halali.
 
Yes Wasomali wengi wanainvest Ethiopia siku hizi lakini wako strict kujua katoka wapi na hela katoa wapi e.g. hawa wanaorudi Africa kutoka Ulaya/Marekani,Waliokimbia vita,Uarabuni.

Mwanakijiji hata western intelijence wameshindwa kuwa-link Al-shabaab na piracy,piracy bases nyingi ziko kuanzia maeneo kama 300km north of Mogadishu mpaka mlango wa Red Sea nje ya eneo lao ambao ni kuanzia Mogadishu mpaka mpakani na Kenya,na pia Al-shabaab wameonyesha wazi kuwakataa pirates kwenye ports wanazo miliki kama Kismayu.
Yes Al-shabaab are linked to al-qaida,yes Al-shabaab are dangerous tuwe waangalifu na watu/mali inayoingia lakini tusi-wavictimize watu wenye nia njema ya ku-invest na kufanya biashara halali.

Nimekupata.. so huwezi kuhisi uhusiano wa maharamia hao na Al-Shaabab?
 
Jamani Watanzania wenzangu,wapendwa wana JF,yanayofanyika hapa TZ nyuma ya pazia ni makubwa sana na laiti tungebahatika kuyaona,sijui ingekuwaje.Siwezi kupinga kabisa suala la kuwepo fedha haramu za maharamia na maharamia wenyewe ama ndugu zao hapa Tanzania,nina rafiki yangu jina ( ) anafanyia Uhamiaji hapa DSM makao makuu kule posta,amenipasha wanapo piga doria au wakipata ramani au taarifa ya kuwepo kwa watu hao,huwa wanafuatilia na wanahongwa hela nyingi sana,jamaa anamaisha safi lakini mshahara wake haufiki hata laki 3,wanao leta ligi na walete lakini habari ndo hiyo.
Tusichanganye mambo wewe unaongelea wazamiaji haramu ambao wengi huwa wanapita wakielekea South Africa na wengine kufanikiwa kuchukuliwa na Marekani/Canada kutoka S.A,na sidhani kama Marekani/Canada watachukua wafuasi wa Al-shabaab.Wasomali ni watu wenye umoja na mara ingine husaidia kuwavusha wakimbizi hawa wanaoelekea South na pindi wakamatwapo huchangishana hela za kuwatoa mikononi mwa vyombo vya dola.Mkiona wanaoonyeshwa kwenye TV au kuandikwa magazetini mjue aidha hawana ndugu au hawajahahusisha ndugu au walikuwa wengi na soo lilishindwa kuzimwa.
 
Nimekupata.. so huwezi kuhisi uhusiano wa maharamia hao na Al-Shaabab?
Mkuu nakuhakikishia maharamia na Al-shabaab hawaivi kwenye chungu kimoja infact Al-shabaab wanawalaumu hawa pirates kwa kuwajazia meli na ndege za Nato baharini/Djibuti ambao wenyewe imewaathiri kwa kufatiliwa kwa karibu na kushindwa kuingiza silaha Somalia.
Utakuja kukumbuka kauli hii yangu Al-shabaab hawajahusika na utekaji nyara wa Watalii/Wafanyakazi wa nchi za Magharibi nchini Kenya na ukweli utakuja julikana tu.
 
Mawazo ya kijinga tu na kichoyo na kutumwa kusema jambo usilolijua undani wake.
Kwa maelezo yako ni pesa gani hazifanyi hizo kazi ulizoziorodhesha.
Halafu unatilia shaka kazi za vyombo vya usalama. Ikiwa ni hivyo hiyo kazi tukupe wewe utuoneshe ushahidi wa kuhamishwa hizo fedha za utekaji meli.Usipoweza wewe ni mtu hataari na mbaya kuliko hata hao Alshabaab.Huna maana kabisa katika jamii ya watu wastaarabu.Ukiwa na nia mbaya naomba Mungu akudhibiti mapema kabla hujaleta balaa katika jamii.
What??!! Kilichokosewa hapa ni nini? Kuueleza umma kinachoendelea nchini na nchi jirani au lipi baya hapa? Jamani wakati mwingine watu tuwe waungwana kidogo hizi lugha za jazba sidhani ni msaada kwa jamii. Mimi nadhani ulipashwa kukakanusha kwa lugha ya kistaarabu na vielelezo sio kukurupuka tu na kumwita mwenzio mjinga. Hili ni jukwaa la kujuzana, kuelimishana na zaidi kujenga udugu kama watanzania.
 
MM afadhari umelianzisha hili. Napenyeza taarifa hii kwa ajili ya uchambuzi na uchunguzi kwa waliojikoni: Fuatilieni Mtu mmoja anaemiliki chains za hotel hapo jijini Dar es Salaam na pia Mzee mmoja anayejiita mshauri wa Chama fulani na katika chaguzi fulani zilizopita alikuwa kampeni manager... ambaye kiutaifa, anashabihiana sana na huyu mmiliki wa hayo mahotel, ndipo mtakapoelewa kwa nini hawa Al-Shaabab ni kama invisible..(Yaani hawaonekani ila wanasikika tu)
 
Mawazo ya kijinga tu na kichoyo na kutumwa kusema jambo usilolijua undani wake.
Kwa maelezo yako ni pesa gani hazifanyi hizo kazi ulizoziorodhesha.
Halafu unatilia shaka kazi za vyombo vya usalama. Ikiwa ni hivyo hiyo kazi tukupe wewe utuoneshe ushahidi wa kuhamishwa hizo fedha za utekaji meli.Usipoweza wewe ni mtu hataari na mbaya kuliko hata hao Alshabaab.Huna maana kabisa katika jamii ya watu wastaarabu.Ukiwa na nia mbaya naomba Mungu akudhibiti mapema kabla hujaleta balaa katika jamii.

Wewe unayepinga tupe ushahidi wa hicho unachopinga kwa nguvu hadi unatoa mapovu mdomoni, Umeguswa nini!!! Yaani hilo swala huhitaji kutumia degree kuchunguza, vyombo vya Usalama ndiyo kazi yake na wanalipwa kodi zetu kwa kazi hiyo, hivyo hatutegemeei kuona nchi inaelekea kubaya wakati kuna watu wamepewa dhamana ya kuilinda !! na wamepewa vyezo na fedha za kutosha.

Na wasiwasi na wewe kama siyo msomali basi Alshababu wa tanzania, unayefanya mipango ya kuelekeza meli zipo wapi . Juzi mmeingia kuteka meli ya utafiti wa mafuta East Mafia bahati mbaya mkakutana na wazee wa kazi Navy TZ wakawafanyia mazoezi, na wale waliokamatwa wanatoa siri zote mtakamatwa wote including you Ami!!!
 
Kwamba Al Shaabab wamekuwa wakipata mamilioni ya dola kutokana na shughuli za uharamia huko Somalia. Lakini dalili zote zinaonesha kuwa fedha hizo huhamishwa na kuingizwa katika mifumo ambayo itazisafisha fedha hizo na kuzifanya halali. Hii ni pamoja na kununua viwanja na nyumba maeneo mbalimbali ya Nairobi na hata inadokezwa kuwa sehemu fulani za Tanzania.. Je, tunajua nini kuhusu kuingia kwa sympathizers wa Al Shaabab nchini?

Ni kweli kuwa ujenzi wa eneo moja huko maeneo ya Bahari Beach nje ya jiji la Dar yumkini unahusiana na masuala haya ya Al-Shaabab?

tick tock..... acha tu sijui watu wana amnesia, na documents za Bahari ziliwekwaga humu kipindi flani...swali zito hili umegusia.
 
Hivi vikundi vya Al shaabab na venginevyo ni machine ya USA kwa ajili ya kuifanya Africa, MidEast kuwa mahali pa vita tu bila ya amani. Hii ndiyo inaitwa New World Order.

Mchina sasa hivi anaitaka Africa, na keshaichukua Africa kiuchumi-investments kwa asilimia kubwa sana. Hivi unadhani Wazungu-West watakubali hivi hivi tu waikose Africa?

Dawa- ni kuanzisha vita ili mikataba mipya ianze kusaigniwa. Tumeona Libya-Wazungu walipoona wameshaanza kuikosa kwa Mchina- dawa ni regime change. Sasa hivi Libya ipo mikononi mwao.

Sasa hivi wanaitaka East Africa. Kwa nini? Kuna port kubwa inayoingiza na kutoa mali kwenda na kurudi kutoka China na Asia. Dawa- anzisha vita. Kama hamna amani hamna biashara.

USA tayari wanazo Drones-Attack ktk East Africa ambayo inaweza kuattak popote pale kama wakipata target ya Al shaabab.

Kazi tunayo EA. Hatuna Amani tena
 
Tatizo kubwa la nchi yetu sasa ni kufubaa kwa vyombo vya ulinzi na usalama ambapo sasa vimetekwa na mafisadi na vinafanya kazi kama matawi ya chama tawala ambacho kwa bahati mbaya kimeshakuwa corrupted na virusi vya ufisadi, udini na ukabila. Ni ukweli usiofichika kwamba asasi muhimu kama za TSS, TAKUKURU, Polisi, Uhamiaji na nyingi nyinginezo zinafanya kazi kwa mdundo wa CCM! Zamani tulikuwa na tumaini na asasi moja tu iliyoonekana imara bila kuyumbishwa kisiasa, nayo ilikuwa ni JWTZ ambayo hali inavyoelekea sasa inaashiria kuingizwa kwenye mduara wa CCM ushahidi mmojawapo ni pale kiongozi wao mkuu alipokurupuka, kuweweseka na kumwaga upupu mbele ya watanzania wa eti JWTZ isingevumilia "Fujo" katika uchaguzi uliopita na ingechukua hatua kulinda usalama! Utadhani yeye ndiye IGP. Ukweli kwamba hakukemewa wala kusahihishwa na wakuu tuliowakabidhi nchi hii ni uthibitisho wa wazi kutumiwa na vibaka wa CCM. Baadae tulishuhudia magari ya Jeshi yakitumiwa "kusambaza na kukusanya" masanduku ya kura ambapo kilichoendelea kinaeleweka na sote; ndiyo kutengeneza matokeo ya Urais na ubunge katika uchaguzi uliopita. Wasiwasi wangu ni kwamba kutokana na asasi hizo kufanya kazi kisiasa zadi tena kwa mujibu wa chama kinachonuka uvundo wa rushwa lolote linawezekana, yaani Al shabaab na hata Al Qaida wanaweza kabisa kujipenyeza na kufanya lolote kwa nguvu ya pesa zao chafu bila asasi hizi kuchukua hatua. Mwenye akili yeyote atajihoji ni kwa vipi katika miji mikubwa kama Dar, Arusha na Mwanza wawekezaji wanaonunua viwanja na kujenga majumba makubwa na ya kifahari ni waarabu na wasomali? Na wazipataje fedha za kufanyia "kufuru" hiyo kama hazina mkono mchafu? Hayo yakitendeke TSS wamelala au labda wanasubiri filimbi ya CCM ndiyo waamke washughulike! Ama kweli tumekwisha. Mungu ibariki Tanzania.
 
Mawazo ya kijinga tu na kichoyo na kutumwa kusema jambo usilolijua undani wake.
Kwa maelezo yako ni pesa gani hazifanyi hizo kazi ulizoziorodhesha.
Halafu unatilia shaka kazi za vyombo vya usalama. Ikiwa ni hivyo hiyo kazi tukupe wewe utuoneshe ushahidi wa kuhamishwa hizo fedha za utekaji meli.Usipoweza wewe ni mtu hataari na mbaya kuliko hata hao Alshabaab.Huna maana kabisa katika jamii ya watu wastaarabu.Ukiwa na nia mbaya naomba Mungu akudhibiti mapema kabla hujaleta balaa katika jamii.

acha mawazo tope kwa kujifanya wewe ni muislamu peke yako na kuwatetea wasomali magaidi,even me am i muslim bt i hate them maana wanapopiga bomu wanaua wa2 wasio na hatia
 
Al-shabab hawana ugomvi kabisa na Kenya wala serikali za Ukanda huu. Kwani hata hao watalii waliotekwa huko mpakani mwa kenya na somalia upande wa kenya haukufanywa na Al-shabaab, hizo ni mbinu za serikali ya kenya walizopewa na marekani ili wapate support kutoka kwenye nchi za Magharibi. Kwa ujanja wa America, hawakuruhusu kwenye jaribio hilo atekwe raia wao, na kuwarushia mpira mataifa ya ulaya. Kwa sasa America wametulia na kuwaangalia hao wafaransa waingie kwenye vta hiyo ya hasara!

Wale waliolipuliwa na mabomu pale Kampala katika fainali ya kombe la Dunia hawakulipuliwa na Alshabab?
 
Mawazo ya kijinga tu na kichoyo na kutumwa kusema jambo usilolijua undani wake.
Kwa maelezo yako ni pesa gani hazifanyi hizo kazi ulizoziorodhesha.
Halafu unatilia shaka kazi za vyombo vya usalama. Ikiwa ni hivyo hiyo kazi tukupe wewe utuoneshe ushahidi wa kuhamishwa hizo fedha za utekaji meli.Usipoweza wewe ni mtu hataari na mbaya kuliko hata hao Alshabaab.Huna maana kabisa katika jamii ya watu wastaarabu.Ukiwa na nia mbaya naomba Mungu akudhibiti mapema kabla hujaleta balaa katika jamii.

Nadhani tumekwisha prove uwepo wao.....ona hoja ya huyu mtu,aifanani na thread ila kaja kuleta mambo yake yasiyo na kichwa wala mkia...
 
Sasa yawezekana hawa jamaa wa Al-Shaabab wakafanya kitu mbaya Tanzania kama tukichukua msimamo mkali dhidi yao? Kama kuungana na Kenya kwenda kuwa flush out?
 
Kuna tetesi kuwa majumba yananunuliwa na kujengwa na hawa ndugu zangu halafu hayana wakaaji. Ile biashara inawalipa kweli. Na hapo naelewa kwanini Shabaab wanakomaa namna hii kwenye mambo yasiyohusiana kabisa na dini, kuteka na kuua watu wasio na hatia!
 
Mawazo ya kijinga tu na kichoyo na kutumwa kusema jambo usilolijua undani wake.
Kwa maelezo yako ni pesa gani hazifanyi hizo kazi ulizoziorodhesha.
Halafu unatilia shaka kazi za vyombo vya usalama. Ikiwa ni hivyo hiyo kazi tukupe wewe utuoneshe ushahidi wa kuhamishwa hizo fedha za utekaji meli.Usipoweza wewe ni mtu hataari na mbaya kuliko hata hao Alshabaab.Huna maana kabisa katika jamii ya watu wastaarabu.Ukiwa na nia mbaya naomba Mungu akudhibiti mapema kabla hujaleta balaa katika jamii.

mkuu mbona povu limekutoka?
 
Back
Top Bottom