Akutwa na ngozi ya mtu huko Mbozi - Je tutafika na hali hii?

Quote:
Originally Posted by Bongolander
Du hiyo kali, kuna nini huko Mbeya? Ajabu ni kuwa nasikia Mbeya ni mkoa wenye makanisa mengi kabisa Tanzania, na ni mkoa wenye matukio makubwa kabisa ya kutisha, wanaJF wa Mbeya mtueleze kidogo kulikoni huko.

Quote:
Originally Posted by Mtanzania
Bongolander,

Unaulaumu mkoa wote kwa makosa ya wapumbavu wachache? Inatakiwa watu kama hao mkong'oto wa nguvu utembee. Hayo yote ni matokeo ya ujinga na siasa mbovu za kushindwa kuwaendeleza watu wetu.

Mie nikaandika:-
Unaona sasa haya mambo? Wametajwa Watu wa Mbeya. Hilo kweli tusi kwa mkoa mzima. Kuna watu wengine na dini zao au sehemu watokapo zingelikuwa zimetajwa basi ungelisikia "uombe msamaha..." Ataacha yote yaliyoandikwa na kushupalia kipointi kidogo tu au kitu ambacho hata si muhimu katika huo ujumbe. Nashukuru Mtanzania, pamoja na kuseme "usilaumu mkoa mzima", bado kaendelea na yeye kulaani kitendo hicho na hivyo kutoibadili hii habari. Hapa wangelikuwa wenyewe basi saa hizi ungelisikia "sisi Wamoravian wa Mbeya inabidi utuombe msamaha....."
Naungana na mie kulaani huu ushamba. Inabidi kweli hawa watu waende jela na kupigwa viboko 30 kila mwezi kwa miaka sawa na umri wa mtu waliyemchuna ngozi ukitoa kwa 100. Akiwa mtoto ndivyo miaka inavyozidi kuwa 100.

Chinkala,
Ukisoma tena hiyo habari juu utajua kwa nini nilisema hayo maneno. Ila mwenzangu naona umedandika hii habari bila kuisoma yote na wakati huo unalaani kuwa mie sikuona tatizo. Heeee, nyani haoni siyo? Mie niliposoma ujumbe na kukuta kumbe ndiyo walikuwa wamepanga kwenda kufanya UCHUNAJI, nikaona hii habari FEKI. Niliamua tu kuandka baada ya kukuta mtu kashambulia mkoa na Mbeya na Mtanzania kajibu. Ila hakujibu na kubadili kabisa topic. Kama ukiangalia aliendelea na hii habari bila ya kuanza kulalama ohh, sisi wa Mbeyaaaaaa......
Sasa watu wanaoharibu hizi topic naona na wewe ni mmoja wapo. Tunaongelea Uchunaji wa ngozi na watu kusema MKOA WA MBEYA. Wewe umekuja hapa na kuanza HONGERA MAMA kwa kufikisha post 2k kwa miezi 7. Mara ohh, mama nakuhusudu. Hivi kuna uhusiano gani kati ya MAMA NAKUHUSUDU au POST 2k na hicho kichwa cha habari na habari yenyewe ingawa na ya ovyo.
Unanikumbusha mtu aliyeulizwa "Ubongo ni nini?" Ahh Ubongo ni kama HD kwenye computer. Hii huwa inawekwa kwenye body ya computer. Ndani ya computer kuna motherbody, RAM, CD rom, Graphic card na pembeni kuna Processor na juu yake kuna feni ........... "Ehhhh, comedown, jibu UBONGO NININI."

NB:- Acha kutafuta wanawake kwenye Mitandao. Utaja pata kaka poa kama mwenzio Ronaldho yaliyomkuta Brazil. Ukikwama kabisa, njoo Sikonge nikupatie mmoja.....
 
.......dah washikaji........hii ya ngozi kali.......nalaani watu wote wanaojihusisha na upumbavu huo..........wanastahili kunyogwa hadi kufa or life in jela......viboko ni adhabu ndogo sana kwa maoni yangu...............
 
Ukisoma vizuri utajua anazunguzmzia wakina nani, ndio mie ni mmoja wao na ninaungana na Mtanzania kusema kwamba mambo ya generalizations ya kome.

Imeoza ktk press na kila kitu mpaka sehemu kubwa ya watu wake, imeoza na inanuka JANABA. Ukitaka kuona uozo huo, mfano ktk hii thread, watu wanajadili mtu kukamatwa na ngozi....wakati habari inasema walikuwa wameandaa mtu wa kumchuna!! Mwandishi kawaingiza kingi, kwasababu wanatabia ya kukurupuka na ma-emotions mengi, wanaanza kujadili kitu ambacho hakipo na mwingine anachukua fursa hiyo kupiga donge dini na kabila za wengine....huo ni uozo wenyewe!!!.

Heheheeee Chinkala,
Ni kweli ukisoma vizuri utajua ninaongelea watu gani. Tatizo nimeandika kuwa wengine wangelisema "..ohhh Sisi Wamoravian umetusema, utuombe msamaha..". Wamoraviani ni wengi sana Mbeya na Sikonge. Mie na Mtanzania ni kanisa hilohilo. Najua ulisoma na ukapata hamu sana ya kutaka niseme ni dini fulani ili upate mwanya wa kutokea. Bahati mbaya mie ndiyo kwanza nilizidi kuongeza Nondo na Zege na high class (B60) na hapo hakipiti kitu. Na Zege lenyewe ni Acid resistance na kwa mwendo huo hizo TINDIKALI zako ukiweka hazipati kitu, lete na maji ha bahari hamna kitu. Hata JANABA halifukuti hapa. Wanasema kama huwezi kumshinda, ungana naye. Nipe basi walau hongera kwa hilo.

NB:- hivi JANABA ni nini? Wengine sisi washamba wa huku Sikonge hatujui haya manano ya kiswahili kisawasawa.
 
Vitu kadhaa vinanitatiza:
1. Kuna Mkuu amesema tusiwaonee hawa wanafanya biashara ya ngozi kwa sababu wanaiga viongozi wao!
2. Kwa vile watuhumiwa walikuwa wanatafuta dili kwanza kabla ya kwenda kumchuna mtu basi si waovu!

Kweli tutafika hivi?

Fundi Mchundo,
Mie huwa nina kawaida ya kwenda ninasoma maneno kwenye nguo za watu. Sasa katika pitapita siku moja nikaona jamaa kavaa T-SHIRT imeandikwa :-
USIIBE KWANI SERIKALI HAIPENDI USHINDANI.

Inawezekana MKUU alikuwa anataka kusema kuwa tatizo liko juu sana na hawa watu wajiangalie kwani hii ni shughuli ya Vigogo tu. Na ukikamatwa una hali mbaya. Kwa maana nyingine inabidi kutengeneza T-Shit yenye maneno:-
USICHUNE WATU NGOZI, SERIKALI HAIPENDI USHIDANI.
 
Vitu kadhaa vinanitatiza:
1. Kuna Mkuu amesema tusiwaonee hawa wanafanya biashara ya ngozi kwa sababu wanaiga viongozi wao!
2. Kwa vile watuhumiwa walikuwa wanatafuta dili kwanza kabla ya kwenda kumchuna mtu basi si waovu!

Kweli tutafika hivi?

Hapa nafikiri tuwe focused!!!!!!! haya masuala ya ushirikina hayapaswi kukubalika kwa namna yoyote ile. huwa yanabadilika kama upepo kutokana na uvumi tu. kuna kipindi ngozi ya binadamu inakuwa biashara nzuri - sasa hivi tunashuhudia viungo vya Albino ndiyo zaidi. kesho hatujui kitugani kitakuwa biashara nzuri. huenda wakahitaji kiungo chochote kutoka kwa yoyote!!! who knows.
Suala kubwa hapa ni kujadili/kuelimishana namna gani nzuri ya kukabiliana na haya matendo maovu
Viongozi wetu hasa wanasiasa wanatumia nguvu za giza zaidi katika kuongoza kuliko hata nguvu za waliowachagua, na huenda inachangia viongozi wasiwajali wananchi wake wakawajali zaidi waganga wao wa jadi.
USHIRIKINA unapaswa utoweke kabisa kwenye jamii zetu ili tuweze kupiga hatua kimaendeleo (kisayansi)
 
Tatizo lako unatumia uwezo wako wooote wa kufikiria wakati una post pumba zako hapa JF..ama kweli waTZ ni vituko na li-nchi limeoza na kunuka janaba.

Kama ulijua nyuzi ni feki kwanini hukusema? hiyo peke yake inaonyesha wewe ni mtu wa namna gani...pole sana na nakutakia wk njema.:)

Chinkala,
Ahoi. Janaba ni nini? Duu, naona hili neno unalipenda sana. By the way unaongea safi sana kijana wangu mzoefu. (Ahoi, Kiczeck hicho maana sisi Moravian na Pilsner tunatokea huko.)
 
Tafuta kamusi, we vipi?
Chinkala,
Wewe unafikiri kila mtu yuko mjini kama wewe? Huku Sikonge hata Maktaba hamna. Nilienda uliza kwa KATIBU KATA akasema hana. Mwalimu mkuu na walimu wake wanazo ila hilo neno hamna maana zao ni ndogo sana. Baada ya kuanza sumbua watu si ueleze tu maana yake ni nini?
HEJ DO.
 
Back
Top Bottom