Akutwa na mabomu manne ya kutupa kwa mkono

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Na John Makambo, Tabora JESHI la Polisi mkoani Tabora, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Ilolangulu, Kata ya Ilolangulu Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, kwa tuhuma za kukutwa na mabomu manne ya kutupa kwa mkono.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, ACP Antony Rutta, alieleza kuwa, kulingana na taarifa zilizolifikia jeshi hilo, mabomu hayo yalikuwa yatumike kwa ajili ya kufanya shambulio ama utekaji katika mnada.

Alimtaja anayeshikiliwa kwa tuhuma hizo ni Nsimbi Masaki, ambaye alikuwa ameyahifadhi mabomu hayo katika mfuko wa sandarusi na kuyafunga pia kwa kutumia mfuko wa Rambo na kisha kuyachimbia chini.

Alisema taarifa za kiintelijensia zinabainisha kuwa, mabomu hayo yanaweza kuwa yameingia nchini kupitia nchi jirani, ambayo hakuweza kuitaja.

Alisema, jeshi hilo linaendelea kuchunguza jinsi mabomu hayo yanavyoweza kuingia nchini na kwamba mtuhumiwa huyo anatarajia kufikishwa mahakamani mara baada ya mahojiano kukamilika.

Wakati huo huo jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa mmoja kutokana na tuhuma za kukutwa na silaha ya gobole, ambalo linauwezo wa kutumia risasi za bunduki ya Shortgun.

Kamanda Rutta alisema kuwa, katika tukio jingine watu 8 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mali zinazodhaniwa ni za wizi.

Mali hizo ni pamoja na seti moja ya tv, radio na mapanga ambayo wanadhaniwa kuyatumia kwa ajili ya kupora ama katika matukio ya ujambazi.
 
hii Tanzania nayooo
Sasa hao hawaoni hata huruma kutaka kutumia hayo kwa ajili ya mambo yao binafsi hivi huwa hawajui kuwa sisi ni wati tunahitaji kuishi kama wao wanavyohitaji? Nashindwa elewa uelewa wa hawa wanao kamatwa na mabomu risasi wawe wanapimwa akili na kuombewa ukute wengine wagonjwa kwani kama unaufahamu huwezi taka fanya kitu kama hiyo
 
Huyo mzembe. Mimi mbona nina mabomu ya aina hiyo na sikamatwi? Kwa ilipofikia nchi hii,mabomu na bunduki ni muhimu
 
Huyo mzembe. Mimi mbona nina mabomu ya aina hiyo na sikamatwi? Kwa ilipofikia nchi hii,mabomu na bunduki ni muhimu


aiseee baba yangu 2naweza za badilishana hayo mabomu na mbege lita 50 nataka niatumie hayo mabomu 2015 kuwalipuwa magamba
 
Back
Top Bottom